Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2005-04-14 20:41:31    
China yathibitisha kimsingi mpango mkuu wa kukuza uchumi wa mzunguko

cri

Kikundi cha "Utafiti wa mkakati wa kukuza uchumi wa mzunguko wa China" katika taasisi ya utafiti wa mambo makubwa ya uchumi ya kamati ya maendeleo na mageuzi ya China kimesema kuwa, mpango mkuu wa kukuza uchumi wa mzunguko nchini China ni kutumia miaka 50 kujenga jamii ya mzunguko yenye masikilizano kati ya binadamu, maumbile na jamii na kuokoa nishati, ambapo kiasi cha uzalishaji wa raslimali, kiasi cha matumizi ya mzunguko wa raslimali na kiasi cha takataka zitakazoshughulikiwa, pamoja na mazingira ya viumbe, na uwezo wa maendeleo endelevu kufikia kiwango cha kisasa cha duniani cha wakati ule, kuinua kwa kiasi kikubwa sifa ya mazingira ya viumbe na kuboresha kikamilifu mazingira tunayoishi, ndipo nchi nzima itakapoweza kuingia kwenye mzunguko mzuri wa maendeleo endelevu.

Kwenye kongamano la ngazi ya juu kuhusu uchumi wa mzunguko wa China lililofanyika hivi karibuni hapa Beijing na taasisi ya utafiti wa maendeleo ya China, Dk. Li Zhenjing kutoka taasisi ya mfumo na usimamizi wa uchumi ya kamati ya maendeleo na mageuzi ya China alidokeza kuwa, hayo yalitolewa kwenye "ripoti ya utafiti kuhusu mkakati wa kukuza uchumi wa mzunguko wa China".

Dk. Li Zhengjing alifahamisha kuwa, kutokana na hali halisi, mpango mkuu wa mkakati wa kukuza uchumi wa mzunguko wa China unatakiwa kutekelezwa kwa vipindi vitatu:

Kipindi cha kwanza kinaanzia mwaka 2005 hadi mwaka 2010, ambapo utaanzishwa mifumo kamili wa kuhimiza maendeleo ya uchumi wa mzunguko, ambayo ni pamoja na mfumo wa sheria, mfumo wa uungaji mkono wa kisera, mfumo wa uvumbuzi wa kiteknolojia na mfumo mwafaka wa kutoa motisha.

Kipindi cha pili kitaanzia mwaka 2011 hadi mwaka 2020, ambapo utajengwa kimsingi mfumo wa uchumi na jamii wenye umaalum wa uchumi wa mzunguko, na kujenga mfumo kamili wa usimamizi na mfumo wa kisera na kisheria wa jamii ya mzunguko.

Kipindi cha tatu kitaanzia mwaka 2021 hadi mwaka 2050, ambapo itajengwa kikamilifu jamii ya mzunguko yenye masikilizano kati ya binadamu, jamii na maumbile.

Uchumi wa mzunguko ni mtindo wa kuongeza uchumi ambao kiini chake ni matumizi ya raslimali kwa ufanisi na ya mzunguko, kanuni yake ni kuokoa na kutumia tena raslimali, mtindo huo unaoendana na mtazamo wa maendeleo endelevu, ni tofauti kabisa na mtindo wa kijadi wa kuongeza uchumi kwa kuzalisha kwa wingi, kutumia kwa wingi na kuacha kwa wingi. Lengo la kukuza uchumi wa mzunguko ni kuokoa nishati na kuboresha mazingira ya viumbe katika hali ya kutoathiri maendeleo ya haraka ya uchumi na jamii, kuisukuma jamii ya binadamu katika njia ya maendeleo endelevu.

Idhaa ya Kiswahili 2005-04-14