Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2005-04-15 17:23:39    
Kwa nini matukio mengi ya milipuko kutokea tena nchini Iraq

cri

Tarehe 14 ilikuwa siku ya umwagaji damu nchini Iraq. Kwa mujibu wa matangazo ya kituo cha televisheni cha Al Jazeera, cha Qatar milipuko miwili ya mabomu yaliyowekwa katika magari ilitokea siku hiyo karibu na jengo la wizara ya mambo ya ndani mjini Baghdad na kusababisha vifo vya watu wasiopungua 18 na wengine 40 kujeruhiwa, wengi wao ni polisi wa Iraq. Zaidi ya hayo, milipuko mingi mingine ilitokea nchini Iraq na kusababisha vifo na majeruhi ya watu zaidi ya 70.

Kabla ya hapo, milipuko kadhaa ilitokea tarehe 13 mjini Kirkuk na Baghdad na kusababisha vifo vya watu 9. Jeshi la Marekani nchini Iraq siku hiyo lilithibitisha kuwa askari mmoja wa jeshi hilo aliuawa na watu wenye silaha mjini Ramadi.

Watu wanaona kuwa waziri wa ulinzi wa Marekani Donald Rumsfeld na naibu waziri wa mambo ya nje Robert Zoellick wiki hii waliitembelea Iraq kwa dharura. Bw Rusmfeld tarehe 12 aliwawekea shinikizo viongozi wapya wa Iraq kuwahimiza wakamilishe kuunda baraza la mawaziri na kuhakikisha mchakato wa kisiasa wa Iraq uendelee kwa mpango uliowekwa hapo awali. Bw Zoellick tarehe 13 alibadilishana maoni na viongozi wapya wa Iraq kuhusu kazi za siasa, uchumi na ukarabati wa usalama baada ya kuundwa kwa serikali mpya. Wachambuzi wanaona kuwa milipuko mingi iliyotokea hivi karibuni nchini Iraq inahusiana na safari za Wamarekani hao wawili nchini Iraq.

Kwanza, Rusmfeld alieleza waziwazi katika kipindi cha ziara yake kuwa, Marekani haina mpango wa kuondoa jeshi lake. Lengo la kundi lenye silaha la Iraq linalopinga ukaliaji wa Marekani kufanya mashambulizi makali, bila shaka ni kuitishia Marekani kuwa, hali ya kawaida haitaonekana nchini Iraq hadi jeshi la Marekani liondoke nchini humo.

Pili, ziara ya Bw. Rumsfeld inaonesha kuwa Marekani inataka kuharakisha kuundwa kwa serikali mpya ya Iraq na kuhimiza mchakato wa ukarabati wa siasa ili kuweka mfano wa demokrasia katika sehemu ya Mashariki ya Kati. Makundi yenye silaha ya Iraq yanafanya mashambulizi makali, kujaribu kuzuia mchakato wa ukarabati wa siasa usiendelee kwa hivi sasa bila vikwazo na kupambana na juhudi zinazofanywa na Marekani kuhusu kutekeleza demokrasia na uhuru wa kimarekani, ambapo pia ni kutishia serikali mpya itakayoundwa hivi karibuni.

Tatu, ukarabati wa usalama ni suala muhimu lililojadiliwa na Bw. Zoellick na viongozi wapya wa Iraq. Marekani inataka serikali mpya ichukue hatua halisi na mwafaka za kuyashambulia makundi yenye silaha ya Iraq. Lakini makundi hayo, hakuogopa bali yanaendelea kufanya mashambulizi.

Wachambuzi wanaainisha kuwa kama serikali mpya ya Iraq itachukua hatua mwafaka baada ya kuundwa kwake, mashambulizi hayo yanatazamiwa kuzuiliwa. Lakini iwapo jeshi la Marekani halitaondoka nchini Iraq, mashambulizi ya kuipinga Marekani hayataishia kamwe.

Idhaa ya kiswahili 2005-04-15