Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2005-04-11 15:47:50    
Mji mdogo wa Boao

cri
Mji mdogo wa Boao uko katika mji wa Qunhai mkoani Hainan, kusini kabisa mwa China. Katika miaka kadhaa iliyopita, mji huo ulikuwa ni mji mdogo wa pwani usiojulikana. Kuanzia mwaka 2001, jina Boao limehusiana na Baraza la Asia, kwani kila ifikapo majira ya mchipuko, mkutano wa mwaka wa Baraza la Asia hufanyika huko. Kutokana na hayo mji huo mdogo umekuwa sehemu yenye vivutio vya utalii nchini China.

Uliosikia ni wimbo uitwao "maji ya mto Wanquan ni safi sana", wimbo huo unajulikana nchini China. Mto Wanquan ni mto wenye maji safi. Mji mdogo Boao uko kwenye mlango wa kuingia baharini kwa maji ya mto huo.

Mto Wanquan ni mto unaohifadhiwa vizuri kwa mazingira yake ya asili ya kanda ya tropiki nchini China, mto huo unazungukwa na miti mingi, mandhari yake inapendeza sana, hata wataalamu wa hifadhi ya mazingira wa Umoja wa Mataifa waliowahi kutembelea huko waliusifu mji wa Boao kuwa ni "mlango wa kuingia baharini kwa maji ya mto ambao mazingira yake ya asili yamehifadhiwa vizuri zaidi kuliko sehemu nyingine duniani.

Katika sehemu ya mlango huo kuna ufukwe wenye umbo la peninsula, sehemu hiyo inaitwa ufukwe wa ukanda wa jade. Wakati mawimbi ya bahari yalipokuja, ufukwe ukabadilika kuwa mwembamba kabisa wenye mita 10 tu, ukiuangalia kwa mballi ufukwe huo unaonekana kama ukanda wa jade ulioko kati ya bahari ya kusini na mto Wanquan. Dada Zhao Min aliyewahi kufika huko alisifu sana mandhari yake akisema:

Ufukwe wa ukanda wa jade kweli ni wenye mandhari nzuri sana, ambao ni kama mstari wa mpaka ambao unatenganisha maji ya mto na maji ya bahari. Pwani ya huko pia ni nzuri sana, watu wakitembea huko wanajisikia vizuri. Nimewahi kutembelea pwani ya dhahabu ya Australia (Gold Coast of Australia) naona mandhari nzuri ya ufukwe wa ukanda wa jade ni sawasawa na ile ya pwani ya dhahabu ya Australia.

Katika sehemu iliyo karibu na ufukwe huo kuna mawe mengi makubwa yanayosimama kidete kama milima yenye miamba mirefu, mawe hayo yanajulikana kwa jina lake Shenggong. Kuna hadithi moja inayohusu mawe ya Shenggong, dada Zhang alituelezea akisema:

Inasemekana kuwa, zamani sana mbingu ilibomoka kwa ghafla, na mafuriko ya siku nyingi mfululizo yakatokea duniani, ambapo raia waliteseka sana. Wakati huo malaika Niuwa alikata shauri ya kuondoa balaa kwa ajili ya raia, akayeyusha mawe yenye rangi mbalimbali ili kuziba mwanya wa mbingu. Lakini siku moja alipoyeyusha mawe, kwa bahati mbaya jiwe moja lenye rangi mbalimbali lilianguka chini na kufika kwenye sehemu ya mlango wa kuingia bahari ya bandari la Boao, hiyo ndiyo sababu ya kuwepo kwa mawe ya Shenggong katika sehemu hiyo mpaka sasa.

Hadithi nzuri iliyapa mawe ya Shenggong hali ya mwujiza, na kuyafanya yawe mawe ya kuabudiwa na wavuvi wa huko. Kila wanapofunga safari kwenda baharini kuvua samaki, wavuvi hutoa heshima na adabu zao kwa mawe hayo, ili kuomba warudi salama.

Sehemu ya Boao ni yenye utulivu na salama, lakini hivi sasa Boaa inaendelea kwa haraka na kuwa sehemu yenye vivutio vya utalii duniani. Miundo mbinu ya huko imekamilika, na pia kuna mahoteli na mikahawa pamoja na viwanja vya michezo. Kila ifikapo jioni, watalii wakikaa kwenye mikahawa iliyoko karibu na bahari, wanajiburusha katika mandhari nzuri ya huko huku wakionja vitoweo vingi vizuri vya kienyeji, kwa kweli wanasikia raha mustarehe.

Idhaa ya kiswahili 2005-04-11