|
Mkutano wa wakuu wa Asia na Afrika wa mwaka 2005 umefunguliwa tarehe 22 huko Jakarta, mji mkuu wa Indonesia. Viongozi wa nchi au wawakilishi wa serikali wa nchi 88 za Asia na Afrika akiwemo rais Hu Jintao wa China pamoja na wachunguzi wa mabara mengine wamehudhuria mkutano huo.
Mabara makubwa mawili ya Asia na Afrika, eneo lao linachukua nusu ya lile la dunia nzima, na idadi ya watu ya mabara hayo mawili inachukua robo tatu ya ile ya dunia. Nusu karne iliyopita, wajumbe 304 kutoka nchi na sehemu 29 za Asia na Afrika walifanya mkutano wa kihistoria huko Bandung, Indonesia. Tangu hapo, nchi zinazoendelea za Asia na Afrika zimekuwa nguvu mpya ya kujiamulia, zikapanda kwenye jukwaa la kimataifa. Baada ya karne mpya kuingia, mabara yanakabiliwa na fursa mpya na changamoto kubwa za mshikamano, ushirikiano na maendeleo. Katika hali hiyo, viongozi wa nchi za Asia na Afrika wamekutana tena nchini Indonesia kujadili mkakati mkubwa kuhusu mshikamano na ushirikiano katika hali mpya.
Rais Hu Jintao wa China ametoa hotuba kwenye mkutano akisema:

Mkutano wa Asia na Afrika uliofanyika miaka 50 iliyopita ulikuwa mnara mkubwa katika harakati za ukombozi wa kitaifa wa Asia na Afrika. "Moyo wa Bandung" uliotetewa kwenye mkutano huo umekuwa nguvu kubwa ya kuhamasisha nchi nyingi zinazoendelea zipambane bila kulegalega ili kutimiza ustawi wa taifa na kusukuma mbele maendeleo ya binadamu, na ulihimiza amani na maendeleo ya dunia.
Ili kujenga uhusiano wa aina mpya wa kimkakati kati ya Asia na Afrika ulio wa muda mrefu, wenye mambo mengi na unaosonga mbele kwa kwenda na wakati, rais Hu Jintao ametoa mapendekezo akisema nchi za Asia na Afrika zinapaswa kuwa wenzi wa kuheshimiana na kuunga mkono katika mambo ya siasa, kusaidiana na kunufaishana katika mambo ya kiuchumi, na kuwa na usawa na uaminifu, kufanya mazungumzo na ushirikiano katika mambo ya usalama.
Rais Hu Jintao amesisitiza kwa makini akisema:
China itashikilia kithabiti njia ya kujiendeleza kwa amani. Nia ya sera ya kidiplomasia ya China ni kulinda amani ya dunia, kusukuma mbele maendeleo ya pamoja, China ni moja kati ya nchi zinazoendelea, kuimarisha mshikamano na ushirikiano na nchi zinazoendelea ni msingi wa mambo ya kidiplomasia ya China, na itashirikiana na kusaidiana daima na nchi nyingi zinazoendelea katika kulinda amani ya dunia na kusukuma mbele maendeleo ya pamoja.
Rais Susilo wa Indonesia, nchi mwenyeji wa mkutano huo alipotoa hotuba alisema:
Uhusiano wa wenzi wa kimkakati kati ya Asia na Afrika unapaswa kuonekana katika nyanja tatu za mshikamano wa kisiasa, ushirikiano wa kiuchumi na mawasiliano ya utamaduni wa jamii, ambao unapaswa kuanzishwa kati ya serikali na serikali na jumuiya za kikanda na kiraia.
Rais Mbeki wa Afrika ya kusini ambayo pia ni nchi mwendeshaji wa mkutano huo akitoa risala alisema:
Asia na Afrika zikishikamana na kuchukua hatua, zitakuwa na nguvu kwa kuvumbua utaratibu mpya wa dunia.
Katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa Kofi Annan alisema:
"Moyo wa Bandung" umewekwa kwenye msingi wa kanuni za katiba ya Umoja wa Mataifa na kanuni za kuishi pamoja kwa amani, ambao umeziwezesha nchi zinazoendelea kuwa na sauti yao kwenye jukwaa la kimataifa na kuubadilisha kabisa Umoja wa mataifa.
Idhaa ya Kiswahili 2005-04-22
|