Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2005-04-19 10:27:51    
Shanxi ya himiza maendeleo ya uchumi kwa kutumia rasilimali za huko

cri

Tangu serikali ya China kutekeleza sera za kustawisha sehemu ya magharibi mwaka 2000, uchumi wa sehemu hiyo umekuwa na mwelekeo wa maendeleo ya kasi. Mko wa Shanxi ni mmoja wa mikoa ambayo serikali ya China inatekeleza sera za ustawishaji, katika miaka ya karibuni mkoa huo umepiga hatua kubwa za maendeleo ya kiuchumi kwa kutumia rasilimali nyingi za mazao ya kilimo, madini, sayansi na teknolojia.

Mkoa wa Shanxi ni mkoa mkubwa wa uzalishaji wa mazao ya kilimo, mashamba ya mkoa huo yamefikia kiasi cha hekta zaidi ya milioni 4.8, ambayo yanachukua 4% hivi ya jumla ya mashamba ya China. Katika katika muda mrefu uliopita ufanisi wa sekta ya kilimo ulikuwa ndogo kutokana na kukosa teknolojia ya kimaendeleo. Ili kuhimiza maendeleo ya kilimo, mkoa wa Shanxi licha ya kuhimiza uzalishaji wa chakula, pia unahimiza uzalishaji wa apple, mboga na maua kwa kufuatana na hali tofauti ya kimaumbile ya sehemu mbalimbali za mkoa huo. Licha ya hayo, serikali ya China ilianzisha eneo la majaribio la uzalishaji chakula kwa teknolojia ya kimaendeleo mwaka 1998 katika sehemu ya Yangling iliyoko katikati ya mkoa wa Shanxi, ambalo limekuwa la pekee la kitaifa.

Kutokana na ujenzi wa miaka zaidi ya 7, sehemu ya Yangling, ambayo ilikuwa kitongoji kilichokuwa nyuma kimaendele hapo zamani, sasa imekuwa sehemu inayohimiza maendeleo ya kilimo cha kisasa na pato lake limeziei Yuan bilioni 1.1. naibu mkurugenzi wa kamati ya usimamizi ya eneo la majaribio la Yangling bibi Chen Jun alisema,

"Njia yetu ni kuunganisha kampuni, wanasayansi, vituo vya uzalishaji na familia za wakulima, kampuni inatoa mbolea, dawa na mbegu bora kwa familia za wakulima, ambao wanaelekezwa na mafundi wa kilimo ili kuongeza uzalishaji; kwa upande mwingine kampuni yetu inanunua mazao yaliyozalishwa na familia za wakulima ili kuhakikisha wakulima wanapata faida."

Bibi Chen alisema kuwa eneo la majaribio ya Yangling linatoa huduma za uzaliishaji, mauzo na teknolojia kwa kupitia kampuni za huduma zilizoanzishwa na eneo hilo. Licha ya hayo, kamati ya usimamizi ya eneo la majaribio inawashirikisha wataalamu kueneza taknolojia ya kilimo kwa wakulima kuambatana na hali tofauti za sehemu mbalimbali. Hatua hiyo si kama tu imeongeza ufanisi wa mafanikio ya sayansi na teknolojia, bali pia ifungua uwanja kwa kampuni kueneza mazao na teknolojia mpya.

Habari zinasema kuwa tangu kuanzishwa eneo la majaribio la Yangling, teknolojia zaidi ya 600 zimeenezwa ikiwa ni pamoja na kuandaa mafunzo kwa wakulima zaidi ya milioni 3, ambayo iliongeza ufanisi Yuan zaidi ya bilioni 10 kwa mwaka. Takwimu inaonesha kuwa mwaka 2004 thamani ya uzalishaji kutokana na uzalishaji wa kilimo mkoani Shanxi imezidi 10% ya jumla ya thamani ya uchumi wa mkoa huo.

