Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2005-04-07 21:02:41    
Matatizo katika kazi za afya ya wanawake na watoto yako vijijini na mkazo wake uko katika sehemu za katikati na magharibi za China

cri

Mkuu wa idara ya huduma za wanawake na watoto na afya mitaani Bw. Yang Qing hivi karibuni alisema kuwa ingawa kiasi cha vifo vya wanawake wajawazito na watoto wachanga kimepungua siku zote, lakini bado kuna matatizo kadhaa katika kazi za afya za wanawake na watoto. Aliainisha kuwa shida za kazi za afya za wanawake na watoto ziko vijijini na mkazo wake uko katika sehemu za katikati na magharibi za China.

Bw. Yang Qing alisema kuwa kuna tofauti kubwa kati ya miji na vijiji na kati ya sehemu za mashariki na magharibi katika kazi hizo. Kutokana na matokeo mapya ya upimaji wa afya, kiasi cha vifo vya wanawake wajawazito vijijini kilikuwa asilimia 0.0654 mwaka 2003, ambayo ni mara 2.4 kuliko ile ya asilimia 0.0276 mijini na kiasi cha vifo vya watoto wachanga vijijini kilikuwa asilimia 2.87 ambayo ni mara 2.5 kuliko ile ya asilimia 1.13 mijini. Kiasi cha wanawake wajawazito na watoto wachanga katika sehemu ya magharibi pia kilikuwa zaidi ya mara 2 kuliko kile cha sehemu ya mashariki.

Bw Yang Qing alisema kuwa vyanzo muhimu vya kusababisha kiasi kikubwa cha vifo vya wanawake wajawazito na watoto wachanga vijijini ni kama vifuatavyo. Kwanza, wakulima wanakosa huduma za msingi za afya na gharama za hospitali kwa wanawake hao vijijini zinalipwa na wanawake hao wenyewe. Gharama hizo ni malipo makubwa kwa familia za wakulima zenye mapato madogo, jambo ambalo linasababisha wanawake wajawazito vijijini wajifungue nyumbani ili kupunguza malipo. Mazingira hafifu na utalaam duni wa matibabu unatishia usalama wa afya za wanawake hao na watoto wao. Pili, uwezo wa idara za huduma za afya za ngazi tatu za wilaya, tarafa na vijiji ni mdogo, hasa ngazi mbili za tarafa na vijiji. Viwango vya elimu za madaktari wanaoshughulikia afya za wanawake na watoto ni cha chini zaidi. Kwa hiyo matatizo kuhusu afya za wanawake na watoto ni makubwa zaidi katika sehemu za katikati na magharibi zilizo maskini kiasi.

Zaidi ya hayo, wakazi maskini mijini na wakulima wanaokwenda mijini kutafuta ajira pia ni tatizo linalopaswa kufuatiliwa katika kazi za afya za wanawake na watoto wanaokosa huduma za tiba. Bw. Yang Qing alisema kuwa aina za huduma za tiba za China ni chache ambazo haziwezi kutosheleza mahitaji ya afya ya wanawake na watoto wenye hali tofauti. Hospitali kubwa za mijini hazina huduma za ngazi ya chini na hospitali za mashina zinashindwa kutoa huduma zenye kiwango cha juu. Kwa hiyo hali hiyo imesababisha wakazi maskini wa mijini na wakulima waliokwenda mijini kutafuta ajira wawe na matatizo ya kwenda hospitali kutokana na mapato kidogo, hali hiyo pia inaathiri kazi ya afya za wanawake na watoto.

Tarehe 7 mwezi Aprili ni "siku ya afya duniani". Kauli mbiu ya mwaka huu ya siku hiyo ni "kumthamini kila mama na mtoto". Bw. Yang Qing alisema: "Ni matumaini yangu kuwa sera ya kina mama kujifungua hospitalini bila malipo itatekelezwa katika vijiji mapema iwezekanavyo".

Idhaa ya kiswahili 2005-04-07