Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2005-04-04 15:50:53    
Kisiwa cha Gulangyu

cri

Kisiwa cha Gulangyu kiko sehemu ya kusini magharibi ya mji wa Xiamen mkoani Fujian, China. Eneo la kisiwa hiki si kubwa ambalo ni zaidi ya kilomita za mraba elfu 17, na wakazi wa kisiwa hiki ni chini ya elfu 20. Lakini kwenye kisiwa hiki kuna piano zaidi ya 500, yaani kwa wastani kila watu 40 wanamiliki piano moja, kiasi hiki kinaongoza nchini China hata ni nadra kuonekana katika dunia. Kila asubuhi au jioni, ukitembea kwenye kisiwa hicho, popote unapokwenda unaweza kusikia muziki uliopigwa kwa piano, ambapo milio ya mawimbi ya bahari na sauti ya muziki wa piano zinachanganyika na kuwa muziki murua wa koncheto. Hivyo kisiwa hicho kinasifiwa kuwa ni kisiwa cha piano. Mwongozaji wa utalii Dada Yang Yan alisema:

Kwa kawaida watalii wanafika kwenye kisiwa hiki wakati wa adhuhuri, ambapo wakazi wa kisiwa hiki wamekwenda kazini. Ni wakati wa asubuhi au jioni, wanapoweza kusikia muziki murua wa piano unaopigwa na familia moja moja na kusikika katika vichochoro mbalimbali kisiwani hapo.

Tokea katikati ya karne ya 19, wamisionari wa nchi za nje walipofika kwenye kisiwa hicho, walifanya shughuli za kidini mara kwa mara kwenye makanisa. Shughuli hizo zilikuwa ni pamoja na kipindi cha kuimba mashairi kwa kuambatana na muziki uliopigwa kwa piano, hata baadhi ya shule zilizoanzishwa na shirika la dini kwenye kisiwa hicho pia ziliweka somo la kuimba mashairi. Kutokana na hali hiyo, shughuli za kupiga piano na kuimba mashairi zikaenea kote kisiwani.

Kwenye kisiwa cha Gulangyu kuna familia nyingi ambazo watu wa kizazi baada kizazi wa familia hizo wanajua kupiga vizuri piano au vinanda vingine. Mwongozaji wa utalii Dada Yang Yan alisema, kila wikiendi au siku za sikukuu, watu wa familia hizo hukusanyika pamoja kufanya tamasha dogo la muziki la kifamilia:

Katika kisiwa hiki, watu wa familia nyingi wanapenda muziki kizazi baada ya kizazi, hivyo kila ifikapo usiku, baadhi ya watu wa familia hizo wanapiga volrin, wengine wanapiga piano kwa kuwafuatana, wengine wanaimba nyimbo, wakijiburudisha katika tamasha dogo la muziki la kifamilia.

Katika kisiwa cha Gulangyu, kuna Jumba la maonesho ya piano lililojengwa kwenye sehemu inayoegemea mlima. Jumba hilo ni jumba pekee linaloonesha piano za kale zaidi ya 70 zilizotengenezwa na Uingereza, Ufaransa, Ujerumani, Marekani, Austria na Australia, baadhi yao hata hazionekani tena katika sehemu nyingine duniani.

Zaidi ya hayo, jumba hilo pia limehifadhi piano nyingi zenye thamani, kama vile piano ya pembe ya ndovu iliyotengenezwa huko Berlin, Ujerumani katikati ya karne ya 19, pia yenye pembe 4 ambayo ni kubwa kabisa duniani, na piano nyingine zenye thamani kubwa. Watalii wanaotembea jumba hilo huvutiwa sana na utamaduni wa piano unaooneshwa huko. Mtalii Wei Yuyu alimwambia mwandishi wa habari akisema:

Mimi najifunza muziki, hivyo piano inaweza kugusa hisia zangu maalum. Nimepata ujuzi mwingi pia naona nimejiburusha katika jumba hilo la maonesho ya piano.

Karibuni kwenye kisiwa cha piano mjisikie mvuto wake.

Idhaa ya kiswahili 2005-04-04