Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2005-04-01 15:49:44    
Uchaguzi wa bunge la Zimbabwe wamalizika katika hali ya utulivu

cri

Uchaguzi wa bunge la Zimbabwe ulifanyika tarehe 31 mwezi Machi. Ukilinganishwa na uchaguzi uliofanyika katika miaka mitano iliyopita, uchaguzi huo ulifanyika katika hali ya utulivu. Migogoro mikubwa haikutokea nchini humo wakati wa kampeni ya uchaguzi na wakati wa upigaji kura. Wachunguzi wanaona kuwa, hii imeonesha kuwa wananchi wa Zimbabwe wamepevuka kisiasa.

Wagombea kutoka vyama vitano na wagombea kadhaa wasio wa vyama walishiriki kwenye uchaguzi huo. Ushindani mkubwa ulikuwa kati ya Chama cha ZANU-PF na Chama cha MDC ambacho ni chama kikubwa cha upinzani nchini humo. Ushindani kati ya wagombea wa vyama hivyo viwili unaonekana katika sehemu zote 120 za uchaguzi nchini humo. Rais Robert Mugabe wa Zimbabwe ambaye pia ni mwenyekiti wa Chama cha ZANU-PF alipiga kura katika kituo kimoja mjini Harare. Baada ya kupiga kura alitoa hotuba fupi akieleza matumaini yake kuwa Chama cha ZANU-PF kitashinda kwenye uchaguzi huo.

Kuna viti 150 katika bunge la Zimbabwe. Wabunge 120 watachaguliwa kutoka sehemu mbalimbali, wakuu wanane wa mikoa ni wabunge bila kupigwa kura, wabunge 10 wanateuliwa na kamati ya watemi wa makabila, na wabunge 12 wameteuliwa moja kwa moja na rais. Uchaguzi huo ni uchaguzi wa kwanza baada ya serikali ya Zimbabwe kufanya mageuzi ya sera ya ardhi bila kujali shinikizo la kisiasa na kiuchumi la nchi za magharibi. Lengo la Chama cha ZANU-PF katika uchaguzi huo ni kupata theluthi mbili ya viti katika bunge, yaani kinatakiwa kupata viti 70 kati ya viti 120, ili kiweze itaweza kurekebisha katiba, kurejesha mfumo wa mabaraza mawili katika bunge na kuanzisha mfumo wa utawala wa baraza la mawaziri. Uchaguzi huo umeonesha kuwa, utawala wake hautabadilika, vizuizi vilivyowekwa na nchi za magharibi vimekuwa bure. Aidha, theluthi mbili ya viti katika bunge vitaimarisha uungaji mkono wa nchi za Afrika hasa jumuiya ya maendeleo kusini mwa Afrika (SADC).

Mageuzi ya sera ya ardhi yaliyotekelezwa mwaka 2000 nchini humo yalizikasirisha nchi za magharibi ikiwemo Uingereza. Uingereza na Marekani zilitangaza kuiwekea vikwazo vya pande zote katika sekta ya kiuchumi, na kumshinikiza Rais Mugabe kujiuzulu. Katika uchaguzi wa tano uliofanyika mwaka 2000, kura zilizopatikana za Chama cha ZANU-PF zilipungua kwa kiasi kikubwa, na kilipata viti 62 tu kati ya viti 120, na Chama cha MDC kinachoungwa mkono na nchi za magharibi kilipata 57, na kikawa chama kikubwa katika bunge.

Baada ya miaka mitano, athari ya kisasa ya Chama cha MDC imepungua kidogo, na hadhi ya Chama cha ZANU-PF imeimarishwa zaidi. Katika kampeni ya uchaguzi huo, chama hicho kilichukuliaa uchaguzi huo kama ni mapambano ya kumpinga waziri mkuu wa Uingereza Bw. Tony Blair na kumshinda kibaraka chake yaani Chama cha MDC. Kauli mbiu hiyo ina nguvu kubwa ya kuwahamasisha wananchi. Zimbabwe ilikuwa koloni la Uingereza, Wazimbabwe walipata uhuru baada ya mapambano ya miaka 20. Lakini Uingereza ilisema wazi kuwa itashirikiana na Chama cha MDC na kuiangusha serikali ya sasa, hivyo Chama cha MDC kimepoteza uungaji wa mkono nchini Zimbabwe. Vyombo vya habari vinaona kuwa, wananchi wa Zimbabwe wataunga mkono Chama cha ZANU-PF ili kuonesha nia yao ya kulinda uhuru wa taifa na kupinga nchi za nje kuingilia mambo ya ndani ya nchi hiyo.

Aidha, katika miaka ya karibuni, watu wengi zaidi wanaona kuwa, Chama cha MDC ni chama ambacho hakina ushirikiano mkubwa na shabaha wazi ya kimkakati, na hakiaminiki. Katika miji mikubwa inayodhibitiwa na chama hicho ukiwemo Bulawayo, uchumi na maisha ya wananchi hayakupata maendeleo makubwa, hii imewafanya wapiga kura kutokiamini. Wachambuzi wanaona kuwa, Chama cha ZANU-PF kitashinda kwenye uchaguzi huo, lakini kitapata viti vingapi itajulikana baada ya uchaguzi huo.

Idhaa ya Kiswahili 2005-04-01