Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2005-04-06 20:49:49    
Vipapatio vya kuku vilivyopikwa na kokakola

cri

Mahitaji

Vipapatio vya kuku gramu 500, kiasi kidogo cha vipande vya vitunguu maji, tangawizi na vitunguu saumu, chumvi, mchuzi, mvinyo wa kupikia, sukari, kokakola na mafuta

Njia

1. Osha vipapatio vya kuku, na vipasue kwa kisu. Vipakue ndani ya bakuli na tia chumvi, mchuzi, mvinyo wa kupikia, sukari, koroga na uviloweshe kwa dakika 40 hivi.

2. Tia mafuta ndani ya sufuria pasha moto mpaka yawe na joto la nyuzi 60 hivi, na tia vipapatio na uvikaange mpaka viwe na rangi ya dhahabu, vipakue.

3. vipashe moto tena, na tia vipande vya vitunguu maji, tangawizi na vitunguu saumu, koroga halafu tia vipapatio, chumvi, mchuzi, mvinyo wa kupikia, sukari, kokakola baada ya kuchemka pungua moto kidogo na endelea kuchemsha kwa nusu saa. Mpaka hapo kitoweo hiki kitakuwa tayari.