Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2005-04-07 20:56:26    
Kazi ya kuwapangia maisha wahamiaji ziendelee kwa juhudi

cri

 Mkutano wa kujumulisha uzoefu na kusifu watu na idara zinazopigiwa mfano katika kazi ya kuwapangia maisha wahamiaji wa sehemu ya hodhi la maji kwenye Magenge Matatu ya Mto Changjiang ulifanyika tarehe 5 katika mji wa Chongqing. Naibu waziri mkuu Zeng Peiyuan alihutubia mkutano huo, alisema kuwa kazi ya kuwapatia makazi mapya wahamiaji wanaohamishwa kutoka sehemu ya hodhi la maji kwenye Magenge Matatu ya Mto Changjiang imemalizika kwa mafanikio, lakini kazi ya kuwasaidia wahamiaji hayo katika uchumi na kuwapatia ajira ili wasiwe na wasiwasi wa maisha katika sehemu walipohamia lazima iendelee kwa juhudi.

Kuanzia mwaka 2000 wakazi walioishi katika sehemu ya hodhi la maji kwenye Magenge Matatu ya Mto Changjiang walianza kuhamishwa kwenye miji na mikoa 11 nchini China. Katika muda wa miaka mitano iliyopita jumla ya wakazi laki 1.66 wamehamishwa, kazi ya kuwapapatia makazi mapya imefanikiwa na hakuna wanaorudia tena. Kwenye mkutano Bw. Zeng Peiyuan alisifu watu na idara zilizopigiwa mfano katika kazi hiyo.

Bw. Zeng alisema wakulima waliohamishwa ni wengi, kazi ni ngumu, lakini kutokana na juhudi kubwa zilizofanywa na watu na idara mbalimbali na ofisi ya baraza la serikali wahamiaji walio wengi waliweza kutanguliza mbele maslahi ya taifa na kuacha maslahi binafsi, wote wamehamia katika muda mfupi kwa hiari na kwa usalama. Hivi sasa katika sehemu walikohamishia miundombinu ya umeme, maji, barabara na mawasiliano ya habari imekamilika, wengi wao wamezoea mazingira mapya wanakoishi na wameanza shughuli za uchumi, wamekuwa wakitoa mchango kwa ajili ya uchumi wa taifa.

Bw. Zeng alisema, kutokana na ujenzi wa kisasa nchini China, miradi mingi mikubwa mikubwa itajengwa, hivyo hakuna budi kuwahamisha wenyeji kutoka mahali penye miradi. Uzoefu wa kuhamisha wenyeji katika sehemu ya hodhi la maji ya Magenge Matatu ya Mcho Changjiang ni mfano wa kuigwa kwa sehemu nyingine zinazofanyiwa miradi. Alisema, kazi za uhamishaji zinahitaji viongozi watilie maanani, na wawasaidie wahamiaji kwa muda mrefu.

Bw. Zeng alisisitiza kuwa idara zote huzika lazima zitambue umuhimu wa kazi za uhamishaji ambazo ni kazi za muda mrefu na za utatanishi, zishikilie kutanguliza mbele maslahi ya umma, na kuwapangia maisha kwa makini na kutekeleza sera na hatua husika ili kuhakikisha mradi wa Magenge Matatu ya Mto Cjhangjiang inaendelea bila matatizo.

Bw. Zeng alizitaka idara zote hisika na serikali za mitaa ziimarishe kazi ya kifikra kwa kina, ziwafahamishe wahamiaji hali ya mikoa, wilaya, vijiji na kutatua tatizo la kutopatana na majirani, na kuwasaidia kwa shughuli za kiuchumi, ziimarishe mafunzo ya kiufundi ili wapate ajira. Fedha kwa ajili ya uhamishaji lazima zitumike bila ubadhirifu.

Bw. Zeng alipokuwa katika mji wa Chongqing alifanya uchunguzi kwa kutembelea familia za wahamiaji, mashirika na viwanda.

Idhaa ya kiswahili 2005-04-07