Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2005-04-20 20:49:27    
Upikaji wa bilinganya kwa sosi tamu

cri

Mahitaji

Biliganya gramu 500, mafuta gramu 500, sosi tamu gramu 25, sukari gramu 10, mchuzi wa soya gramu 19, chumvi gramu 1, M.S.G gramu 1, maji ya wanga gramu 25, tangawizi, vitunguu maji na vitunguu saumu gramu 50

Njia

1. Ondoa ganda la bilinganya, na ulikate kuwa vipande vyenye sm 2.

2. Tia mafuta ndani ya sufuria na chemsha mpaka yawe na joto la nyuzi 50, tia vipande vya bilinganya mpaka iwe rangi ya dhahabu ipakue.

3. Weka mafuta kidogo kwenye sufuria, pasha moto tena, tia tangawizi, vitunguu maji na vitunguu saumu, koroga na tia sosi tamu, korogakoroga na mimina maji kidogo, halafu tia vipande vya bilinganya, sukari, chumvi, M.S.G na mchuzi wa soya, baada ya kuchemka punguza moto kidogo, mimina maji ya wanga, vipakue. Mpaka hapo kitoweo hiki kitakuwa tayari kuliwa.