Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2005-04-06 16:27:58    
Mtindo wa maisha ya Pudong Shanghai-Ufanisi, mtundo na namna ya kimataifa

cri

Mchana, wafanyabiashara wanafanya kazi kwenye kampuni au kufanya mikutano kwenye hoteli za nyota tano; usiku wanakutana na marafiki kwenye baa au kwenda kwenye bustani zilizo kando ya mto kunywa chai na kahawa, ambapo wanajiburudika katika madhari nzuri ya usiku; katika wikendi wanasikiliza muziki kwenye kituo cha sanaa cha Dongfang au kwenda kucheza Golf wakifanya mazoezi ya kujenga mwili chini ya mwangaza wa jua, aidha wanafanya mazungumzo kuhusu ushirikiano wa biashara na wafanyabiashara wengine?hivi sasa, huko Pudong, Shanghai mji mkubwa ulioko mashariki ya China, wafanyabiashara wa China na nchi za nje wanafanya kazi na kuishi maisha kwa mtindo huo.

Miaka 10 iliyopita, ikiwa wilaya moja ya mji wa Shanghai, Pudong ilikuwa imeendelea kwa haraka, hivi sasa Pudong ni sehemu muhimu ya uchumi nchini China na hata duniani.

Mtaalamu wa Japan alisema kuwa, katika miji mingi mikubwa duniani, watu wana mitindo mbalimbali ya maisha. Kwa mfano, New York ina mtindo wa maisha ya New York, Tokyo ina mtindo wa maisha ya Tokyo. Hivi sasa mtindo wa maisha ya Pudong ambao unaonesha ufanisi, mtindo na namna ya kimataifa unakaribishwa na kufuatwa na wafanyabiashara wengi wa China na nchi za nje.

Zamani watu wa Shanghai walisema kuwa, " Bora tupate kitanda kimoja tu huko Puxi kuliko kupata nyumba katika Pudong." (" Puxi" ni sehemu ya magharibi ya Mto Huangpu wa Shanghai ambayo uchumi wake uliendelea haraka zamani; " Pudong" ni sehemu ya Mashariki ya Mto Huangpu wa Shanghai, ambayo ilikuwa nyuma kuliko Puxi, katika miaka ya hivi karibuni maendeleo ya uchumi wa eneo hilo yamevuta watu duniani. Hivi sasa hali imebadilika sana, nyumba za Pudong zinauzwa kwa bei ya juu sana. Kutokana na mazingira mazuri ya kuishi na kufanya kazi huko Pudong, wafanyabiashara laki moja wakiwemo wageni elfu 30 wameanzisha shughuli zao huko Pudong na kuishi huko.

Mfanyabiashara mmoja aliyetoka Marekani alisema kuwa, sehemu ya Pudong ina mandhari nzuri, utulivu na usalama, hasa ni nzuri zaidi kuliko hata baadhi ya sehemu za nchi za magharibi.

Msaidizi wa Meneja mkuu wa Kampuni ya Zhongxin ya kimataifa Bw. Yuning alisema kuwa, mazingira ya uwekezaji vitega uchumi na maisha ya Pudong ni mazuri ya kiwango cha juu duniani, ambapo hali yake kisasa na utamaduni wake una mvuto mkubwa. Kufanya kazi na kuishi Pudong si kama tu kunaonesha mafanikio makubwa yaliyopatikana katika kazi, bali pia ni kuchagua mtindo mpya wa maisha. Pudong inawawezesha watu wajisikia uhuru, uchangamfu na uerevu.

Idhaa ya kiswahili 2005-04-06