Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2005-04-01 20:30:38    
Ndege wa Vichakani

cri

Picha ndefu ya kuviringisha "NDEGE WA VICHAKANI" iliyochorwa kwenye karatasi ina urefu wa sentimita 34 na upana wa sentimita 1121.2. Katika picha ndefu za kuviringisha zilizochorwa mnamo Enzi ya Ming, ni nadra kwa picha ndefu kama hiyo kuonekana. Picha hiyo ni picha bora miongoni mwa picha za mchoraji Lin Liang zilizopokewa kizazi hadi kizazi.

Lin Liang alizaliwa Nanhai, mkoani Guangdong. Alikuwa mchoraji maarufu wa kwenye kasri ya ufalme na mchoraji mashuhuri wa maua na ndege wa kipindi cha kati cha Enzi ya Ming. Walakini kumbukumbu zinazohusu historia yake na uchoraji wake ni kidogo. Kuna utatanishi kuhusu mwaka wake wa kuzaliwa na wa kufa. Kuna wanaosema kuwa alizaliwa mwaka 1416 na alikufa mwaka 1480; na wengine wanasema kuwa aliishi katika kipindi cha kati ya mwaka 1436 na 1505. Mchoraji huyo alikuwa hodari wa kuchora tangu utotoni mwake. Katika sehemu alikozaliwa, mchoraji huyo alijulikana kwa uchoraji wake wa picha. Kutokana na historia yake ya uchoraji na picha zake zilizopokeza, hadi leo tunaweza kuona kuwa ustadi wake wa kuchora ulikuwa bora na imara. Kuna kazi zake nyingi ambazo zimekuwa zikipokewa kizazi baada ya kizazi mpaka hivi leo, miogoni mwake nyingi zaidi ni picha za maua na ndege zilizochorwa kwa rangi nyeusi ya maji. Alipenda kuchora vichaka, na kuchanganya ndege na mandhari ili kuonyesha kisanaa maumbile yaliyojaa uhai.

Picha ndefu ya NDEGE WA VICHAKANI inaonyesha aina kadhaa za ndege walioishi kwenye mlima na dimbwi la maji. Kuhusu ubunifu, mawazo ya kisanaa na ustadi wake wa kuchora, kama asingekuwa mchoraji hodari, asingethubutu kuchora picha ndefu namna hiyo. Picha hiyo ndefu ilichorwa kwa mfululizo kuanzia mwanzo mpaka mwisho, kama kwamba ilimalizwa kuchorwa kwa pumzi moja, kwa hivyo ni ngumu zaidi.

Kwenye mwanzo wa picha hiyo ndefu kuna shorewanda watatu wanaotaka kutua juu ya matawi ya kichaka. Maumbo yao yakiwa yanatofautiana, shorewanda hao wanapendeza sana. Nyuma yao wanaonekana mdiria wawili ndani ya kichaka cha matete, wakiwa wanawaangalia shorewanda hao. Baada ya sehemu hiyo unaonekana mti mmoja wenye majani madogo, na vitwitwi, virumbizi, kunguru na teleka. Wengine wanarukaruka na kulialia. Nusu nyingine ya kulia isiyoonekana pia ni dunia moja iliyojaa uhai. Katika vichaka na mianzi kuna ndege wengi. Wengine wanalia kwa kuinua midomo yao na wengine wako juu ya mianzi na vichaka, pia inaonekana misonobari yenye mashina makongwe na liana zinazoning'inia hewani. Mbele ya misonobari kuna mawe, michirizi na ndege wanaotafuta chakula majini; na mwishoni kwa mbali wanaonekana teleka wakija. Utungaji wa picha hii ni kamili na unawiana.

Lin Liang ni mwanzilishi wa picha za maua na ndege zilizochorwa huria kwa brashi, na rangi nyeusi ya maji; pia alikuwa mwakilishi maarufu wa picha za aina hiyo. Kuinua na kusukuma mbele kiwango cha picha za China zilizochorwa kwa rangi nyeusi ya maji.

Idhaa ya Kiswahili 2005-04-01