Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2005-04-11 20:35:20    
Usimamishaji wa vita kati ya Palestina na Israel uko hatarini

cri

Siku za karibuni migogoro kati ya Palestina na Israel ilizuka tena. Tarehe 9, askari wa Israel waliwaua vijana watatu wa Palestina katika sehemu ya kusini mwa Gaza na kusababisha ghadhabu kubwa kwa Wapalestina. Hatimaye, watu wenye silaha wa Palestina walirusha mabomu kadhaa yasiyo ya kawaida kwenye makazi ya Wayahudi yaliyoko katika sehemu ya Gaza ili kulipiza kisasi. Kwa upande mwingine, kundi la watu wenye msimamo mkali wa Israel walipiga kelele wakitaka kushambulia Temple Mount, sehemu takatifu ya waumini wa kiislam iliyoko mjini Jerusalem, kujaribu kuchochea mgogoro wa kidini na kumzuia waziri mkuu wa Israel Bw. Ariel Sharon asitekeleze mpango wake wa upande mmoja. Kusimamishwa vita kati ya Palestina na Israel kunakabiliwa tena hali ya hatari.

Tarehe 10, Wapalestina elfu kadhaa wenye ghadhabu walibeba maiti za vijana watatu wa Palestina zilizofunikwa na bendera ya taifa ya Palestina, kwa kupiga makelele ya kulipiza kisasi na kuwafanyia mazishi. Msemaji wa kundi la Hamas alisema kuwa Wapalestina hawawezi kuvumilia tukio hilo bila kikomo na watapiga moyo konde kuishinda Israel bila kujali chochote. Baadaye watu wenye silaha wa Palestina waliyashambulia vikali kabisa makazi ya Wayahudi tangu mwezi Februari mwaka huu.

Tukio la ufyatuaji wa risasi lilileta hali ya hatari katika sehemu ya Temple Mount. Kabla ya siku kadhaa, makundi kadhaa yenye msimamo mkali ya Israel yalisema yataandamana huko Temple Mount tarehe 10 ili kuwalazimisha polisi wa Israel walioko katika sehemu ya Gaza warudi mjini Jerusalem na kuweka vikwazo kwa mpango wa upande mmoja unaotekelezwa na serikali ya Sharon. Utawala wa Israel una wasiwasi kuwa makundi yenye msimamo mkali ya Israel na Waislam watapambana huko Temple Mount.

Ili kudhibiti hali ya hivi sasa, polisi ya Israel imewatuma askari elfu 3, kuimarisha ulinzi katika mji wa zamani wa Jerusalem na kuwatia nguvuni wanachama kadhaa wa makundi yenye msimamo mkali waliotaka kuingia Temple Mount. Kutokana na kuzuiliwa na polisi wa Israel, mpango wa wanachama hao wa kuandamana huko haukufanikiwa.

Vyombo vya habari vinaona kuwa katika hali ya hivi sasa, pande mbili zote zimetekeleza msimamo wa kujizuia. Ingawa makundi ya kisilaha ya Palestina yalirusha mabomu kwenye makazi ya Wayahudi, lakini mabomu hayo hayakusababisha hasara kubwa. Jeshi la Israel pia halikujibu mashambulizi kwa makundi yenye silaha ya Palestina. Waziri wa ulinzi wa Israel Bw. Shaul Mofaz alieleza matumaini yake kuwa pande mbili za Palestina na Israel zitajitahidi kutuliza tukio hilo kama tukio la kisehemu na kutofanya hali ya hivi sasa izidi kuwa mbaya.

Watu wote wanatumai kuwa, pande hizo mbili zitashughulikia tukio hilo kwa utaratibu na kuzuia mgogoro mkubwa wa kumwaga damu usitokee tena.

Idhaa ya kiswahili 2005-04-11