Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2005-04-06 18:36:45    
Ukaguzi wa mara nne kuhusu vitabu vya kiada vya historia

cri

Serikali ya Japan kila baada ya miaka minne inakagua vitabu vya kiada vya historia vinavyotungwa na mashirika ya uchapishaji yasiyo ya kiserikali. Tokea miaka ya 80 ya karne iliyopita hadi hivi sasa vitabu hivyo vilivyokaguliwa mara nne na serikali ya Japan vyote vilibadilisha historia na kuboresha vita vya kishambulizi, ambavyo vimesababisha hamaki na malalamiko ya nchi za Asia na jumuiya ya kimataifa.

Vitabu vya kiada vya historia vilivyokaguliwa na wizara ya utamaduni na sayansi mwezi Juni mwaka 1982, vilibadilisha maneno yaliyosema kuwa mwaka 1894 jeshi la baharini la Japan lilivamia jeshi la baharini la China na kuanzisha vita na China kuwa "Manowari za nchi mbili za Japan na za enzi ya Qing zilipigana vita"; kubadilisha tukio la tarehe 19 Septemba, ambalo jeshi la Japan lilikalia sehemu ya kaskazini mashariki ya China kuwa "jeshi la Japan lilibomoa reli ya sehemu ya kusini ya Manchuria"; kubadilisha "kushambulia sehemu ya kaskazini ya china" kuwa "kuingia na kutoka sehemu ya kaskazini ya China"; kubadilisha mauaji makubwa ya Nanjing yaliyofanywa na jeshi la Japan kuwa "tukio lililosababishwa na upinzani mkali wa jeshi la China".

Vitendo vya kubadilisha historia vya wizara ya utamaduni na sayansi ya Japan kwa njia ya kubadilisha meneno yaliyomo ndani ya vitabu vya kiada vimeshutumiwa vikali na watu wa sekta mbalimbali za Japan pamoja na jumuiya ya kimataifa. Chini ya shinikizo kubwa ya vyombo vya habari, waziri kiongozi wa Japan tarehe 26 Agosti katika mwaka ule alitoa "maelezo ya serikali" kuhusu suala la vitabu vya kiada yakisema kuwa Japan inakubali ukosoaji wa nchi jirani, na kuwa "serikali itawajibika kufanya marekebisho" kuhusu makosa yaliyotokea katika vitabu vya kiada. Alisema kuwa serikali ya Japan na wananchi wake wametambua kabisa kuwa vitendo ilivyotenda Japan siku za nyuma vilileta taabu na hasara kubwa na watu wa nchi mbalimbali za Asia, Japan inajikosoa na kuhakikisha kuwa vitendo hivyo kavitarudiwa tena. Waziri mkuu wa Japan wa kipindi kile alipotoa hotuba tarehe 9 mwezi Septemba mwaka ule alisema kuwa Japan itapokea kabisa ukosoaji wa nchi husika na kutatua suala la vitabu vya kiada kwa moyo wa dhati. Waziri wa utamaduni na sayansi wa Japan tarehe 26 Novemba mwaka ule alisema, "wakati wa kushughulikia matukio kati yake na nchi jirani za Asia kuhusu historia ya miaka ya karibuni, Japan inatakiwa kuyazingatia na kuyatatua kwa maelewano na usuluhishi wa kimataifa", ambazo zilikuwa "kanuni kuhusu nchi jirani" zilizowekwa na wizara ya utamaduni na sayansi ya Japan katika kukagua vitabu vya kiada.

Mwezi Mei mwaka 1986, vitabu vya kiada vya historia vijulikanavyo kama "Vitabu vipya ya historia ya Japan", ambavyo vilitungwa na bunge la kulinda wananchi wa Japan, havikutaja kwamba Japan iliwahi kushambulia nchi nyingine, katika sehemu nyingi vilipotosha historia na kujaribu kukanusha lawama kuhusu vita vya kishambulizi vilivyoanzishwa na Japan.

Mwezi Aprili mwaka 2001wizara ya utamaduni na sayansi ya Japan ilipitisha vitabu vya kiada vya historia vilivyotungwa na kundi la watu wa mrengo wa kulia, ambavyo vilisema vita vya bahari ya Pasifiki ni kwa ajili ya "kujilinda", "kukomboa Asia" na ni "vita vya haki".

Tarehe 5 mwezi Aprili mwaka 2005 wizara ya utamaduni ya sayansi ya Japan ilikubali kabisa kundi hilo la mrengo wa kulia kutunga "vitabu vipya vya kiada vya historia" na kuvipitisha. Ingawa vilifanyiwa marekebisho 124, lakini bado kuna makosa mengi muhimu ya kupotosha historia.

Watu wameona kuwa ukaguzi wa mara mbili baada ya kuingia karne mpya, serikali ya Japan haijali kabisa "kanuni kuhusu nchi jirani" zinazoendana na maelewano na usuluhishi wa kimataifa. Mwelekeo huo umeonesha mabadiliko ya mkakati wa kidiplomasia wa Japan.

Idhaa ya Kiswahili 2005-04-06