Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2005-04-14 14:07:31    
Umoja wa Mataifa wapitisha mkataba wa kimataifa wa kuzuia vitendo vya ugaidi vya nyuklia

cri

Mkutano mkuu wa 59 wa Umoja wa Mataifa tarehe 13 ulipitisha Mkataba wa Kimataifa wa Kuzuia Vitendo vya Ugaidi vya Nyuklia (International Convention for the Suppression of Acts of Nuclear Terrorism). Haya ni matokeo ya juhudi za miaka minane zilizofanywa na nchi wanachama wa Umoja wa Mataifa.

Mkataba huo umebaini tafsiri ya vitendo vya ugaidi vya nyuklia ambavyo vimegawanyika katika sehemu: Moja ni kumiliki zana zenye vitu vya mionzi ya madhara na nyuklia vinavyolenga kumdhuru binadamu, mali na mazingira; Pili ni kuwa kwa lengo hilo kutumia vitu vyenye mionzi ya madhara na zana za nyuklia au kuharibu zana za nyuklia; Tatu ni kutishia kutumia vitu vyenye mionzi ya madhara na nyuklia kwa ajili ya kutimiza lengo hilo.

Mkataba huo unataka serikali za nchi mbalimbali zitunge sheria kwa mujibu wa mkataba huo ili kuhakikisha vikundi na watu binafsi wanaoshiriki kupanga na kutenda vitendo vya ugaidi wanaadhibiwa. Na kwamba unataka nchi zote wanachama wa Umoja wa Mataifa ziaimarishe ushirikiano ikiwa ni pamoja na kupashana habari na kutilia mkazo usimamizi wa matumizi ya vitu vyenye mionzi vyenye madhara.

Katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa Bw. Kofi Anna kwenye mkutano alifurahishwa na kupitishwa kwa mkataba huo. Alisema, hii ni hatua kubwa ya ushirikiano wa pande mbalimbali za jumuyia ya kimataifa katika juhudi za kuzuia vitendo vya ugaidi, na mkataba huo utasaidia kuimarisha mfumo wa kimataifa dhidi ya ugaidi. Alizihimiza nchi zote zimalize mapema mswada wa mkataba huo. Imefahamika kuwa Bw. Kofi Anna atawasilisha mkataba huo kwenye mkutano wa viongozi wa Umoja wa Mataifa na kutiwa saini.

Mkataba huo ni moja ya mikataba ya kimataifa 13 iliyopitishwa na Umoja wa Mataifa kuhusu mapambano dhidi ya ugaidi. Ugaidi ulioanzia miaka ya 70 ya karne iliyopita na kuendelea hadi sasa umeenea nje ya mipaka ya mataifa, vitendo vyake vimekuwa vya kikatili zaidi, na njama zake zimekuwa za siri zaidi, vyombo vinavyotumika kwa ugaidi vimekuwa vya kisasa zaidi, na maafa yake ni makubwa zaidi. Tukio lililotokea tarehe "11 Septemba" mwaka 2000 lilifikisha ugaidi kwenye "kilele". Katika siku hizi ambapo teknolojia zimeendelea sana, hata maboksi kadhaa ya maziwa yanatosha kwa kutengeneza mabomu ya nyuklia kwa kutumia uranium, kama teknolojia hiyo ikiwa mikononi mwa magaidi matokeo yatakuwa mabaya yasiyoweza kukadirika. Kwa hiyo baadhi ya watu wanasema kuwa katika karne ya 21 matishio matatu hapa duniani ni ugaidi, ufisadi wa kisiasa na uchafuzi wa mazingira.

Ingawa serikali za nchi zote zinatilia maanani mapambano dhidi ya ugaidi baada ya tukio la "11 Septemba", lakini kutokana na kuwa mapambano dhidi ya ugaidi yanahusisha sheria za kila nchi na kuhusika na sera za zinazotumika sasa za nchi hizo katika ushirikiano wa kimataifa, mawazo ya namna moja ya tafsiri kuhusu ugaidi hayajapatikana hadi sasa. Mkataba uliopitishwa hivi sasa kimsingi unalenga kuzuia vitendo vya upande mmoja vya uharamia, utekaji nyara angani na ardhini kwa kutumia vitu vya nyuklia.

Wachambuzi wanaona kuwa shughuli za ugaidi zimekuwa tishio kubwa kwa binadamu. Nchi yoyote, yenye nguvu kubwa au dhaifu, zote zinakabiliwa na tishio hilo. Kulinda raia wasio na hatia ni jukumu la pamoja la jumuiya ya kimataifa na pia ni msingi wa mapambano dhidi ya ugaidi. Nchi zote zinapaswa kuacha maslahi binafsi na kuzuia matatizo ya kupinga ugaidi yasiwe ya kisiasa, yaani zisitumia kisingizio cha kupinga ugaidi kutekeleza utetezi wa upande mmoja, wala zisitumie kisingizio cha kulinda mamlaka ya taifa kuhamasisha na kuunga mkono ugaidi.

Tafsiri iliyowekwa na Mkataba huo uliopitishwa na Umoja wa Mataifa itasaidia jumuyia ya kimataifa kuafikiana kimawazo kuhusu ugaidi, na hii itasukuma mbele ushirikiano wa kimataifa na kupata ushindi mkubwa zaidi katika mapambano dhidi ya ugaidi.

Idhaa ya kiswahili 2005-04-14