Tarehe 10 serikali ya Ujerumani ilifanya maadhimisho ya miaka 60 ya ukombozi wa kambi ya wafungwa katika mji maarufu wa kihistoria Weimar, mashariki mwa Ujerumani. Chansela wa Ujerumani Gerhard Schroeder alipohutubia maadhimisho hayo alisisitiza kuwa Ujerumani inapaswa kuwajibika na ukatili wa Nazi, kisiasa na kimaadili, Wajerumani lazima waikumbuke historia hiyo na wasiruhusu itokee tena.
Kambi ya wafungwa ya Buchenwald ilijengwa 1937 kwenye kiunga cha mji wa Weimar, mwanzoni waliofungwa huko walikuwa wafungwa wa kisiasa, Wayahudi na Wagypsy, baada ya vita vya pili vya dunia kuanza walifungwa Wayahudi na mateka wa kivita. Vita vya pili vya dunia vilipomalizika wafungwa walifikia zaidi ya laki mbili na elfu 50, na miongoni mwao elfu 56 walikufa katika kambi hiyo. Tarehe 11 Aprili mwaka 1945 kambi hiyo ilikombolewa na jeshi la muungano dhidi ya ufashisti, watu elfu 21 waliokolewa.
Chansela Schroeder, spika wa bunge Wolfgang Thierse, na spika wa baraza la juu Matthias Platzeck, na wajumbe 1200 waliotoka kutoka nchi 26 wakiwa pamoja na askari waliookolewa katika kambi hiyo na wajumbe wa vijana kutoka sehemu mbalimbali za Ulaya walihudhuria maadhimisho hayo. Baada ya maadhimisho Bw. Schroeder akiwa pamoja na wajumbe wa waliookolewa kwenye kambi hiyo walikwenda kwenye kumbukumbu ya kambi hiyo wakiweka mashada ya maua mbele ya mnara wa kuwakumbuka waliouwawa.
Maadhimisho ya miaka 60 ya ukombozi wa kambi ya wafungwa ya Buchenwald ina maana kwa historia na kwa leo. maadhimisho hayo ni kama utangulizi wa kuadhimisha mwaka wa 60 tokea ushindi wa vita dhidi ya ufashisti. Hivi sasa watu waliookolewa kwenye kambi ya Buchenwald na kambi nyingine katika vita vya pili vya dunia wamekuwa wazee, wengi wao huenda ni mara yao ya mwisho kuhudhuria maadhimisho kama hayo. Namna ya kuitambua historia na kuifanya isirudie tena katika siku za usoni na kutoiacha historia isahauliwe pamoja na wazee hao kuiaga dunia, ni kazi ya maana ya hivi sasa. Kwenye hotuba Bw. Schroeder alisema, kumbukumbu pengine itafifia kadiri siku zinavyopita, lakini inatukumbusha kwamba tusisahau yale ya zamani na kabisa tusikatae mambo ya zamani.
Bw. Schroeder alisema, Ujerumani kamwe haitaruhusu kuwepo kwa nguvu zisizo za haki, na kabisa haitaruhusu utetezi wa kupinga uyahudi, na ukabila. Na kwamba Ujerumani inawajibika na ukatili wa Nazi kisiasa na kimaadili, watu wa Ujerumani lazima waikumbuke historia, wasiisahau daima na kwa uthabiti wapambane dhidi ya ukatili wowote usio wa haki. Watu wa Ujerumani wanapaswa watoe mchango kwa ajili ya kulinda amani na uhuru na kuleta hali nzuri ya siku za baadaye duniani, hilo sio jukumu la kizazi cha sasa tu, bali pia ni jukumu la vizazi vya baadaye vya Ujerumani.
Mkurugenzi wa kamati ya waliookolewa katika kambi ya Buchenwald Bw. Bertrand Herz alsema, ingawa miaka 60 imepita, lakini "Ahadi ya Buchenwald" ya kufyeka kabisa Unazi bado haijatimizwa. Leo nguvu za siasa kali za mrengo wa kulia zimefufuka tena, chama cha nguvu hizo katika majimbo ya Sachsen na Brandenburg kimeingia katika bunge, vituko vilivyopangwa na nguvu za siasa kali za mrengo wa kulia vinatokea mara kwa mara. Nguvu za kupinga Uyahudi zimeanza kuibuka, na ukabila bado upo. Yote hayo yanatuambia kuwa ni kuwa kuwafanya vijana wengi zaidi waitambue hisotia, na kwa hiyari yao wabebe majukumu ya historia, ndipo msiba wa historia hiyo hautarudia tena, na amani na utulivu wa dunia unaweza kuhakikishwa. Kwa hiyo maana kubwa ya makumbusho ya ukombozi wa kambi ya wafungwa ya Buchenwald ni kuwafanya vijana wasisahau historia na kuendelea kufanya juhudi kwa ajili ya mustakbali mzuri wa siku za usoni.
Idhaa ya kiswahili 2005-04-11
|