Sehemu ya magharibi ya China ina rasilimali nyingi, mkoa wa Shanxi ni moja ya mikoa yenye rasilimali nyingi ya madini katika sehemu ya magharibi ya China. Hususan ni sehemu ya kaskazini ya mkoa wa Shanxi, ambayo ina makaa ya mawe, ges ya asili na mafuta ya asili ya petroli nyingi. Katika miaka ya karibuni sekta ya nishati imepewa kipaumbele katika mkoa wa Shanxi. Mkurugenzi wa kamati ya maendeleo ya mageuzi ya Shanxi Bw. Li Xiaodong alisema kuwa hivi sasa sekta ya nishati ya Shanxi imepata maendeleo, katika siku za usoni mkoa huo utawekeza mitaji ya Yuan bilioni 200 ili kuendeleza sekta ya nishati na kazi za viwanda vya kemikali.

"Shanxi ina rasilimali nyingi za nishati, hususan makaa ya mawe, licha ya kuchimba makaa ya mawe, tunatakiwa kuongeza pato letu na pato la wakazi wa mkoa huo kwa kutumia rasilimali hiyo, kw ahiyo tumetoa wito wa kuongeza thamani ya rasilimali kwa kuzalishaji umeme na kujenga viwanda vya kemikali."

Ofisa huyo pia alisema kuwa wakati wa kuongeza ufanisi wa rasilimali, mkoa wa Shanxi unazingatia hifadhi ya mazingira ya rasilimali na asili, na kudhibiti maendeleo ya sekta zinazotumia nishati nyingi na kutoa uchafuzi mwingi.

Kwa kulinganishwa na sehemu nyingine za sehemu ya magharibi ya China, mkoa wa Shanxi una hali bora katika miundombinu, elimu, sayansi ya teknolojia, mkoa wa Shanxi ni wa kwanza kwa kuweko vyuo vikuu na taasisi za utafiti wa sayansi katika sehemu ya magharibi ya China, hali ambayo imeanzisha mazingira bora kwa uendelezaji wa sekta ya teknolojia ya kimaendeleo. Katika miaka ya karibuni, mkoa wa Shanxi umeanzisha maeneo miongo kadhaa ya ustawishaji pamoja na sayansi na teknolojia, ambayo thamani ya uzalishaji wake imechukua kiasi cha 10% ya pato la uchumi wa mkoa huo. Eneo la ustawishaji wa teknolojia ya kimaendeleo la mji wa Xian inavutia watu zaidi miongoni mwa maeneo hayo, ambalo limethabitishwa na shirika la maendeleo ya viwanda la Umoja wa Mataifa kuwa ni "moja ya miji na sehemu zenye uhasama mkubwa nchini China".

Eneo la ustawishaji wa teknolojia ya kimaendeleo la Xian lilianzishwa kabla ya miaka 15 iliyopita, baada ya kuendelezwa kwa miaka zaidi ya 10, eneo hilo limekuwa sekta kubwa za mawasiliano ya zana za elektroniki, software na dawa, kampuni zaidi ya 6,000 zimejenga matawi yake katika eneo hilo vikiwemo vituo vya utafiti vilivyoanzishwa na kampuni kubwa za kimataifa ambazo ni pamoja na FUJITSU, INTEL NA Infineon. Pato la eneo hilo la Xian lilizidi Yuan bilioni 20 katika mwaka 2004.

Kampuni ya mawasiliano ya kielektroniki ya Datang ni moja ya kampuni kubwa za huduma na uzalishaji wa zana za mawasiliano ya habari, kampuni hiyo ilianzishwa kabla ya miaka 7 iliyopita na kituo muhumu chake cha utafiti kiko katika eneo la uswatishi la Xian. Mkurugenzi wa idara ya usimamizi na mpango wa kampuni ya Datang Bw. Wu Jie alisema,

"Xian ina vyuo vikuu vingi pamoja na rasilimali nyingi za nguvukazi, na kuweko kwa kutuo cha utafiti wa mfumo mkuu wa mawasiliano ya habari cha wizara ya mawasiliano ya habari ya China, hali ambayo inachangia maendeleo ya sehemu hiyo."

Habari zinasema kuwa katika miaka karibu mitano iliyopita uchumi wa mkoa wa Shanxi ulidumisha wastani wa ongezeko la zaidi ya 8%. Imekadiriwa pato la mkoa huo lita fikia Yuan bilioni 440 ifikapo mwaka 2010 na wastani wa pato la kila mtu utafikia Yuan elfu 11 kwa mwaka.

Idhaa ya kiswahili 2005-04-19