Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2005-04-22 19:27:49    
Shirika la Kilimo la China kushughukia mashamba nchini Zambia

cri
    Shirika la Kilimo la China ni shirika kubwa linalomilikiwa na taifa la China. Mwaka 1990, shirika hilo lilinunua shamba lake la kwanza nchini Zambia, lililoko kilomita 20 magharibi mwa Lusaka mji muku wa nchi hiyo. Shamba hilo lenye eneo la hekta 667 sasa linajulikana kama Shamba la Urafiki kati ya China na Zambia. Kwa Shirika la Kilimo la China, shamba hilo ni hatua yake ya kwanza katika kuanzisha shughuli nchini Zambia, na uzoefu uliopatikana katika shamba hilo limenufaisha sana shughuli za baadaye.

    Mwaka 1994, Shirika la Kilimo la China lilinunua shamba jingine moja la mzungu kwa dola laki mbili na elfu ishirini za kimarekani. Shamba hilo lenye eneo la hekata 3,500 liko milimani kilomita 50 kaskazini mashariki mwa mji wa Lusaka. Hilo ni shamba la pili la shirika hilo nchini Zambia. Shirika la Kilimo la China lilikopa dola za kimarekani laki 6 kutoka wizara ya uchumi na biashara ya China. Kiasi cha pesa hizo kilitumiwa kuchimba visima vya maji, kuweka nyaya za umeme, kujenga nyumba za kisasa kwa mifugo, na kuagiza mashine mengi ya kilimo. Mnamo mwaka 1997, Shirika la Kilimo la China lililipa madeni ya awali, na kupanua shughuli zake la shamba hilo kwa kukopa mkopo mwingine wa dola za kimarekani milioni moja na laki tano. Baada ya maendeleo ya miaka kadhaa, mpaka sasa shamba hilo lina mali zenye thamani ya dola za kimarekani milioni tatu na laki tano. Shamba hilo hasa linashughulikia kufuga mifugo. Sasa shamba hilo lenye wafanyakazi kadhaa wachina na zaidi ya mia moja wenyeji linafuga kuku laki moja na elfu kumi wanaotaga mayai, kuku laki tatu ya nyama, ng'ombe 1,000 wa nyama, ng'ombe zaidi ya 200 wa kutolea maziwa. Mwaka 2003, shamba hilo lilitoa nguruwe 2,000, ambapo mwaka 2004 wameongezeka kuwa 6,000. Sasa shamba hilo limechukua nusu ya soko la mayai huko Lusaka. Mbali na hayo, limepanda mahindi ya mamia ya hekta.

    Mwaka 1998, Shirika la Kilimo la China lilianzisha shamba lake la tatu nchini Zambia, kwa kutenga dola za kimarekani laki moja na elfu arobaini. Shamba hilo lenye eneo la hekta 2600 linajulikana kama Shamba la Urafiki la Shirika la Kilimo la China nchini Zambia. Shughuli zake hasa ni kufuga ng'ombe wa maziwa, ng'ombe na kuku wanaotoa nyama.

    Naibu meneja mkuu wa Shirika la Kilimo la China Bw. Han Xiangshan alisema kuwa, Bara la Afrika ni sehemu bora zaidi ulimwenguni kwa wachina kufanya kazi za kilimo. Bara hilo lina ardhi kubwa na maliasili nyingi, ambazo zina hitaji sana nafaka, China ina teknolojia nzuri ya kilimo na wataalam wengi wanaohusika, ambao wanaweka kutoa mchango wao.

    Bw Han alieleza kuwa, Zambia ina ardhi zenye rutuba na hali nzuri ya hewa. Eneo la ardhi la kila mtu kwa wastani nchini humo ni mara 40 kuliko nchini China. Lakini kutokana na sababu mbalimbali, kazi ya kilimo haikuendelea vizuri kwenye nchi hiyo, hata wakati wengine wa nchi hiyo wanakabiliwa na njaa. Bw. Han alisema kuwa, ingawa gharama za kupatia mibegu, mbolea, madawa ya kuwaua wadudu, mafuta na vitu vinginevyo ni za juu kidogo kuliko nchini China, lakini mashamba nchini Zambia hupata mapato zaidi kutokana na bei za juu za mazao.

    Kuhusu mafanikio ya Shirika la Kilimo la China, Bw. Han alisema kuwa, kanuni ya shirika lake la kuanzisha na kuendeleza shughuli nchini Zambia ni kuwa kuanzisha kazi na kilimo ya kiasili, kuendeleza kazi na kilimo ya kisasa na kisayansi, kuweka utengenezaji upya wa mazao kuwa shughuli muhimu.

    Bw. Han alisema kuwa, nchi za Afrika hivi sasa zinaendelea kwa kasi. Alieleza kuwa, alipokwenda nchini Zambia mara yake ya kwanza mnamo mwaka 1994, nchini humo haikuwepo supermarket, lakini sasa zimeanzishwa vizuri. Bw. Han alieleza kuwa, Bara la Afrika lina maliasili, ambapo China ina teknolojia na mali. Nchi za Afrika zinawakaribisha sana wachina kuwekeza vitega uchumi kwenye kazi ya kilimo nchini kwao. Pande hizi mbili zinaweza kushirikiana kuanzisha mashamba ya kupanda ni chakula, na kufuga, ili kuendeleza maendeleo ya kilimo ya pande hizi mbili.

Idhaa ya Kiswahili 2005-04-22