Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2005-04-27 15:47:02    
Mzizi wa yungiyungi wenye ladha ya asali uiliowekwa mchele yake

cri

Mahitaji

Mzizi wa yungiyungi, mchele gramu 150, sukari gulu gramu 150, asali gramu 50, maji ya wanga gramu 2, mafuta gramu 40.

Njia

1. osha mchele, uweke ndani ya maji kwa nusu saa, ondoa ganda la mzizi wa yungiyungi, kata vipande viwili, jaza matundu ya mzizi wa yungiyungi kwa mchele, ukijaza pigapiga mzizi wa yungiyungi ili mchele ujae vizuri kwenye mzizi wa yungiyungi.

2. tia mzizi wa yungiyungi ndani ya sufuria lenye maji, tia sukari gulu na ulichemshe kwa saa moja, lipakue na liache lipoe, likate kuwa vipande vipande venye unene wa 2 cm.

3. weka maji ya kuchemsha mzizi wa yungiyungi ndani ya sufuria, tia sukari gulu, asali, baada ya kuchemsha, mimina maji ya wanga, koroga koroga yapakue na kuweka kwenye vipande vya mzizi wa yungiyungi, mpaka hapo kitoweo hiki kiko tayari kuliwa.