Mkutano wa pili wa viongozi wakuu wa nchi za Asia na Afrika utafanyika tarehe 22 hadi 23 huko Djakarta, mji mkuu wa Indonesia. Rais Hu Jintao wa Chinapamoja na viongozi au wajumbe wa serikali za nchi 87 za Asia na Afrika watahudhuria mkutano huo. Mkutano huo umeandaliwa na Indonesia na kauli mbiu ya mkutano huo ni "kufufua 'moyo wa Bandung' na kuanzisha uhusiano wa aina mpya wa kiwenzi na kimkakati".
Huu ni mkutano mkubwa mwingine wa nchi zinazoendelea za Asia na Afrika baada ya mkutano wa Bandung uliofanyika mwaka 1955. Kutokana na mpango, rais Susilowa Indonesia , raisMbeki wa Afrika Kusini , rais Hu Jintao wa China na katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa Bw. Kofi Annan watahutubia mkutano huo. Katika siku za mkutano viongozi hao watasikiliza ripoti kuhusu mkutano wa mawaziri uliofanyika tarehe 20 na ripoti kuhusu mkutano wa biashara uliofanyika tarehe 21, na kujadili na kuanzisha uhusiano wa aina mpya wa kiwenzi na kimkakati na kusaini "Taarifa ya Uhusiano wa Aina Mpya wa Kiwenzi na Kimkakati wa Asia na Afrika".
Mabadiliko makubwa yametokea katika muda wa miaka 50 iliyopita, ukoloni sio tena adui wa pamoja wa nchi za Asia na Afrika. Kwa mara nyingine tena viongozi wa nchi hizo wanaokutana katika mkutano huo wanatumai kuimarisha ushirikiano katika nyanja za siasa, uchumi, utamaduni na nyanja nyingine, na kuufanya 'moya wa Bandung' uliokuwa wa miaka 50 iliyopita, utekelezwe kwa vitendo ili kutimiza matumaini ya amani, ustawi na maendeleo.
Katika miaka ya karibuni nchi za Asia na Afrika zinashirikiana vizuri katika mambo ya siasa na matokeo mazuri yamepatikana katika ushirikiano wa kiuchumi. Ili kuanzisha uhusiano wa aina mpya wa kiwenzi na kimkakati, "mkutano wa mawaziri wa nchi za Asia na Afrika" ulifanyika mwezi Julai, mwaka 2003 ambao wajumbe kutoka nchi 36 za Asia na Afrika na mashirika 22 ya kimataifa na za kikanda walihudhuria mkutano huo na kwa kauli moja walikubaliana kuanzisha uhusiano wa aina mpya wa kiwenzi na kimkakati wa nchi za Asia na Afrika. Mwezi Machi na Agosti kikao cha kwanza na cha pili cha kikazi cha mkutano huo vilifanyika mjini Durban, Afrika Kusini. Na katika kikao cha tatu kanuni kadhaa ziliwekwa zikiwa ni pamoja na kushikilia 'moyo wa Bandung', kutambua aina tofauti za mifumo ya jamii na uchumi na tofauti ya vipindi vya maendeleo ya kiuchumi, kusisitiza kufanya mazungumzo na majadiliano kwa haki na usawa, kuheshimiana na kunufaishana, na kufanya ushirikiano kwa mujibu wa hali ilivyo ya taifa. Kikao hicho kimsingi kimefikia ushirikiano wa nchi za Asia na Afrika katika kipindi kipya cha historia na kimefanya tumaini kubwa la kupata mustakbali mzuri wa nchi za Asia na Afrika kwa mshikamano lionekane.
Sambamba na hayo, mabara mawili ya Asia na Afrika pia yanakabiliwa na changamoto kubwa. Kwamba licha ya kulinda uhuru na mamlaka ya taifa, nchi za Asia na Afrika pia zinakabiliwa na mashinikizo kutoka pande mbalimbali yakiwa ni pamoja na kuanzisha mfumo mpya wa kiuchumi ulio wa haki na halali duniani, kupigania usawa wa kijamii na biashara ya haki, kuondoa umaskini na shinikizo la madeni na kupunguza athari mbaya kutokana utandawazi na kuendana na teknolojia ya upashanaji habari inayoendelea kwa kasi. Hivi sasa viongozi wa nchi za Asia na Afrika wote wametambua haja kubwa ya kuimarisha haraka ushirikiano katika kipindi hiki cha kihistoria na wanatumai kuwa ushirikiano huo utakuwa wa vitendo kupitia mkutano huo wa viongozi wakuu wa nchi za Asia na Afrika mwaka 2005.
Wachambuzi wanaona kuwa kutokana na juhudi za pamoja mkutano wa viongozi wa nchi za Asia na Afrika hakika utafanikiwa, na uhusiano wa aina mpya wa kiwenzi na kimkakati utafanya ushirikiano wa nchi hizo uingie kwenye kipindi kipya cha historia.
Idhaa ya kiswahili 2005-04-21
|