Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2005-04-01 20:17:14    
Mguinea Bw. Kuruma alivyouona urafiki kati ya China na Guinea

cri

Bw. Kuruma mwenye umri wa miaka 75 alikuwa ofisa wa ngazi ya juu wa Wizara ya Afya ya Guinea, na hivi sasa akiwa mbunge wa nchi hiyo bado ni mchangamfu sana katika jukwaa la mambo ya kijamii, na kupewa huduma na heshima mbalimbali.

Bw. Kuruma ana uzoefu mwingi kutokana na kujishughulikia na mambo ya kisiasa kwa miaka mingi, na jambo linalomfurahisha ni kutafuta na kutunza vitabu vya kisiasa, magazeti na matangazo kuhusu afya. Kutokana na hayo, moja ya matumaini yake ni kuanzisha Jumba la binafsi la maonesho, lakini halijatimiza lengo hilo kutokana na kutokuwa na fedha za kutosha.

Lakini, tatizo hilo haliwezi kukwamisha juhudi za Bw. Kuruma kutimiza ndoto yake, aliandaa vyumba viwili vya maonesho katika makazi yake: Nyumba ya Bw. Kuruma ina eneo la mita za mraba zipatazo 300, na theluthi mbili ya nyumba hiyo imejengwa kama ni vyumba vya maonesho. Kwenye milango ya vyumba hivyo, Bw. Kuruma amechora alama ya kuuliza yenye rangi kijani, na alama nyingine ya mshangao yenye rangi nyekundu. Hii itakuwa alama ya jumba lake la maonesho litakalojengwa siku za baadaye. Alisema, rangi ya kijani inamaanisha amani na nyekundu inamaanisha shari. Mzee huyo anaona kuwa, hii inaonesha historia ya Guinea, na historia ya Afrika.

Mwaka 2004, wakati Kituo cha Televisheni cha Beijing kilipokwenda Guinea kuandaa vipindi kuhusu "Njia ya Urafiki", na kujitahidi kupata habari kuhusu hayati waziri mkuu wa China Bw. Zhou Enlai alipotembelea Guinea katika miaka ya 60 ya karne ya 20, Bw. Kuruma alipata habari hiyo kwa wakati, na kwenda kwenye Ofisi husika kuwaelezea maofisa matarajio yake ya kukutana na kundi la waandishi wa habari wa kituo cha televisheni cha Beijing. Alisema yeye shahidi wa historia ya urafiki kati ya China na Guinea, anapenda kuwafungulia mlango wachina hao kwenye maonesho yake nyumbani kwake. Kama alivyotoa ahadi, kwenye makazi yake, ujumbe wa kituo cha televisheni cha Beijing ulipata fursa ya kuona picha na ripoti zinazomhusu Bw. Kuruma alizopiga mwanzoni mwa miaka ya 60 ya karne iliyopita, pia ujumbe huo ulitembelea vyumba vikubwa viwili vya maonesho vilivyoandaliwa Bw. Karuma kwa miaka mingi.

Bw. Kuruma ni mpiganaji mzee tangu miaka mingi iliyopita. Mwaka 1958, wakati Guinea ilipotangaza kupata uhuru, alikuwa akijiunga na jeshi nchini Ufaransa. Mwaka 1959, aliondoka kutoka Chuo Kikuu alikosoma nchini Ufaransa na kurejea nyumbani kwake, na kuanza kushughulikia mambo ya afya nchini Guinea. Alianzisha kituo cha kwanza cha watoto barani Afrika nchini Guinea, na kuwa ofisa wa Wizara ya afya ya Guinea. Kutokana na wadhifa huo, alianza kuwasiliana na China. Mwaka 1963, akiwa ofisa kijana akifuatana na ujumbe wa maofisa waandamizi wa serikali ya Guinea kutembea China, ambapo alikutana na viongozi wa wakati huo wa China marehemu Mao Zedong, Zhou Enlai na Deng Xiaoping. Mpaka sasa bado anakumbuka mambo halisi kuhusu viongozi hao wa China. Pia Bw. Kuruma alimwambia mwandishi wa habari kwa fahari kubwa: aliwahi kutembelea: mji wa Hangzhou, na miji mikubwa mitatu ya Beijing, Shanghai na Guangzhou. Baada ya safari hiyo, serikali za China na Guinea zilianza kufanya mawasiliano barabara.

Mwaka 1968, Beijing ilipeleka kundi la kwanza la madaktari nchini Guinea. Kundi hilo liliundwa na watu 50 na vikundi vidogo vitano, na kushughulikia kazi mbalimbali za tiba katika sehemu mbalimbali nchini Guinea. Juhudi zao zilianzisha daraja la urafiki kati ya Guinea na China moyoni mwa watu wa nchi hizo mbili.

Wakati kundi hilo lilipowasili nchini Guinea, Bw. Kuruma alikuwa ni mwendeshaji wa Tamasha la Hospitali ya Yastin la kulikaribisha kundi hilo. Bw. Kuruma aliwatambulisha wageni hao kwa wenyeji wa huko, kila mfanyakazi wa kundi la madaktari la China alipigiwa makofi kwa ukarimu, wakati alipomtambulisha mpishi wa kundi hilo, Bw. Kuruma alitangaza kwa vichekesho: "Huyo ni daktari wa madaktari wetu!" baada ya kusema hayo, makofi ya shangwe kubwa yalisikika na kuendelea kwa muda mrefu. Njia hiyo aliyoitumia iliigwa na watu na kuendelea mpaka sasa. Wapishi wa kundi la madaktarivileivile huwa wanaona fahari kubwa kwa kuhakikisha afya njema ya madaktari, na kufanya kazi kwa bidii zaidi.

Mpaka sasa, Beijing imepeleka vikundi 19 vya matibabu nchini Guinea. Hivi sasa madaktari 13 kutoka Hospitali ya Ji Shuitan ya Beijing inayojulikana kwa kutibu majeruhi wa mifupa, wanafanya kazi kwenye hospitali nchini humo. Bw. Kuruma anawakaribisha kwa moyo dhati madaktari hao wa China kutembelea vyumba vyake vya maonesho. Anaamini kithabiti kuwa, historia ya Guinea iliyoandikwa na mababu wa nchi hiyo itaongezwa mambo mapya na vijana wa karne mpya, na itatia nuru zaidi kwa dunia nzima.

Idhaa ya Kiswahili 2005-04-01