Hivi karibuni Zimbabwe ilifanya uchaguzi wa bunge bila vizuri, chama tawala cha ZANU-PF kilipata zaidi ya nusu ya viti vya bunge. Ingawa chama cha upinzani cha MDC tarehe 6 kilitoa taarifa ikisema kuwa imepata ushahidi kuhusu udanganyifu mbaya wa chama tawala katika uchaguzi, na kusema kuwa kitakabidhi ushahidi huo kwa Jumuiya ya maendeleo ya kusini mwa Afrika, lakini kutokana na hali ya pande mbalimbali, maoni tofauti ya chama cha upinzani hayawezi kubadilisha matokeo ya uchaguzi wa bunge wa Zimbabwe.
Kwanza, msimamo wa wapiga kura wa Zimbabwe ni sababu kubwa ya kutoweza kubadilisha matokeo ya uchaguzi kutokana na ushahidi uliotolewa na chama cha MDC. Hivi sasa hali ya nchini Zimbabwe ni tofauti kabisa na ile ya kufanya uchaguzi mkuu wa bunge mwaka 2000. Wakati huo mapendekezo ya chama cha MDC kilichoanzishwa kwa mwaka mmoja yalivutia wapiga kura wengi, na nchi za magharibi pia zilikuwa na matumaini makubwa na chama hicho, lakini kiliweza kupata viti 57 na kuvunja hali ya kuwepo kwa chama kikubwa kimoja tu cha ZANU PF. Katika miaka ya hivi karibuni, ili kuweza kudumisha hadhi ya utawala na kupata ushindi katika uchaguzi huo, Chama cha ZANU PF kilifanya maandalizi ya kutosha. Si kama tu kilitekeleza mageuzi ya ardhi na kuwapatia ardhi wakulima wengi ambao hakuwa na ardhi, pia kiliongeza nguvu ya kupambana ufisadi, na kuwaadhibu wafisadi ndani ya chama tawala. Hatua hizo zimewafurahisha sana wananchi, hivyo si hali ya ajabu kwa chama tawala kupata theluthi mbili ya kura zilizopigwa katika uchaguzi huo. Lakini mapendekezo ya uchaguzi ya chama cha MDC katika uchaguzi huo yalikosa mvuto kwa wapiga kura, hivyo kilipata viti 41 tu katika uchaguzi, viti hivyo ni vichache kuliko awamu iliyopita, lakini matokeo hayo si ya kushangaza. Baada ya uchaguzi, Chama cha ZANU PF kiliwataka wapiga kura waache migongano na kufanya juhudi za pamoja kwa ajili ya ujenzi wa taifa, mwito huo uliitikiwa na wapiga kura wengi, watu wanataka kuona amani na utulivu wa taifa. Katika hali hiyo, juhudi za chama cha MDC za kutaka kubadilisha matokeo ya uchaguzi haziwezi kuungwa mkono na wananchi.
Aidha, ushahidi kiliousema chama cha MDC haukubaliwi na idara husika. Tarehe 2 baada ya matokeo ya uchaguzi kujulikana, Chama cha MDC kilisema kuwa idadi ya wapiga kura katika majimbo 32 ya uchaguzi kati ya majimbo 120 nchini humo hailingani na hali halisi. Baada ya kufanya uchunguzi, tume ya wachunguzi ya Jumuiya ya maendeleo kusini mwa Afrika ilitoa hoja kuwa uchaguzi huo wa bunge umeonesha nia ya wananchi wa Zimbabwe, na uchaguzi huo ulifanyika kwa amani, wazi na kutegemeka na uliandaliwa vizuri. Ushahidi wa chama cha upinzani si wa kutosha, tume ya wachunguzi haiwezi kuthibitisha hali ya udanganyifu inayolaumiwa na chama cha upinzani.
Ingawa serikali ya Zimbabwe ilikuwa na uhasama na nchi za magharibi kama vile Uingereza na Marekani, lakini serikali hiyo bado inaungwa mkono na nchi nyingi katika sehemu ya kusini mwa Afrika. Kama jumuiya ya maendeleo ya kusini mwa Afrika utaunga mkono ushahidi wa chama cha MDC na kubadilisha matokeo ya uchaguzi mkuu wa Zimbabwe, hii hakika ingefanya chama tawala cha Zimbabwe na chama cha upinzani cha nchi hiyo kuanzisha tena mgogoro, na kuathiri amani na utulivu wa nchi hiyo na sehemu ya kusini mwa Afrika, nchi yoyote ya kusini mwa Afrika haitaki kuona hali kama hiyo. Na Jumuiya ya maendeleo kusini mwa Afrika inayobeba jukumu kubwa la kulinda amani na utulivu wa kikanda haiwezi kupokea hoja ya chama cha upinzani.
Zaidi ya hayo, pendekezo la chama cha MDC halikupata uungaji mkono mkubwa wa nchi za Uingereza na Marekani.
Idhaa ya Kiswahili 2005-04-07
|