Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2005-04-25 16:39:52    
Upigaji kura katika uchaguzi wa rais wa Togo wamalizika

cri
    Upigaji kura katika uchaguzi wa rais wa Togo ulimalizika tarehe 24, Aprili. Hivi sasa kazi ya kuhesabu kura inafanyika, na matokeo yanatazamiwa kujulikana ndani ya siku mbili zijazo.

    Ofisa wa Tume ya uchaguzi ya Togo alieleza kuwa, wapiga kura zaidi ya milioni 2 walishiriki kwenye upigaji kura uliofanyika siku hiyo. Vituo mbalimbali vya upigaji kura ulifanya shughuli kwa utaratibu mzuri, na hakukutokea migogoro kati ya wapiga kura kutoka chama tawala na Muungnao wa vyama vya upinzani. Umoja wa Afrika na ECOWAS na wasimamizi zaidi ya 100 walisimamia uchaguzi huo.

    Wagombea watatu wameshiriki kwenye uchaguzi huo kutombea nafasi ya urais, nao ni pamoja na Faure Gnassingbe ambaye ni mtoto wa rais wa zamani wa nchi hiyo Gnassingbe Eyadema kutoka chama tawala cha nchi hiyo "Muungano wa umma wa Togo"; Bw. Emmanuel Bob Akitani ambaye ni naibu mwenyekiti wa kwanza wa chama muhimu cha upinzani cha Togo "Muungano wa nguvu ya mageuzi"; na Bw. Harry Olympio anayetoka chama kingine cha upinzani. Wachambuzi wanaona kuwa, ushindani mkali utafanyika kati ya Bw. Faure na Bw. Akitani.

    Rais wa zamani wa Togo Bw. Gnassingbe Eyadema alifariki dunia kwa ghafla tarehe 5, Februali. Bunge la umma la Togo lilifanya marekebisho ya katiba chini ya uungaji mkono wa jeshi, na kumteua Bw. Faure kuwa spika, na alishika madaraka ya rais baadaye. Lakini kitendo hicho kililaumiwa na jumuiya ya kimataifa ukiwemo Umoja wa Afrika na vyama vya upinzani vya nchi hiyo. Umoja wa Afrika na ECOWAS ziliiwekea Togo vikwazo vya pande zote, ili kuihimiza irejeshe utaratibu wa katiba. Kutokana na shinikizo kubwa kutoka nchini na nchi za nje, Bw. Faure alijiondoa kutoka kwenye wadhifa wa urais, na kutangaza kufanya uchaguzi wa urais mwezi Aprili, mwaka huu. Bw. Faure alipokea uteuzi wa chama tawala akawa mwenyekiti wa chama hicho, na kushiriki kwenye uchaguzi mkuu akiwa mgombea wa urais.

    Kujiondoa kutoka wadhifa wa urais kwa Bw. Faure kulikaribishwa na jumuiya ya kimataifa. Umoja wa Afrika na ECOWAS ziliamua kuondoa vikwazo dhidi ya Togo. Lakini baada ya tarehe ya uchaguzi mkuu kuwekwa mwanzoni mwa mwezi Machi, Muungano wa vyama vya upinzani ulitaka kuahirisha uchaguzi huo uahirishwe, kwa kisingizio kuwa Serikali ya Togo haina uwezo wa kuendesha uchaguzi wa haki na wazi ndani ya muda mfupi. Aidha, muungano huo ulilaani kuwa serikali ya Togo ilidhibiti kazi ya uandikishaji wa wapiga kura na kufanya udanganyifu, na ulitaka Umoja wa Mataifa na Umoja wa Afrika kupeleka walinzi wa amani nchini Togo, ili kusaidia kusimamia uchaguzi huo. Wakati huo huo, waunga mkono wa chama tawala cha Togo na vyama vya upinzani walifanya mikutano mbalimbali ya hadhara, na kuchochea mgogoro nchini humo.

    Wachambuzi wanaona kuwa, ingawa mgombea kutoka chama tawala Bw. Faure alilaumiwa kutokana na kushika madaraka baada ya kufariki dunia kwa baba yake, lakini kuna uwezekano mkubwa wa yeye kushinda katika uchaguzi mkuu.

    Bw. Faure mwenye umri wa miaka 39 alisoma nchini Marekani na Ufaransa. Ingawa alishughulikia mambo ya kisiasa kwa muda mfupi tu, lakini anafahamu mambo ya kiuchumi, na alikuwa mshauri wa uchumi wa baba yake Eyadema kwa muda mrefu, na kudhibiti shughuli za madini ambazo ni nguzo ya chumi wa Togo. Bw. Faure siku zote anasisitiza kufanya mageuzi ya kisiasa na kutimiza maafikiano ya kitaifa. Pia Bw. Faure alieleza mara kwa mara, endapo atachaguliwa kuwa rais, ataunda serikali ya umoja wa kitaifa, na kuwashirikisha wanachama wa vyama vya upinzani. Msimamo huo wa Bw. Faure unakaribishwa na wananchi. Aidha, chama tawala cha Togo pia kinapata uungaji mkono mkubwa zaidi katika sehemu ya kaskazini na ya kati nchini humo.

    Mgombea kutoka Muungano wa vyama vya upinzani Bw. Akitani ana umri wa miaka 74, umri wake mkubwa unakosa nguvu ya ushindani. Aidha, waungaji mkono wa muungano huo wengi wako katika sehemu ya Kusini yenye umaskini nchini Togo.

    Lakini, hayati rais Eyadema alishika madaraka ya urais kwa miaka 38, hali hiyo iliwachosha watu wengi. Hivyo, bado kuna uwezekano kuwa, chama tawala wa nchi hiyo na Muungano wa vyama vya upinzani vitalingana katika uchaguzi mkuu, hata kuna uwezekano kwa vyama vya upinzani kushinda katika uchaguzi huo.

Idhaa ya Kiswahili 2005-04-25