Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2005-04-13 14:56:21    
Ziara ya waziri mkuu wa China italeta athari kubwa nzuri katika kusukuma mbele urafiki na ushirikiano kati ya China na nchi za Asia ya kusini

cri

Waziri mkuu wa China Wen Jiabao alifanya ziara rasmi kutokana na mwaliko wa Pakistan, Bangladesh, Sri Lanka na India kuanzia tarehe 5 hadi 12 Aprili. Katika ziara yake, waziri mkuu Wen Jiabao alikuwa na pilikapilika za kufanya mazungumzo na mikutano, kutoa hotuba na kufanya ukaguzi. Waziri wa mambo ya nje wa China Bwana Li Zhaoxing aliyefuatana na waziri mkuu katika ziara yake alisema kuwa, ziara hiyo ni ya urafiki, ujirani mwema na ushirikiano na unaoelekea siku za usoni.

Mawasiliano ya kirafiki kati ya China na Asia ya kusini yana historia ndefu. Baada ya kuanzishwa kwa Jamhuri ya watu wa China, uhusiano wa kirafiki kati ya China na nchi mbalimbali za Asia ya kusini umeendelea siku hadi siku chini ya juhudi za pamoja za serikali za nchi mbalimbali na wananchi wao. Baada ya kuingia karne ya 21, ushirikiano kati ya China na nchi za Asia ya kusini katika sekta mbalimbali umeendelea kwa nguvu kubwa.

China na nchi za Asia ya kusini zote ni nchi zinazoendelea, ambazo zinaweza kusaidiana kiuchumi, na zina nguvu kubwa ya ushirikiano. Katika ziara yake hiyo, waziri mkuu Wen Jiabao na viongozi wa nchi alizotembelea walifikia maoni ya pamoja kuhusu mambo mengi mapya na njia mpya za kuzidisha ushirikiano wa kunufaishana, na kuthibitisha taratibu mpya na mipango mipya mingi ya kuanzisha ushirikiano wa muda mrefu na wastani. Katika ziara yake hiyo, China na nchi hizo 4 zilisaini nyaraka 53 za pande mbili mbili, theluthi mbili ya nyaraka hizo zinahusu ushirikiano wa kiuchumi na kibiashara, ambazo zitapanua zaidi sekta za ushirikiano, kuinua kiwango cha ushirikiano, kuimarisha hatua za kurahisisha uwekezaji na kufanya ujenzi wa sehemu za biashara huria upate maendeleo. Bwana Li Zhaoxing anaona kuwa, ushirikiano wa kunufaishana kati ya China na Asia ya kusini unasaidia utulivu na usitawi wa Bara la Asia, na pia unasaidia nchi zinazoendelea ziweze kukabiliana vizuri zaidi na changamoto ya utandawazi wa uchumi duniani.

Ziara ya India ni ziara muhimu zaidi katika safari hiyo ya waziri mkuu Wen Jiabao. Katika ziara hiyo, waziri mkuu Wen Jiabao alibadilishana maoni kwa dhati na kwa kina na viongozi wa India na kufikia maoni ya pamoja kuhusu kanuni za uelekezaji wa kisiasa wa utatuzi wa suala la mpaka, ambapo pande hizo mbili zilitoa waraka wa kwanza wa kisiasa kuhusu utatuzi wa suala la mipaka katika zaidi ya miaka 20 iliyopita na kuweka msingi mzuri kwa kufanya mazungumzo ya amani ili kutatua kwa haki na mwafaka suala la mipaka. Bwana Li Zhaoxing alisema kuwa, matokeo ya ziara hiyo yameonesha kuwa China imetekeleza kwa moyo wa dhati sera ya kujenga ujirani mwema, kuweka mazingira ya usalama na nchi jirani na kushirikiana na nchi jirani kupata maendeleo kwa pamoja, hii inasaidia China na nchi mbalimbali za Asia ya kusini ziimarishe auminifu, kushika njia ya maendeleo ya amani na kujenga mazingira ya kirafiki.

Katika ziara yake hiyo, waziri mkuu Wen Jiabao aliwapa pole kwa dhati na vifaa vya misaada wananchi wa Sri Lanka waliokumbwa na maafa kutokana na tetemeko la ardhi kwenye Bahari ya Hindi mwishoni mwa mwaka jana na kuwa.

Katika ziara yake hiyo, China na Pakistan, India, Bangladesh na Sri Lanka zimebainisha wazi uhusiano wa ushirikiano wa kimkakati, hii imeonesha kuwa urafiki na ushirikiano kati ya China na Asia ya kusini umeingia katika kipindi kipya cha maendeleo. Ziara ya waziri mkuu Wen Jiabao imetimiza lengo la kuongeza uaminifu, kuzidisha urafiki, kupanua ushirikiano na kuweka mipango ya kujenga siku za usoni, ziara hiyo italeta athari kubwa nzuri kwa urafiki na ushirikiano kati ya China na Asia ya kusini katika sekta zote.

Idhaa ya kiswahili 2005-04-13