Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2005-04-25 17:34:10    
Kukumbuka historia na kutupia macho siku za mbele

cri

Shughuli za kuadhimisha miaka 50 ya mkutano wa Bandung zilifanyika tarehe 24 huko Bandung, Indonesia. Rais Hu Jintao wa China na viongozi au wawakilishi wa nchi mbalimbali waliohudhuria mkutano wa wakuu wa Asia na Afrika walishiriki kwenye shughuli zilizofanyika huko.

Bandung ni mji mkuu wa mkoa wa Java ya magharibi, ambao ni mji mkubwa wa tatu wa Indonesia uliosifiwa kuwa ni "Paris Java". Jumba la uhuru liko kwenye barabara ya Asia na Afrika ambapo mkutano wa Bandung uliwahi kufanyika kwenye jumba hilo miaka 50 iliyopita.

Saa 3 asubuhi tarehe 24, viongozi au wawakilishi wa serikali za nchi zaidi ya 80 za Asia na Afrika pamoja na jumuiya za kimataifa walitembea kutoka hoteli Savoy Homann ambayo ni hoteli ya kale kabisa huko Bandung, wakifuata barabara ya Asia na Afrika na kukanyaga njia waliyowahi kupita wajumbe wa nchi za Asia na Afrika waliohudhuria mkutano wa Bandung miaka 50 iliyopita, na kuingia kwenye Jumba la uhuru.

Shughuli za kuadhimisha miaka 50 ya mkutano wa Bandung zilianzishwa kwa kuambatana na sauti ya kwaya ya "Hujambo, Bandung!". Rais Susilo Yudhoyono wa Indonesia, nchi mwandaaji wa shughuli hizo alitoa risala akisema:

Miaka 50 iliyopita, viongozi wa Asia na Afrika walifanya mkutano wa kwanza wa wakuu wa Asia na Afrika huko Bandung, mkutano huo umeeleza nia ya wananchi wa Asia na Afrika ya kutaka uhuru, amani na usawa, huu ni kiini cha "Moyo wa Bandung". Leo nchi za Asia na Afrika zinakutana tena Bandung kukumbuka "Moyo wa Bandung", zikikumbusha moyo huo na kutia nguvu za uhai kwa moyo huo. Na kwa kufuata moyo huo, nchi za Asia na Afrika zimeanzisha uhusiano mpya wa kimkakati.

Wajumbe wengine kutoka nchi za Asia na Afrika na harakati za kutofungamana na upande wowote pia walitoa hotuba wakisema kuwa, "Moyo wa Bandung" uliothibitishwa miaka 50 iliyopita bado una nguvu kubwa ya uhai mpaka sasa. Nchi za Asia na Afrika zikiimarisha mshikamano na ushirikiano hakika zitatimiza utulivu, maendeleo na usitawi wa kikanda.

Mzee Paul Tedja Surya aliyewahi kushiriki kwenye mkutano wa Bandung miaka 50 iliyopita akiwa mwandishi wa habari siku hiyo pia alikwenda huko, alipohojiwa na waandishi wa habari alisema:

Mkutano uliofanyika miaka 50 iliyopita ulihudhuriwa na viongozi wa nchi 29 tu, lakini mkutano wa mwaka huu umewashirikisha viongozi au wawakilishi wa nchi zaidi ya 80. Wakati wa miaka 50 iliyopita, watu wa familia nyingi kabisa za Bandung walikuwa bado hawajaanza kutumia umeme, waliweza tu kwenda mtaani kufahamishwa hali ya mkutano, lakini hivi sasa watu wa huko wanaweza kutazama televesheni kuona jinsi mkutano unavyoendelea.

Dk Teuku Rezasyah kutoka chuo kikuu cha Padjadjaran alisema:

Hivi leo tunatakiwa kufanya ushirikiano barabara zaidi, naamini kuwa, baada ya mkutano wa wakuu wa Asia na Afrika wa mwaka huu, kama tukiimarisha ushirikiano, tutaunda umoja wenye nguvu kubwa ili kukabiliana na changamoto za pamoja.

Mfanyakazi aliyeshiriki kwenye shughuli Bwana Srijanto Agusti alisema:

Mkutano wa wakuu wa Asia na Afrika wa mwaka 2005 na shughuli za kuadhimisha miaka 50 ya mkutano wa Bandung zimefanyika nchini Indonesia, nikiwa raia wa Indonesia naona fahari kubwa. Kufanikiwa kwa mkutano wa wakuu wa Asia na Afrika kumeongeza ushirikiano kati ya nchi mbalimbali za Asia na Afrika katika sekta za siasa, uchumi na jeshi.

Idhaa ya Kiswahili 2005-04-25