Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2005-04-14 20:48:22    
Mji wa Hangzhou

cri

 

Mji wa Hangzhou uko kusini mwa Delta ya Mto Changjiang, magharibi ya Ghuba ya Hangzhou, sehemu ya chini ya Mto Qiantang na sehemu ya kusini ya Mfereji wa Jinghang. Mji huo ni kituo muhimu cha mawasiliano katika Delta ya Mto Changjiang na sehemu ya kusini mashariki mwa China. Sehemu za kaskazini magharibi na kusini magharibi za mji huo ni sehemu zenye milima midogo midogo; na sehemu za kaskazini mashariki na kusini mashariki ni tambarare ya sehemu ya kaskazini ya mkoa wa Zhejiang, ambako kuna mito mingi. Eneo la milima midogo midogo linachukua asilimia 65.6 ya eneo lote la mji huo, eneo la tambarare linachukua asilimia 26.4, na eneo la mito, maziwa na mabwawa linachukua asilimia 8.

Hali ya hewa ya Hangzhou ni ya pepo za misimu ya ukanda wa semi-tropiki. Kuna majira manne, hali ya hewa ni ya fufutende na yenye mvua nyingi. Joto la wastani kwa mwaka ni nyuzi 16.2 sentigredi, joto la wastani katika majira ya joto ni nyuzi 28.6 sentigredi, na joto la wastani katika majira ya baridi ni nyuzi 3.8 sentigredi.

  

Mazingira ya kimaumbile ya mji huo ni mazingira yenye mito, maziwa na milima. Kuna Mto Qiantang, Mto Dongtiaoxi, Mfereji Jinghang, Mfereji Xiaoshao na Mto Shangtang mjini humo. Mfumo wa Mto Qiantang ni pamoja na Mto Xin'anjiang na Mto Fuchunjiang. Bwawa la Xin'anjiang ni bwawa kubwa kabisa katika sehemu ya pwani ya mashariki mwa China. Eneo la bwawa hilo ni kilomita za mraba 570, na linaweza kujaa maji mita za ujazo bilioni 17.8. Katika bwawa hilo kuna visiwa 1078, hivyo bwawa hilo pia linaitwa "ziwa lenye visiwa elfu moja". Ziwa la Magharibi lililoko katikati ya mji wa Hangzhou ni ziwa lenye urefu wa kilomita 3.3 kutoka kusini hadi kaskazini na kilomita 2.8 kutoka mashariki hadi magharibi. Eneo lake ni kilomita za mraba 5.66. Kusini magharibi mwa mji huo kuna Mlima Tianmu, Mlima Baiji na Mlima Qianligan, na kusini mashariki mwa mji huo kuna Mlima Longmen.

Mji wa Hangzhou una historia ndefu. Pia ni moja ya machimbuko ya utamaduni wa China. Kabla ya miaka 4700 iliyopita, binadamu walianza kuishi huko na kuanzisha utamaduni wa Liangzhu.

 

Mji wa Hangzhou uliwahi kuwa mji mkuu wa dola la Wuyue katika kipindi cha Enzi Tano na mji mkuu wa Enzi ya Song ya Kusini, na ni mmoja wa miji mikuu saba ya kale nchini China.

Tarehe 3 mwezi Mei mwaka 1949, ukombozi wa mji wa Hangzhou ulifungua ukurasa mpya katika historia ya mji huo.

Mwaka 2003, mapato ya uzalishaji(GDP) ya mji huo yalikuwa zaidi ya yuan trilioni 2 na kufikia yuan 2.092. Mapato ya kilimo katika mwaka huo yalifikia yuan bilioni 12.7. Na mapato ya viwanda yalikuwa yuan bilioni 93.5. Sekta ya uzalishaji ya mji huo imekuwa na mfumo kamili, na ina uwezo mkubwa ya kukabiliana na changamoto za soko.

Idhaa ya Kiswahili 2005-04-14