Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2005-04-11 16:49:11    
Mradi wa kufikisha matangazo ya redio na televisheni kwenye kila kijiji nchini China wapata mafanikio makubwa

cri

Hivi karibuni mkutano kuhusu mradi wa kufikisha matangazo ya redio na televisheni kwenye kila kijiji nchini China ulifanyika katika mkoa wa Guangxi, mkutano huo umeweka kiwango kipya cha mradi huo.

China ni nchi yenye milima mingi, hali ya uchumi inatofautiana katika sehemu tofauti, wakulima wengi wanaoishi katika sehemu maskini na sehemu za mbali zisizo rahisi kufikika hawawezi kusikiliza matangazo ya redio na kukangalia televisheni. Ili kutatua tatizo hilo, China ilianzisha Mradi wa Kufikisha Matangazo ya Redio na Televisheni kwenye Kila Kijiji mwishoni mwa karne iliyopita. Baada ya juhudi za miaka sita, mafanikio makubwa yamepatikana.

Kijiji cha Quancun kiko katika sehemu yenye milima, umbali wa kilomita 16 na mji mkuu wa wilaya, ingawa mazingira ya kimaumbile ya kijiji hicho si mabaya, lakini kabla ya mradi huo kuanza kutekelezwa wenyeji wa sehemu hiyo kiasi cha theluthi moja walikuwa hawawezi kusikiliza matangazo ya redio wala kuangalia televisheni. Hivi sasa usikivu wa redio na matangazo ya televisheni katika sehemu hiyo ni mazuri. Mwanakijiji Bw. Mo Xianshou alisema,

"Mradi huo umetuletea idhaa nyingi za televisheni, kwa kuangalia televisheni tumeweza kufahamu siasa na sera za taifa na shughuli za serikali ya mitaa, redio na televisheni zinatusaidia sana uchumi wetu."

Kijiji kingine cha Tingshe kiko karibu na mji wa Laibin kwa kilomita 35 mkoani Guangxi, kuna wanakijiji 450 katika familia 82. Wakati wa sikukuu ya taa ya Kichina kijiji hicho cha milimani kimetimiza "ndoto ya kupata matangazo ya redio na televisheni". Mkuu wa Idara kuu ya Matangazo ya Redio na Televisheni Bw. Wang Taihua alifika kwenye kijiji hicho nyumbani kwa Huang Zhengxian, wakaanza kuzungumza,

Wang: "Unafurahia idhaa gani zaidi?"

Huang: "Idhaa ya saba, idhaa ya kilimo."

Wang: "Wengi wanafurahia idhaa hiyo, ni idhaa ya elimu ya kilimo. Unafaidika na idhaa hiyo?"

Huang: "Sana. Kwa kuangalia idhaa hiyo nimeelewa mambo mengi ya kilimo. Sasa nafahamu namna ya kupanda, kutia mbolea na kupalilia shamba la miwa yangu."

Wang: "Kwa hiyo televisheni ni kama shule ya nyumbani kwako,

mtaalamu wako wa mambo ya kilimo, na tena ni mwalimu wa kukufundisha muziki na ngoma eh!" (kicheko)

Tokea mradi huo uanzishwe mwaka 1998 vijiji laki 1.2 vyenye wakulima milioni 70 vilivyokuwa na umeme vimepata matangazo ya redio na televisheni.

Kuanzia mwezi Agosti mwaka 2004, China imeanzisha mradi

wa kuvipatia vijiji vyenye familia zaidi ya 50 kwa kila kijiji kilichopatiwa umeme matangazo ya redio na televisheni. Katika sehemu za milima mkoani Guangxi kwa mfumo wa waya na mfumo usio wa waya, familia zenye watu milioni 1.1 zimetatuliwa tatizo la kutopata matangazo ya redio na televisheni. Kuna vijiji 8400 kama kijiji cha Quancun na kijiji cha Tingshe, katika sehemu hiyo, ambavyo vimewekwa katika mradi huo wa kuvipatia vijiji vyenye familia zaidi ya 50 kila kimoja.

Mradi huo umebadilisha hali ya kuwa nyuma vijijini. Kutokana na kuangalia televisheni na kusikiliza matangazo ya redio, wakulima wameweza kupata habari za nje, wanapata elimu na maisha yao yamestawi. Wakulima wanasema: Kutokana na kusikiliza matengazo ya redio na kuangalia televisheni, masikio yao yamezibuka, macho yao yamefumbuka, wao wameerevuka na maisha yao yana matumaini."

Kuhusu mafanikio yaliyopatikana katika Mkoa wa Guangxi naibu mkuu wa Idara Kuu ya Matangazo ya Redio na Televisheni Bw. Zhang Haitao alisema,

"Mradi huo unaotekelezwa mkoani Guangxi unaongoza na umekuwa kama ni mfano na msukumo kwa sehemu nyingine nchini China. Vijiji tulivyovitembelea, baadhi vinaweza kupata idhaa za televisheni zaidi ya 30 na vingine vinapata idhaa zaidi ya 10, picha na sauti zote ni safi."

Mafanikio yaliyopatikana katika Mkoa wa Guangxi ni ya mwanzo. Hivi sasa bodo kuna vijiji zaidi ya laki nne ambavyo havijapata matangazo ya redio na televisheni, na vijiji hivyo vingi viko katika sehemu ya katikati na ya magharibi, sehemu ambazo ni maskini na mbali. Vijiji hivyo ni vidogo, mazingira yake ya kijiografia ni mabaya, hali ya uchumi ni mbaya, habari za nje hazipatikani na maisha ya utamaduni ni duni. Kwa hiyo wakulima wanatamani sana kupatiwa matangazo ya redio na televisheni. Kazi ya mradi huo bado ni ngumu."

Kutokana na hali hiyo, Idara Kuu ya Matangazo ya Redio na Televisheni imeweka lengo la kuvipatia vijiji elfu 90 vyenye familia zaidi ya 50 kwa kila kimoja mwaka 2005, na kuhakikisha vijiji hivyo vinapata idhaa za televisheni zisizopungua nne na idhaa za redio zisizopungua mbili.

Wasikilizaji wapendwa, mlikuwa mkisikiliza maelezo kuhusu mradi wa kufikisha matangazo ya redio na televisheni kwenye kila kijiji nchini China. Shukrani kwa kutusikiliza. Kwaherini.

Idhaa ya kiswahili 2005-04-11