Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2005-04-25 21:33:09    
Mkoa wa Henna waongeza nguvu katika kusimamia virusi vya ugonjwa wa Ukimwi

cri

Mkoa wa Henan hivi karibuni ulitoa mswada wa utekelezaji wa kusimamia virusi vya ugonjwa wa ukimwi ili kuimarisha usimamizi na upimaji wa ugonjwa wa ukimwi.

Imefahamika kuwa, kutokana na muswada huo, mkoa huo utafanya upimaji wa virusi vya ukimwi kwa mfululizo na kwa kiwango kikubwa mkoani kote. Madaktari, wauguzi na wapimaji wa hospitali, idara za kukinga na kutibu magonjwa na idara za kukusanya damu wote wanawajibika kutoa ripoti ya hali ya maambukizi ya ukimwi. Kuripoti kwa wakati kwa kupitia mtandao matukio yoyote ya ukimwi yaliyogunduliwa na kufanya uchunguzi kuhusu watu walioambukizwa.

Mkoa huo pia utaanzisha mfumo wa kutoa tahadhari ya ugonjwa wa ukimwi, na kushughulikia matukio yote kwa wakati.