Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2005-04-06 16:35:00    
Raia wa Sudan waandamana kulaani azimio la Umoja wa Mataifa

cri

Maelfu kumi kadhaa ya raia wa Sudan tarehe 5 waliandamana katika mji mkuu Khartoum, wakilaani Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa kupitisha azimio nambari 1593 mwishoni mwa mwezi uliopita na kuunga mkono serikali ya Sudan kutangaza kupinga azimio hilo.

Waandamanaji walishutumu azimio hilo kutoheshimu mamlaka ya Sudan na kuona kuwa mashirika kadhaa ya Umoja wa Mataifa kwa kusimamiwa na nchi fulani za magharibi yalijaribu kuzusha machafuko na kulifanya suala la Darfur liwe la utatanishi zaidi na kuiweka Sudan vikwazo katika mchakato wa amani ya maendeleo nchini Sudan.

Tarehe 31 mwezi Machi, Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa lilipitisha azimio nambari 1593 na kuwafikisha maofisa wa jeshi na serikali ya Sudan, wanamgambo wanaopendelea serikali na askari wa makundi ya upinzani kwenye mahakama ya kimataifa ya The Hague kwa hatia za vita na uhalifu dhidi ya ubinadamu. Serikali ya Sudan tarehe 3 ilitangaza kupinga azimio hilo na kuamua kuunda tume kuu ya kutatua mgogoro ili kuondoa kwa dharura athari zilizosababishwa na azimio hilo kwa Sudan.

Mwezi Februari, tume ya uchunguzi ya kimataifa iliyoteuliwa na katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa Bw. Kofi Annan ilitoa ripoti kwa Baraza la Usalama, likiwashitaki Wasudan 51 wakiwemo polisi na wanamgambo wanaopendelea serikali na askari wa makundi ya upinzani kuwa na hatia za vita na uhalifu dhidi ya ubinadamu. Mwanzoni mwa Machi, Ufaransa iliwasilisha muswada wa azimio kwa Baraza la Usalama kuitaka mahakama ya kimataifa kuwahukumu watu hao. Hatimaye, pendekezo hilo lilipitishwa kwa kutopigiwa kura na Marekani, China, Brazil na Algeria na limekuwa azimio nambari 1593.

Serikali ya Sudan imepinga azimio hilo kutokana na azimio hilo kuathiri maslahi ya taifa ya Sudan na hukumu ya mahakama ya kimataifa itawezekana kuchochea nguvu za mfarakano. Serikali ya Sudan pia ilisisitiza kuwa serikali hiyo ina uwezo wa kuwahukumu watuhumiwa hao. Mwishoni mwa mwezi uliopita, idara ya sheria ya Sudan iliwatia nguvuni polisi 15 waliotuhumiwa kuwaua watu katika sehemu ya Darfur bila hatia yoyote.

Wachambuzi wanaona kuwa azimio nambari 1593 haliwezi kukwama serikali ya Sudan. Kwanza Sudan sio nchi iliyosaini mkataba wa kimataifa kuhusu kuunda mahakama ya kimataifa, kwa hiyo haina wajibu wa kutekeleza mkataba huo. Pili, nchi kadhaa ikiwemo Marekani hazikupiga kura kwa azimio hilo, jambo hilo linaonesha kuwa jumuiya ya kimataifa ina maoni tofauti. Tatu, Umoja wa Mataifa haukutunga hatua zinazoambatana na azimio hilo. Ingawa Baraza la Usalama limeamua kuweka jeshi la kulinda amani katika sehemu ya kusini mwa Sudan, lakini mjumbe maalum wa Umoja wa Mataifa kuhusu suala la Sudan Bw. Jan Pronk alieleza kuwa sasa jeshi hilo halitatekeleza jukumu la kuwatia nguvuni watuhumiwa hao. Kwa hiyo, ni vigumu kukadiria matokeo kuhusu serikali ya Sudan kupinga azimio nambari 1593.

Idhaa ya kiswahili 2005-04-06