Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2005-04-14 17:25:19    
Mkoa wa Heilongjiang wafuata njia ya maendeleo ya masikilizano kati ya viumbe na uchumi

cri

Tambarare ya "Beidahuang" iliyoko kaskazini mashariki kabisa mwa China ni ghala kubwa kabisa ya nafaka nchini China, ni moja cha vituo vya viwanda vikubwa nchini China, pia ni vivutio vya utalii wa misitu na kituo cha kuzalisha chakula kisichokuwa na vitu vya uchafuzi. Japokuwa kuna migongano kati ya hifadhi ya viumbe na maendeleo ya uchumi, lakini mkoa wa Heilongjiang unajitahidi kukuza uchumi wa maelewano kati ya viumbe na uchumi.

Takwimu zilizotolewa na idara husika ya mkoa wa Heilongjiang zimeonesha kuwa, mwaka 2004, thamani ya uzalishaji wa viwanda wa mkoa huo ulifikia yuan bilioni 162 hivi, ikiwa inaongezeka kwa asilimia 15.3 kuliko mwaka uliotangulia; eneo la kulima chakula kisichokuwa na vitu vya uchafuzi lilifikia hekta milioni 1.59, likichukua nafasi ya kwanza nchini China, na mapato yake kutokana na utalii yalikuwa yuan bilioni 25, yakiongezeka kwa asilimia 12.6 kuliko mwaka uliotangulia..

Tangu China mpya iasisiwe, mkoa wa Heilongjiang umekuwa kituo muhimu cha kuzalisha nishati, malighafi na nafaka, ukiwa umetoa mchango mkubwa katika ujenzi wa China mpya, lakini maendeleo yake pia yameleta athari mbaya kwa mazingira ya viumbe.

Katika miaka ya hivi karibuni, mkoa wa Heilongjiang imebadilisha mtizamo na mtindo wa zamani wa kuleta ongezeko la uchumi kwa kuharibu mazingira na malighafi, na kuanza kujenga mtindo mpya wa maendeleo yenye uwiano kati ya uchumi na jamii, mazingira na malighafi. Kutokana na hiyo, mwezi Oktoba mwaka 2001, mkoa huo uliidhinisha mpango wa kujenga mkoa wa viumbe.

Katika miaka kadhaa iliyopita, mkoa wa Heilongjiang umejitahidi kukuza uchumi huku ukifuatilia kuhifadhi mazingira ya viumbe, kuchukua hatua za kisheria dhidi ya shughuli haramu za kuharibu mazingira ya viumbe kama vile kuharibu misitu, nyasi na kutumia ovyo ardhieovu. Pia umechukua hatua mwafaka za kuhifadhi mazingira ya maumbile kama vile kurudisha mashamba ya kilimo kuwa misitu tena, kudhibiti mmomonyoko wa udongo. Kwa kufanya hivyo, mazingira ya viumbe ya sehemu kadhaa ya mkoa huo yameboreshwa kwa ufanisi, sambamba na hali ya maendeleo ya uchumi.

Mazingira mazuri ya viumbe ni raslimali bora ya tambarare ya "Beidahuang", pia ni chanzo kipya cha kuendeleza uchumi wa sehemu hiyo. Hivi sasa, miradi ya ujenzi wa kilimo cha viumbe, utengenezaji wa chakula kisichokuwa na vitu vya uchafuzi, na utalii wa viumbe na miradi mingine inajulikana nchini China hata duniani, imekuwa uhai mpya wa kuleta maendeleo ya uchumi wa huko.

Mkoa wa Heilongjiang ni mkoa unaozalisha nafaka nyingi zaidi nchini China. Mkoa huo umethibitisha mkakati wa kuendeleza kilimo cha viumbe na kukuza viwanda vya kutengeneza chakula kisichokuwa na vitu vya uchafuzi, ambayo imekuwa uti wa mgongo wa uchumi wa vijiji vya mkoa huo .

Utalii wa viumbe umetoa mchango mkubwa katika kuleta ongezeko la uchumi wa mkoa huo. Hivi sasa mkoa wa Heilongjiang kwa tofauti umeendesha tamasha la kimataifa la kutekeleza kwenye theluji, tamasha la kimataifa la barafu na theluji la Harbin, tamasha ya utalii wa viumbe wa misitu ya Yichuan, na matamasha mengine. Matamasha hayo yanajulikana hata duniani na kuwavutia watalii wengi wa nchini na wa ng'ambo.

Mkuu wa idara ya utalii ya mkoa wa Heilongjiang amedokeza kuwa, mwaka jana mkoa huo kwa jumla uliwapokea watalii milioni 40 wa China na watalii laki 7 na elfu 33 wa nchi za nje, idadi hiyo imeongezeka kwa 11.4% na 24.3% kwa tofauti. Hivi sasa mkoa wa Heilongjinag unajulikana nchini hata duniani kutokana na umaalum wake wa utalii wa viumbe.

"Beidahuang" ya zamani iliwavutia watu kutokana na utajiri wa rasilimali, "Beidahuang" ya leo inawafurahisha watalii kutokana na mazingira mazuri ya viumbe na usitawi wa uchumi.

Idhaa ya kiswahili 2005-04-14