Kuanzia tarehe 18 hadi tarehe 24 mwezi Aprili mwaka 1955, mkutano wa kwanza wa Asia na Afrika ulifanyika mjini Bandung, Indonesia, mkutano huo ulizishirikisha nchi na sehemu zipatazo 29. Mkutano huo ulitunga kanuni kumi za kuhimiza amani na ushurikiano duniani kutokana na kanuni tano za kuishi pamoja kwa amani zilizotolewa na serikali ya China. Wakati miaka 50 ya mkutano wa Bandung inapotimia, waandishi wetu walimhoji profesa Ahmed Rasheedi wa idara ya siasa na uchumi ya chuo kikuu cha Cairo.
Miaka 50 iliyopita, chini ya juhudi za China na nchi nyingi zilizohudhuria mkutano wa Bandung, mkutano huo ulipitisha "taarifa ya mwisho ya mkutano wa Asia na Afrika" na kuthibitisha kanuni kumi za kuelekeza uhusiano wa kimataifa. Kanuni hizo kumi ni maendeleo ya kanuni tano za kuishi pamoja kwa amani zilizotolewa na marehemu waziri mkuu wa China Zhou Enlai. Profesa Ahmed Rasheedi alisifu ipasavyo kanuni tano za kuishi pamoja kwa amani zilizotolewa na Zhou Enlai, akisema:
"Marehemu waziri mkuu wa China Zhou Enlai alitoa kanuni tano za kuishi pamoja kwa amani kwenye mkutano wa Bandung na kusisitiza kuishi pamoja kwa amani kwa mataifa mbalimbali, jambo hilo bila shaka linawakilisha kanuni kuu iliyotumika katika uhusiano wa kimataifa katika miongo kadhaa baadaye. Baada ya vita vya pili vya dunia, kundi la mashariki lililongozwa na Urusi ya zamani na kundi la magharibi lililoongozwa na Marekani yaliundwa duniani. Nchi za dunia ya tatu au za kusini zilianzisha harakati zisizofungamana na upande wowote kutokana na mapendekezo ya Misri, China, Yugoslavia na India. Harakati hizo zilifuatilia sana "suala la kusini" na kuzingatia kuondoa athari mbaya za vita baridi zilizofanywa na nchi kubwa zenye mabavu kwa nchi za kusini. Kanuni tano za kuishi pamoja kwa amani siku zote ni kanuni muhimu za uelekezaji za kusawazisha uhusiano wa kimataifa kwa harakati hizo".
Profesa Rasheedi alisisitiza kuwa mabadiliko makubwa yametokea duniani baada ya vita baridi, Marekani inataka kujenga dunia ya ncha moja kwa nguvu zake kubwa na kutekeleza umwamba duniani. Katika hali hiyo, dunia inapaswa kuanzisha zaidi mazungumzo kati ya ustaarabu mbalimbali kwenye msingi wa kanuni tano za kuishi pamoja kwa amani, na hazipaswi kufanya mapambano au migogoro. Alisema:
"Baada ya tukio la tarehe 11 Septemba, Marekani imeweka shabaha yake kwa dunia ya kiarabu kwa kisingizio cha kupambana na ugaidi, hii ni hatari sana. China, nchi za kiarabu na dunia ya kiislam zina ustaarabu wao maalum na kanuni hizo tano zimejenga daraja kwa mazungumzo kati ya utamaduni na ustaarabu tofauti, kwa hiyo zina athari muhimu zenye juhudi".
Profesa Rasheedi anaona kuwa kanuni tano za kuishi pamoja kwa amani zinahusu mambo mbalimbali, kama vile kushirikiana na kusaidiana, akisema:
"Kama amani inajaa duniani, nchi mbalimbali zinaweza kufanya juhudi kubwa za kuendeleza uchumi wao, jambo hilo ni muhimu zaidi kwa nchi zinazoendelea"
Profesa Ahmed Rasheedi alisifu China itekeleze kanuni tano za kuishi pamoja kwa amani katika uhusiano wa kimataifa na kuweka mfano mzuri wa kuigwa kwa nchi nyingi zinazoendelea ikiwemo Misri.
Idhaa ya Kiswahili 2005-04-18
|