Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2005-04-04 20:44:24    
Kundi la upinzani la Rwanda FDLR latangaza kusalimisha silaha.

cri

Kundi kubwa la upinzani la kabila la Wahutu nchini Rwanda FDLR tarehe 31 lilitangaza huko Rome, mji mkuu wa Italia kusimamisha vita dhidi ya serikali ya Rwanda, kusalimisha silaha na kurudi nyumbani kutoka Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo. Hii ni mara ya kwanza kwa kundi hilo kueleza hayo tangu mwaka 1994 mauaji makubwa ya kikabila yalipotokea nchini Rwanda.

Kiongozi wa FDLR Bw. Ignace Murwanashyaka siku hiyo alitoa taarifa akishutumu mauaji makubwa ya kikabila yaliyotokea mwaka 1994 nchini Rwanda na kueleza kuwa kundi hilo litaweka chini silaha, kushiriki katika mchakato wa amani nchini Rwanda na kushirikiana na idara za sheria za kimataifa. Msemaji wa serikali ya Rwanda siku hiyo alisema kuwa serikali hiyo iko tayari kuwapokea askari wa FDLR warudi nyumbani, lakini alieleza pia, ni lazima kuwatia nguvuni watu wote walioshiriki kwenye mauaji hayo makubwa.

Mwaka 1994, mauaji makubwa yalifanywa na Wahutu dhidi ya Watusi nchini Rwanda, ambapo Watusi na Wahutu wasiopendelea upande wowote wapatao laki 8 waliuawa. Askari wengi wa FDLR waliojiunga na jeshi la serikali la Wahutu la Rwanda wakati huo wameshitakiwa kushiriki kwenye mauaji hayo. Mwezi Julai mwaka 1994, baada ya kundi la RPF la Rwanda lililoongozwa na rais wa sasa wa nchi hiyo, ambaye pia ni Mtusi Bw. Paul Kagame kuuchukua mji mkuu Kigali, askari wa FDLR walikimbilia sehemu ya mashariki ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, iliyo jirani na Rwanda. Sasa bado kuna askari wa FDLR wapatao elfu 15 hadi elfu 20 nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo.

Vyombo vya habari vinaona kuwa kundi la FDLR kutoa uamuzi wa kuweka chini silaha kunatokana na sababu mbili. Kwanza, serikali ya Rwanda iliitaka mara nyingi Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo inyang'anye silaha za FDLR na kutishia kuwa kama serikali ya nchi hiyo haitachukua hatua, serikali ya Rwanda italishambulia kundi la FDLR.

Pili, kutokana na kulazimishwa na Rwanda, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo na ujumbe maalum wa Umoja wa Mataifa katika nchi hiyo uliwahi kueleza kuchukua hatua ya kunyang'anya silaha za kundi la FDLR, hatua ambayo ililifanya kundi hilo halina budi kufikirie kuweka chini silaha na kushika njia ya amani.

Wachambuzi wanaainisha kuwa ingawa kundi la FDLR limetoa msimamo wa kuweka chini silaha, lakini kama askari wote wa kundi hilo wataweka chini silaha na kurudi nyumbani au la, ni jambo ambalo bado halijajulikani. Kwani askari wa kundi la FDLR wameshitakiwa kushiriki kwenye mauaji makubwa, ingawa wamekubali kuweka chini silaha zao, lakini serikali ya sasa ya Rwanda haitawasamehe. Serikali ya Rwanda sasa bado inawahukumu watuhumiwa walioshiriki kwenye mauaji hayo katika mahakama ya nchini humo. Kama askari wa kundi la FDLR watarudi nyumbani, sehemu kubwa ya askari hao watahukumiwa. Katika hali hiyo, ni shida kubaini kama askari hao watasalimisha silaha na kurudi nyumbani.

Idhaa ya kiswahili 2005-04-01