Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2005-04-26 15:43:28    
Mkutano wa 11 wa Umoja wa Mataifa dhidi ya makosa ya jinai wafungwa

cri

Mkuktano wa 11 wa siku nane wa Umoja wa Mataifa dhidi ya makosa ya jinai ulifungwa tarehe 25 mjini Bangkok, Thailand. Mkutano huo ulipitisha Taarifa ya Bangkok, ambao umeonesha nia thabiti ya kuungana pamoja kati ya nchi zote wanachama wa Umoja huo katika ushirikiano wa kupambana na makosa ya jinai, mkutano huo umeweka mwongozo wa mapambano hayo.

"Taarifa" inazitaka nchi zote zishirikiane katika mapambano dhidi ya biashara ya watu, utekaji nyara na biashara ya dawa za kulevya.

Mkutano huo ukiwa na kauli mbiu ya "Kuanzisha muungano wa kisheria na mapambano ya pamoja dhidi ya makosa ya jinai" ulijadili kwa kina namna ya kupambana na uhalifu wa biashara ya watu, utekaji nyara na biashara ya dawa za kulevya, na umeanzisha mfumo halisi wa kufanya mapambano hayo.

Washiriki wa mkutano huo wanaona kuwa uhalifu uliopangwa wa vikundi unatokea kutonana hali ya utatanishi ambayo inahusika na siasa, uchumi, utamaduni na pande mbalimbali za jamii za taifa, kwa hiyo adhabu peke yake haiwezi kukomesha matatizo hayo kikamilifu, jumuyia ya kimataifa ni lazima zifanye utafiti wa kina.

Wajumbe walioshiriki kwenye mkutano huo wanaona kuwa kutokana na jinsi utandawazi unavyoendelea, uhalifu umekuwa wa kimataifa, uhalifu uliopangwa wa kikundi na uhalifu mwingine mkatili umekukwa tishio kubwa kwa amani ya dunia na maendeleo na utulivu wa jamii. Kwa hiyo kutilia mkazo mapambano dhidi ya uhalifu, na hasa uhalifu uliopangwa wa vikundi na ufisadi ni lazima.

Bishara ya dawa za kulevya ni uhalifu muhimu unaopangwa wa vikundi ambao unahatarisha usalama na utulivu wa taifa. Kwa makadirio, faida zinazopatikana katika biashara za dawa za kulevya zinafikia dola za Kimarekani bilioni 300 na hata 500 kila mwaka, na katika sehemu fulani faida hizo hata zinalingana na thamani zote za bidhaa zilizozalishwa za taifa, na biashara hiyo inachangia kushamiri kwa Ukimwi.

Aidha, ufalifu wa biashara ya watu na utekaji nyara umekuwa ukiongezeka duniani, mauzo ya watu walioibwa na utekaji nyara unalenga kulimbikiza fedha kwa ajili ya uhalifu uliopangwa wa vikundi na hasa ugaidi. Mkutano huo umependekeza kuchukua hatua za hakika dhidi ya vitendo vya uhalifu huo na kuanzisha mfumo wa mapambano hayo, na hatua zichukuliwe ili kuwalinda na kuwasaidia waathirika na jamaa waliokumbwa na uhalifu huo.

Uhalifu wa ufisadi ni tishio jingine kubwa linalokabili binadamu katika karne hii ya 21, ni athari mbaya kabisa kwa uchumi wa taifa, siasa ya kidemokrasia na ujenzi wa sheria, na unasaidia uhalifu uliopangwa wa vikundi kuenea, na kudhoofisha uwezo wa serikali wa kuhudumia umma. Washiriki wa mkutano huo wanaona kuwa ili kufanikisha mapambano dhidi ya ufisadi, ni lazima uongozi wa kisiasa uimrishwe na zichukuliwe hatua za uhakika za kuzuia na kuadhibu uhalifu wa ufisadi, kadhalika umma lazima uwe macho nao.

Washiriki wa mkutano huo wanaona "Mkataba wa Mapambano dhidi ya Uhalifu wa Kuvuka Mipaka" ulioanza kutekelezwa mwezi Septemba mwaka 2003 na "Mkataba wa Umoja wa Mataifa dhidi ya Uhalifu" utakaoanza kutekelezwa ni nyaraka muhimu katika kuimarisha ushirikiano wa kimataifa, kudhibiti na kuzuia uhalifu unaopangwa wa vikundi. Kwa hiyo mkutano huo umetoa wito wa kutaka nchi zote wanachama ziharakishe kusaini na kuidhinisha mikataba husika ya Umoja wa Mataifa, ili kushirikiana kisheria katika kurudisha wahalifu nchini kwao, kufuatilia fedha haramu, kufanya upelelezi wa kimataifa katika mapambano dhidi ya uhalifu na kulinda amani ya dunia kwa pamoja.

Idhaa ya kiswahili 2005-04-26