Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2005-04-01 19:46:05    
Watu wa kikundi cha kwanza waliojitolea kupewa chanjo ya ukimwi wanaendelea na hali nzuri

cri

Idara husika jana ilitoa taarifa ikisema kuwa, hivi sasa watu 8 wa kikundi cha kwanza waliojitolea kupewa chanjo ya ukimwi wanaendelea na hali nzuri, hakuna mtu yeyote aliyepatwa na tatizo mwilini.

Watu wanane wa kikundi cha kwanza waliojitolea walipewa chanjo ya ukimwi tarehe 12 March. Imefahamika kuwa, jaribio hilo linafuata utaratibu maalum, anayejitolea akiwa na hali mbaya, atasaidiwa kwa hatua mwafaka. Daktari anawasiliana nao kwa wakati, na idara husika imetunga mswada wa dharura ili kushughulikia hali ya dharura itakayowatokea waliojitolea.

Mwezi Novemba mwaka 2004, China iliidhinisha kufanya utafiti wa awamu ya kwanza kuhusu chanjo ya ukimwi kwa kufanya majaribio kwa mwili wa binadamu ili kutathmini usalama wa chanjo hiyo. Utafiti huo utakuwa na awamu tatu, ya kwanza itafanyika kwa miezi 14.