Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2005-04-26 19:06:00    
Iraq yaahirisha tena kuunda serikali mpya

cri

Vyama vikubwa mbalimbali vya Iraq tarehe 25 bado havijaafikiana kuhusu ugawaji wa nyadhifa kwenye baraza la mawaziri, hivyo vimeahirisha tena kuunda serikali mpya iliyotazamiwa kuundwa siku hiyo.

Wachambuzi wanadhihirisha kuwa, kiongozi wa "Shirikisho la umoja wa Iraq" ambalo ni shirikisho kubwa kabisa la kisiasa kwenye bunge la mpito la Iraq Bwana Ibrahim al-Jafari tarehe 7 Aprili alipewa uteuzi wa wadhifa wa waziri mkuu, akabeba jukumu la kuunda baraza la mawaziri ndani ya mwezi mmoja, na kuwasilisha orodha ya majina ya mawaziri kwenye bunge la mpito ili ipitishwe. Kwa kuwa Shirikisho la umoja wa madhehebu ya Shiya limepata viti 140 miongoni mwa viti vyote 275 vya bunge la Iraq, si vigumu kupata kura nyingi za ndio kwenye bunge la mpito, lakini shirikisho hilo likitaka kushika hatamu za serikali na kuiendesha bila matatizo, tena kuziwezesha sera kubwa mbalimbali za serikali mpya zipitishwe kwenye bunge, linatakiwa kupata uungaji mkono wa shirikisho la Kurd ambalo ni shirikisho kubwa la pili pamoja na kundi la vyama vya madhehebu ya Suni linalowakilishi maslahi ya waislamu wa madhehebu ya Suni wanaochukua asilimia 20 ya idadi ya jumla ya watu wa Iraq. Lakini hivi sasa migongano kati ya vikundi hivyo vitatu ina utatanishi mkubwa, haviwezi kuungana kama kitu kimoja, hii ni sababu ya kuahirishwa tena na tena kutangazwa kwa orodha ya mawaziri.

Kwanza Shirikisho la Kurd bado lina wasiwasi kuhusu Jafari kushika wadhifa wa waziri mkuu. Wakurd wanataka kupata haki ya kujiendesha kwenye kiwango cha juu katika siku za usoni, lakini Jafari anatetea kufanya utawala wa kidikteta. Ili kudhibiti Shirikisho la umoja katika serikali ya siku zijazo, Shirikisho la Kurd linashikilia kuunda serikali moja inayowawakilisha wananchi wa pande zote, na lazima kukialika chama kikubwa cha tatu kwenye bunge yaani kundi la Allawi na kundi la vyama vya madhehebu ya Suni yaliyopata viti 40 kwenye bunge.

Aidha, hivi karibuni mashambulizi ya kimabavu dhidi ya waislamu wa madhehebu ya Shiya yanapanda moto na kuzidisha migongano kati ya madhehebu ya Shiya na Suni. Kiongozi wa shirikisho la umoja la madhehebu ya Shiya amesema mara kwa mara kuwa, kama wanasiasa na waumini wa madhehebu ya Suni hawataonesha nguvu zao za athari ili kupunguza mashambulizi dhidi ya majeshi ya Shiya, madhehebu ya Shiya yatachukua vitendo vya kulipiza kisasi. Hali hiyo ya wasiwasi hakika haiwezi kusaidia pande hizo mbili kuafikiana kwenye mazungumzo.

Baada ya kupata uteuzi wa wadhifa wa waziri mkuu, Bwana Jafari alianzisha mara moja mazungumzo na kundi la Allawi na kundi la vyama vya madhehebu ya Suni. Lakini kuhusu ugawaji wa nyadhifa wa mawaziri, migongano kati ya pande mbalimbali ni mikubwa, kila upande unataka kupata nyadhifa nyingi zaidi.

Zaidi ya hayo, hivi sasa migongano mbalimbali pia ipo ndani ya vikundi mbalimbali, mpaka sasa kila kundi halijaweza kuthibitisha wateuzi wa mawaziri na halijaweza kutoa orodha ya wateuzi wa baraza la mawaziri kwa Bwana Jafari, hii ni sababu kubwa moja ya kuahirishwa kwa uundaji wa serikali mpya.

Wakati serikali mpya ya Iraq inapoahirishwa kuundwa, hali ya usalama nchini Iraq inazidi kuwa mbaya, wairaq wengi wanasema kuwa hali hiyo inasababishwa na kuahirishwa kwa uundaji wa serikali mpya. Wakati huo huo, makamu wa rais wa Marekani Dick Cheney na waziri wa mambo ya nje Condoleezza Rice pia wametoa shinikizo shirikisho la umoja na shirikisho la Kurd kuyataka yaungane kwa kitu kimoja ili kukamilisha kazi ya kuunda baraza la mawaziri.

Kutokana na kukabiliwa na shinikizo kutoka nchini na nje, mashirikisho hayo mawili yameona kuwa kazi ya kukamilisha uundaji wa baraza la mawaziri imekuwa ya dharura.

Idhaa ya Kiswahili 2005-04-26