Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2005-04-07 21:25:29    
Mchakato wa amani ya Cote D'Ivoire warejea kuwa na hali nzuri tena

cri

    Viongozi wa pande mbalimbali zilizopambana za Cote D'Ivoire tarehe 6 huko Pretoria, nchini Afrika ya Kusini walisaini Makubaliano ya Pretoria, wakikubali kusimamisha kwa pande zote vita vya wenyewe kwa wenyewe sasa hivi. Maoni ya raia yamesema, kusainiwa kwa makubaliano hayo kunamaanisha kuwa mchakato wa amani ya Cote D'Ivoire umetokewa hali nzuri tena, lakini bado haijajulikana kama makubaliano hayo yatatekelezwa kwa makini au la.

    Chini ya uendeshaji wa rais Thabo Mbeki wa Afrika ya Kusini, ambaye pia ni mpatanishi aliyeteuliwa na Umoja wa Afrika kushughulikia suala la Cote D'Ivoire, viongozi wa pande mbalimbali zilizopambana za Cote D'Ivoire walikuwa na mazungumzo, ambapo rais Laurent Gbagbo wa Cote D'Ivoire, rais wa zamani Bw. Henri Konan Bedie, viongozi wa makundi ya upinzani, waziri mkuu wa zamani Bw. Alassane Ouattara na kiongozi wa kundi la "the New Forces" Bw. Guillaume Soro walihudhuria mazungumzo hayo. Hayo ni mazungumzo ya ngazi ya juu kabisa tangu mazungumzo yaliyofanyika mwaka jana ya makundi mbalimbali.

    Kwenye mkataba huo pande mbalimbali zimetangaza kusimamisha vita na vitendo vyote dhidi ya pande nyingine na kuwanyang'anya silaha wanamgambo wote wanaopambana. Pia pande mbalimbali zimekubali kufanya uchaguzi mkuu na kutatua suala la sifa ya wagombea wa urais ndani ya wakati fulani; kundi la "the New Forces" na makundi mengine ya upinzani yamekubali kushiriki tena kwenye serikali ya maafikiano ya makabila. Aidha, pande zote zimekubali kupokea wanamgambo zaidi ya 600 wa upinzani wa zamani kujiunga na kikosi cha polisi.

    Jaribio la kupindua serikali lilitokea Mwezi Septemba mwaka 2002 nchini Cote D'Ivoire, na kuzusha vita vya wenyewe kwa wenyewe. Ingawa pande mbalimbali zilizopambana zilisaini Mkataba wa Marcoussis na Mkataba wa Accra mwaka 2003 na mwaka 2004, lakini wakati mikataba hiyo miwili ilipotekelezwa, kutokana na pande mbalimbali kuzidi kupambana ili kujipatia udhibiti, mchakato wa amani ya Cote D'Ivoire ulikwama mara kwa mara. Tangu Mwezi Novemba mwaka 2004, hali ya Cote D'Ivoire imekuwa mbaya zaidi. Kutokana na hali hiyo, Umoja wa Afrika ulimteua wa rais Thabo Mbeki wa Afrika ya Kusini kuwa mpatanishi wa kushughulikia suala hilo ili kuanzisha tena mchakato wa amani ya Cote D'Ivoire.

    Wachambuzi wanaona kuwa ingawa kusainiwa kwa makubaliano ya Pretoria kutasaidia kupunguza hali ya wasiwasi nchini Cote D'Ivoire, lakini utekelezaji wake utakabiliwa na shida nyingi.

    Kwanza, mkataba huo kwa ujumla ni sawa na mikataba miwili ya zamani, ambayo imezitaka pande mbalimbali zitekeleze kwa makini unyang'anyaji wa silaha na kutatua suala la sifa ya wagombea wa urais.

    Pili, makubaliano hayo hayajaweka ratiba wazi ya kutekeleza vifungu mbalimbali. Kabla ya hapo, kundi la "the New Forces" liliwahi kukataa kutekeleza vifungu husika hata kulikuwa na ratiba wazi kwenye mikataba miwili ya zamani.

    Tatu, wataalam wamesema kuwa uchaguzi mkuu wa Cote D'Ivoire utahitaji maandalizi ya miezi isiyopungua 18. Kwa mujibu wa mpango, uchguzi huo utafanyika baada ya miezi sita, yaani mwezi Oktoba mwaka huu, lakini mpaka hivi sasa kazi ya maandalizi haijaanza. Hivyo haijulikani kama uchaguzi huo utafanyika kwa wakati au la na kuwa kama utafanyika kwa wakati uliowekwa, utasaidia kuanzisha tena kwa mchakato wa amani au la.

    Maoni ya raia yamesema kuwa, ni hadi pande mbalimbali zitakapoamiana, kuelewana na kutekeleza mikataba ya amani tu, ndipo mchakato wa amani ya Cote D'Ivoire utaanzishwa tena.

Idhaa ya Kiswahili 2005-04-07