Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2005-04-07 20:02:28    
Mto Zhujiang

cri

Mto Zhujiang ulioko kusini mwa China ni mmoja kati ya mito saba mikubwa nchini China.

Maliasili ya maji katika mto huo ni nyingi ambayo ni ya pili baada ya Mto Changjiang nchini China na ni mara 6 kuliko maliasili ya maji katika Mto Manjano.

Katika bonde la Mto Zhujiang kuna eneo kubwa lenye milima midogo midogo, ambalo linachukua asilimia 94.5 ya eneo lote, eneo la tambarare ni dogo ambalo linachukua asilimia 5.5. Urefu kutoka usawa wa bahari wa sehemu ya kaskazini magharibi ni mkubwa kuliko sehemu ya mashariki kusini. Katika sehemu ya kaskazini magharibi kuna uwanda wa juu wa Yunnan na Guizhou ambao urefu wa wastani wa mita 1000 hadi 2000 kutoka usawa wa bahari. Mashariki ya uwanda huo kuna sehemu yenye milima midogo midogo yenye urefu wa wastani wa mita 500 kutoka usawa bahari.

Bonde la Mto Zhujiang liko kwenye ukanda wa nusu-tropiki. Mstari wa Tropiki ya Kansa unapitia katikati ya sehemu hiyo. Hali ya hewa ya huko ni ya ukanda wa tropiki na ya ukanda wa nusu-tropiki yenye mvua nyingi. Katika majira ya Spring, mvua hunyesha kwa siku nyingi; katika majira ya joto, hali ya hewa ni joto sana na mvua mkubwa hunyesha; katika majira ya Autumn tufani zinatokea mara kwa mara; na katika majira ya baridi hali ya hewa si baridi sana na mvua ni ndogo. Katika sehemu nyingi joto la wastani kwa mwaka ni nyuzi 14 hadi nyuzi 22 sentigredi, na kiasi cha mvua kwa mwaka ni milimita 1200 hadi 2200.

Bonde la Mto Zhujiang linaundwa na mifumo minne ya mito ikiwemo Mto Xijiang, Mto Beijiang, Mto Dongjiang na mito kadhaa kwenye Delta ya Mto Zhujiang.

 Maliasili ya ardhi katika bonde la Mto Zhujiang ni hekta milioni 44.2, hekta milioni 4.8 kati ya hizo ni mashamba, na hekta milioni 12.6 ni misitu. Nafaka muhimu katika sehemu hiyo ni mpunga, mahindi, ngano na viazi. Mazao ya kiuchumi ni pamoja na miwa, tumbaku, mkonge na miti ya forosadi. Upandaji wa miwa unapata maendeleo ya haraka, na uzalishaji wa sukari huko unachukua nusu ya uzalishaji nchini China. Mazao ya kiuchumi ya ukanda wa tropiki ni pamoja na miti ya mpira, michikichi, kahawa, kakao, mkonge na Cymbopogon.

Madini muhimu katika sehemu hiyo ni pamoja na madini ya manganizi, chuma, tungsten, alumini, bati na salfa.

Miji ya Guangzhou, Zhanjiang na Beihai ni bandari muhimu katika sehemu hiyo, na miji ya Shenzhen, Zhuhai, Shantou na mkoa wa Hainan ni sehemu maalum za kiuchumi. Delta ya Mto Zhujiang ni sehemu ya maendeleo ya kiuchumi iliyoko katika pwani nchini China.

Idadi ya watu wa sehemu hiyo ni milioni 89.9, na idadi ya watu wa makabila madogo madogo waishio huko ni kubwa zaidi nchini China. Makabila muhimu katika sehemu hiyo ni makabila ya Wahan, Wazhuang, Wamiao, Wabuyi na Wamaonan.

  

Idhaa ya Kiswahili 2005-04-07