Mkutano wa pili wa Asia na Afrika utafunguliwa tarehe 22 mwezi Aprili, huko Jakarta, mji mkuu wa Indonesia. Huu ni mkutano mkubwa mwingine utakaoitishwa na nchi nyingi zinazoendelea barani Asia na Afrika baada ya mkutano wa kwanza wa Asia na Afrika yaani mkutano wa Bandung uliofanyika mwaka 1955. Wakati huo, shughuli za kuadhimisha miaka 50 ya mkutano wa Bandung zitaanzishwa tarehe 24 mwezi huu mjini Bandung. India ikiwa nchi moja iliyoanzisha mkutano wa Bandung namna itaeleza vipi maana ya kihistoria na kisasa ya mkutano huo? Waandishi wa habari wa Radio China Kimataifa walimhoji mwanadiplomasia mzoefu wa India Bw. V. K. Nambiar.
Bw. V. K. Nambiar alikuwa balozi wa India nchini China, kamishina mwenye cheo cha juu wa India nchini Pakistan na mjumbe wa kudumu wa India katika Umoja wa Mataifa. Sasa yeye ni naibu mshauri wa usalama wa taifa wa India. Bw. Nambiar anaona kuwa mkutano wa Bandung ulifanyika mara tu baada ya nchi kadhaa za Asia na Afrika kuuondoa utawala wa kikoloni na kupata uhuru, huu ni mkutano muhimu wa kihistoria, akisema:
"Msingi wa kanuni kumi zilizopitishwa kwenye mkutano wa Bandung ni kauni tano za kuishi pamoja kwa amani ambazo ziliitikiwa na nchi zinazoendelea za Asia na Afrika kwa utaratibu wa kimataifa baada ya vita vya pili vya dunia na vita baridi. Kanuni tano za kuishi pamoja kwa amani ni wazo jipya na jaribio jipya la kubadilisha hali ya kupambana kwa makundi ya nchi kubwa na zilitumai kuwa nchi mbalimbali zitaweza kuishi kwa amani. Huu ni mchango mkubwa uliotolewa na viongozi wa nchi za Asia na Afrika kwa uhusiano wa kimataifa".
India ni moja ya nchi zilizopendekeza kanuni tano za kuishi kwa amani. Bw. Nambiar anaona kuwa kanuni hizo pia ni msingi wa sera za kidiplomasia za India. Aliainisha kuwa India ikiwa nchi moja ya nchi zilizoanzisha harakati zisizofungamana na upande wowote, ilitaka kutojihusisha katika vita baridi na kutojiunga na mapambano kati ya nchi mbili kubwa zenye nguvu za kupindukia, akisema:
"Kufanya uamuzi kwa uhuru kwa mambo ya kimataifa, kuheshimu utaratibu wa kisiasa wa nchi nyingine na kuziruhusu nchi mbalimbali zisimamie mambo ya nchi zao ni kutoingilia kati mambo ya ndani ya nchi nyingine. Maoni hayo yako katika kanuni tano za kuishi kwa amani".
Katika miaka 50 iliyopita, mabadiliko makubwa yametokea duniani, je kanuni kumi za uhusiano wa kimataifa zilizoafikiwa kwenye mkutano wa Bandung zina maana kwa sasa? Bw. Nambiar anaona kuwa matumaini ya kanuni za kuishi kwa amani hazikubadilika wala hazipitiwa na wakati. Alisisitiza kuwa ni lazima kuheshimu tofauti kati ya nchi na nchi na masuala yote yasingepimwa kwa kigezo kimoja. Katika baadhi ya sehemu barani Asia, kushikilia mawazo ya asili ya mamlaka na kuheshimu mamlaka bado ni mwelekeo mkuu. Kwa hiyo ni lazima kuheshimu tofauti hizo na kuziruhusu nchi hizo ziwe na maeneo ya maendeleo na kukabiliana na changamoto. Mkutano wa pili wa Asia na Afrika utajadili hasa suala la kupambana na changamoto hizo.
Idhaa ya kiswahili 2005-04-21
|