Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2005-04-06 14:47:56    
Kompyuta yenye mifumo miwili kwa ajili ya watoto na watu wazima

cri

Hivi sasa, kompyuta imekuwa mahitaji ya watu katika kazi, elimu na maisha. Ingwa kuna aina mbalimbali za kompyuta zinazouzwa sokoni, lakini kulikuwa hakuna kompyuta inayoweza kutimiza mahitaji ya watu waizma na ya watoto. Siku chache zilizopita, China imetatua suala hilo kwa kuwa na kompyuta yenye mifumo miwili, mmoja kwa ajili ya watu wazima na mwingine kwa watoto.

    Kompyuta na tovuti zimerahisisha maisha yetu, lakini pia zimeleta masuala mengi ya kijamii, kama vile tovuti zinazohusu matumizi ya kimabavu na ngono zinawaelekeza watoto kwa makosa. Aidha, hivi sasa watoto wengi wana tabia ya kucheza michezo ya kompyuta na kuwasiliana na wengine kwenye tovuti, hali ambayo inawabidi baadhi ya wazazi kuwasimamia watoto wao kila wakati wanapotumia kompyuta ili wasije wakaathiriwa na vitu vibaya kwenye tovuti. Ingawa wazazi hao wanajitahidi, lakini hiyo sio njia nzuri.

    Mtoto wa Bw. Zhang wa Beijing anasoma katika shule ya msingi, Bw. Zhang ana wasiwasi kuhusu suala hilo, akisema:

    "Kwa kweli siwezi kumzuia mtoto wangu asiwasiliane na wageni kwenye tovuti. Ninachoweza kufanya ni kumwambia mara kwa mara tu asifanye hivyo. Kwenye tovuti kuna habari za aina mbalimbali, nina wasiwasi kuwa mtoto wangu ataathiriwa na habari mbaya, na hivi sasa kuna ripoti nyingi kuhusu hatari ya kukutana na marafiki wapya wa kwenye Internet, ambazo zimeongeza wasiwasi wangu."

    Wazazi wanatumai kuwa kompyuta haitakuwa midoli inayopoteza wakati wa watoto, bali kitakuwa ni kifaa cha kujifunzia, kinachoweza kuwasaidia watoto katika masomo yao. Bibi Li, ana mtoto mmoja wa kiume mwenye umri wa miaka 14, anaona kuwa ni afadhali kompyuta yangu nyumbani itakuwa mwalimu binafsi baada ya masomo, akisema:

    "Hivi sasa, mimi na mume wangu tumebanwa na shughuli nyingi, hivyo hatuna nafasi za kumhimiza mtoto wetu ashiriki kwenye madarasa ya uchoraji, Kiingereza na hisabati kama wazazi wengine wanavyofanya, hivyo tunatumai kuwa kompyuta inaweza kufanya kazi kama mwalimu binafsi."

    Kadiri kompyuta yenye mifumo miwili kwa ajili ya watu wazima na watoto inavyotengenezwa nchini China, ndivyo masuala hayo yanayowasumbua wazazi yanavyozidi kutuliwa. Kompyuta za aina hiyo zilizotengenezwa na kampuni maarufu ya kompyuta ya China Group of Fangzheng na kampuni ya Intel, hasa ni kwa ajili ya watoto wenye umri kati ya miaka mitatu na miaka 16, na wazazi wanaweza kuchuja habari kwa njia rahisi bila kuzima kompyuta.

    Mkurugenzi wa sekta ya biashara ya rejareja ya kampuni ya Fangzheng Bi. Wujun alimwambia mwandishi wetu wa habari, akisema:  

    "Kompyuta kwa ajili ya watoto inapaswa kutilia mkazo katika elimu na burudani. Tulipotengeneza aina hiyo mpya ya kompyuta tulitilia maanani juu ya namna ya kuwaelekeza watoto kwa usahihi katika elimu na burudani."

    Kwa kupitia swichi moja mfumo wa kompyuta hiyo unaweza kubadilishwa, njia ambayo ni rahisi sana kama kubadilisha vituo vya televisheni. Ukitoa kifunguo, mfumo wa kompyuta haubadiliki, hivyo watoto wanaweza kutumia kompyuta za aina hiyo chini ya udhibiti wa wazazi wao.

    Imefahamika kuwa kompyuta hiyo ina software zinazoweza kuchuja habari ili watoto wasije wakasoma habari mbaya kama vile nguvu za kimabavu na ngono.

    "Software" na "hardware" za kompyuta za aina hiyo zote zinatimiza vizuri mahitaji ya watoto.

    Ili kutimiza mahitaji ya watoto, kompyuta hiyo ina kioo kinachoweza inayoweza kuandikwa maneno moja kwa moja, ambayo inafanya kazi kama "keyboard" na "mouse", hivyo watoto wanaweza kuchagua kwa kidole taarifa mbalimbali. Pia kompyuta ya aina hiyo ina meza moja inayoweza kubadilishwa kutokana na urefu wa watoto, ili wasome na kuandika vizuri.

    Aidha, kompyuta ya aina hiyo isiyo na nyaya nyingi za umeme, ni salama kwa watoto.

    Mbali na hayo, kompyuta ya aina hiyo ina software nyingi za elimu na burudani zinazowafaa watoto wenye umri mbalimbali, na software hizo zitawavutia watoto kwa katuni nyingi. Sio kama tu watoto wanaweza kujifunza fasihi, hisabati na Kiingereza na masomo mengine mengi kwa kutumia kompyuta hiyo, bali pia wanaweza kucheza michezo ya kopyuta inayowafaa na kuwavutia.

    Habari zinasema kuwa kompyuta za aina hiyo zimesifiwa katika maonesho ya kompyuta yaliyofanyika katika nchi za nje, na zitauzwa nchini Marekani na katika nchi za Ulaya.

    Naibu meneja wa sekta ya uzalishaji ya kampuni ya Fangzheng Bi. Bai Xiangchun alisema kuwa kampuni hiyo itajitahidi kuboresha teknolojia na kutengeneza kompyuta za aina mpya inayowafaa zaidi watoto, akisema:

    "Tutarahisisha zaidi matumizi ya kompyuta za aina hiyo, pia tutashirikiana na makampuni mengine ya software na Internet kwa watoto, ili kuwaletea watoto taarifa mbalimbali nzuri kwa kupitia kompyuta za aina hiyo."

Idhaa ya Kiswahili 2005-04-06