Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2005-04-08 15:08:53    
Kuruhusiwa mabasi kwenda Kashmir kwahimiza maendeleo ya uhusiano kati ya India na Pakistan.

cri

Mabasi yaliruhusiwa rasmi tarehe 7 kupita kati ya mji mkuu Srinagar wa Kashmir inayodhibitiwa na India na mji mkuu Muzaffarabad wa Kashmir inayodhibitiwa na Pakistan. Ingawa tukio la kuyashambulia mabasi lilitokea siku hiyo, lakini abiria wa pande hizo mbili wote waliwasili salama kwenye miji hiyo. Hii ni mara ya kwanza kwa mabasi kuruhusiwa kupita kati ya sehemu mbili za Kashmir katika miaka karibu 60 iliyopita. Hayo ni mafanikio makubwa yaliyopatikana katika mchakato wa maafikiano kati ya India na Pakistan ambayo yana umuhimu kwa kuendeleza kuhimiza uhusiano kati ya nchi hizo mbili.

Siku hiyo, waziri mkuu wa India Bw. Manmohan Singh alipohutubia sherehe ya kuruhusiwa mabasi kupita alisema kuwa hiyo ni hatua ya kwanza iliyopigwa kwenye njia ndefu ya amani ya nchi hizo mbili India na Pakistan. Saa tano asubuhi ya siku hiyo, mabasi mawili ya pande hizo mbili yalifunga safari kutoka Srinagar na Muzaffarabad na kuwapeleka abiria upande mwingine.

Tarehe 16 mwezi Februari mwaka huu, India na Pakistan zilifikia makubaliano kuhusu kuruhusu kupita mabasi kati ya Kashmir inayodhibitiwa na India na inayodhibitiwa na Pakistan. Hatimaye, pande hizo mbili zilifanya juhudi kubwa ili kuyaruhusu mabasi kupita.

Kuruhusiwa kwa mabasi kupita huko Kashmir sio tu kumehimiza kukutana kwa jamaa waliotenganishwa kwa mstari unaodhibitiwa, bali pia kumeleta athari kubwa kwa ajili ya kutatua suala la Kashmir kwa nchi hizo mbili, na kutimiza amani katika sehemu hiyo hakika kutasaidia maendeleo ya uhusiano kati ya nchi hizo mbili. India siku zote inajaribu kuwa nchi kubwa duniani, lakini mgogoro wa Kashmir umeisumbua India kwa muda mrefu. Kwa Pakistan, hali ya wasiwasi na kukabiliana kijeshi katika sehemu ya Kashmir kumeleta mzigo mkubwa kiuchumi, kutimiza amani kutasaidia maendeleo ya uchumi ya Pakistan. Gazeti la India Times lilieleza, kufanikiwa kuyaruhusu mabasi kupita katika sehemu ya Kashmir, sio tu kumeondoa wasiwasi kwa watu, bali pia kumewawezesha watu waone mustakbali wa juhudi za amani kati ya India na Pakistan.

Sasa, India na Pakistan zote zina wasiwasi kutokana na kuruhusu kupita mabasi kwa muda mrefu na kutimiza kupitika kwa mstari unaodhibitiwa kati ya raia wa sehemu mbili za Kashmir. Kwani misimamo ya kikanuni ya nchi hizo mbili katika suala la Kashmir haitasuluhishwa kirahisi na bado kuna tofauti kubwa katika suala hilo.

Lakini, vyombo vya habari vinaona kuwa, bila kujali kama mabasi hayo yanaweza kusafiri kati ya sehemu mbili za Kashmir kwa muda mrefu au la. Safari hii, kuruhusu kupita mabasi kutahimiza maendeleo ya uhusiano kati ya nchi hizo mbili. Rais Musharraf wa Pakistan ataitembelea India tarehe 17 mwezi huu kutokana na mwaliko wa waziri mkuu wa India Bw. Manmohan Singh. Bw Singh pia alieleza kuwa anapenda kufanya mazungumzo kuhusu masuala yote na Musharraf wakati wowote. Wachambuzi wanaona kuwa kutokana na kuhimizwa na msimamo wa kufuatilia mambo halisi, mafanikio mengi yatapatikana katika uhusiano wa nchi hizo mbili.

Idhaa ya kiswahili 2005-04-08