Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2005-04-25 15:21:03    
Ushirikiano wa Afia na Afrika waingia zama mpya

cri

Mkutano wa Bandung wenye maana ya kihistoria umepita miaka 50, tarehe 24 viongozi wakuu wa nchi za Asia na Afrika walikutana mjini Djakarta kushiriki sherehe ya kuadhimisha miaka 50 ya mkutano huo baada ya mkutano wa viongozi hao kumalizika kwa mafanikio. Wenyeviti wa mkutano wa viongozi wakuu wa nchi za Asia na Afrika, rais Susilo Yudhoyono wa Indonesia na rais Thabo Mbeki wa Afrika Kusini tarehe 24 walisaini "taarifa ya uhusiano wa aina mpya wa kiwenzi na kimkakati" na kuifanya taarifa hiyo iwe rasmi mara moja. Hii inaonesha kuwa ushirikiano wa Asia na Afrika umeingia katika zama mpya, na ushirkiano wa mabara hayo mawili umehamia kwenye siasa, uchumi na utamaduni badala ya ushirikiano wa siasa pekee, kama hapo awali. Vyombo vya habari vinasema kuwa mkutano huo wa viongozi wakuu wa nchi za Asia na Afrika umejenga madaraja matatu kati ya mabara hayo mawili. Rais Susilo Yodhoyono wa Indonesia tarehe 23 kwa ufupi alitafsiri mkutano huo, kwamba "taarifa ya uhusiano wa aina mpya wa kiwenzi na kimkakati" ni waraka muhimu wa mkutano huo; pili mkuktano huo umetia saini "taarifa ya pamoja ya viongozi wa nchi za Asia na Afrika kuhusu kupunguza hasara za maafa", umeonesha nia ya pamoja ya nchi hizo katika kupambana na maafa, kuimarisha upashanaji habari na kujenga mfumo wa kutoa tahadhari. Tatu, mpango wa utekelezaji wa uhusiano wa aina mpya wa kiwenzi na kimkakati uliopitishwa hapo mapema na mkutano wa mawaziri wa nchi za Asia na Afrika umeweka hatua mfululizo za ushirkiano. Rais wa Indonesia alisema kuwa kupitia uhusiano huo mpya, nchi za Asia na Afrika zitawaleta utajiri mkubwa wa kiuchumi na kiutamaduni kwa vizazi vya baadaye. Alisema, mkutano huo utakuwa "kumbukumbu ya kihistoria".

Kwenye mkutano wa viongozi wakuu wa nchi za Asia na Afrika, maneno yaliyotumika mara nyingi ni amani, ushirkiano na utetezi wa pande nyingi. Viongozi walipohutubia mkutano huo walisema, kuukumbuka moyo wa Bandung hakumaanishi kukumbuka historia bali ni kutaka amani, uadilifu, ushirikiano na utetezi wa pende nyingi duniani, ili nchi zilizopata uhuru za Asia na Afrika ziweze kupata maendeleo ya uchimi na jamii, na zifaidike na utandawazi.

Katika miaka kadhaa ya karibuni, utetezi wa upande mmoja tu na siasa ya ubabe inatamba duniani na kusababisha watu wa nchi zinazoendelea kuwa na wasiwasi. Kwa hiyo viongozi wa nchi za Asia na Afrika wanaona kuwa nchi hizo lazima ziungane pamoja ili kujipatia nguvu. "Taarifa ya uhusiano wa aina mpya wa kiwenzi na kimkakati" inaona kuwa moyo wa Bandung ulioelezwa kwa ufupi wa "Umoja, Usawa na Ushirikiano" laizima uendelee na uwe moyo wa kuendeleza uhusiano wa nchi za Asia na Afrika na uwe msingi wa kutatua matatizo yote duniani.

Rais Thabo Mbeki wa Afrika Kusini alisema, uhusiano wa aina mpya wa kiwenzi na kimkakati haulengi mtu yeyote mwingine, bali ushirikiano huo wa pande nyingi unasaidia maslahi ya Asia na Afrika.

Kama mkutano wa Bandung wa miaka 50 iliyopita ulikuwa ni ngoma ya kuitaka nchi za Asia na Afrika kuungana pamoja, basi mkutano uliomalizika sasa hivi ni mbiu kwa nchi za Asia na Afrika kupambana na umaskini na kupigania uhuru wa kiuchumi.

Katika zama hizi, moyo wa Bandung umekuwa chimbuko la kusukuma umoja na ushirikiano wa nchi za Asia na Afrika, kwa kurithi na kuenzi moyo wa Bandung viongozi wa Asia na Afrika wataikabili changamoto mpya na kufungua ukurasa mpya wa kihistoria katika ushirikiano.

Idhaa ya kiswahili 2005-04-25