Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2005-05-19 18:58:10    
Bw Faure Gnassingbe achaguliwa kuwa rais, hali ya Togo yatazamiwa kuwa tulivu siku hadi siku

cri

Mahakama ya katiba ya Togo tarehe 26 usiku ilitangaza kuwa, katika uchaguzi wa rais uliofanyika tarehe 24, mgombea kutoka Shirikisho la umma la Togo Bwana Faure Gnassingbe amepata kura nyingi za ndiyo na kuchaguliwa kuwa rais mpya wa Togo. Vyombo vya habari vinasema kuwa kama Bwana Faure ataweza kufuata ahadi ya kuunda serikali ya umoja wa kitaifa, basi hali ya Togo itatulia siku hadi siku.

Baada ya kujulikana kwa matokeo ya uchaguzi, Umoja wa uchumi wa nchi za Afrika ya magharibi ECOWAS ulitoa taarifa mara moja ukivitaka vikundi mbalimbali vya kisiasa vya Togo vipokee matokeo hayo. Wasimamizi wa uchaguzi mkuu wa Togo kutoka ECOWAS walisema kuwa, utaratibu kamili wa uchaguzi huo ulilingana na kigezo cha kimataifa, vikundi mbalimbali vya Togo vinapaswa kuheshimu matokeo ya uchaguzi na kubeba jukumu la kila upande, kulinda utulivu baada ya uchaguzi, na kuunda serikali mpya mapema iwezekanavyo. ECOWAS pia imeitaka jumuiya ya kimataifa iisaidie Togo kushinda taabu za hivi sasa. Katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa Bwana Kofi Annan alisema kupitia msemaji wake kuwa anaunga mkono juhudi zote zilizofanywa na ECOWAS na jumuiya nyingine za kikanda kwa ajili ya kulinda amani nchini Togo.

Baada ya kuambiwa matokeo ya uchaguzi, Bwana Faure alisema tena kwenye mkutano na waandishi wa habari kuwa anakarbisha wawakilishi wa vyama vya upinzani kujiunga na serikali ya umoja wa kitaifa. Aidha ametoa mwito kuvitaka vyama mbalimbali vya Togo kutupilia mbali uhasama na kufanya juhudi katika ujenzi na maendeleo ya taifa. Namna ya kushughulikia uhusiano wasiwasi na shirikisho la vyama vya upinzani, hii itakuwa changamoto ya kwanza inayoikabili Serikali mpya ya Bw Faure. Lakini wachambuzi wamedhihirisha kuwa, kama Bwana Faure atatekeleza kwa makini ahadi yake ya kuunda serikali ya umoja wa kitaifa, na akithubutu kusonga mbele na mchakato wa mageuzi ya kisiasa nchini humo, serikali mpya ya Faure inaweza kutambuliwa duniani, ambapo Bwana Faure atakuwa na uwezo wa kushughulikia uhusiano na shirikisho la vyama vya upinzani.

Wachambuzi wanaona kuwa, ingawa baada ya kufariki dunia kwa baba yake, Bw Faure aliyeshika madaraka ya urais chini ya uungaji mkono wa jeshi, na kupingwa na vyama vya upinzani na jumuiya za kikanda, baadaye alilazimika kujiuzulu chini ya mashikinizo ya nchini na nje. Lakini Bwana Faure alikuwa na kiwango cha juu cha elimu na mtizamo wa kisiasa wa kimaendeleo na yeye bado ni kijana, hizo ni sababu kubwa za kumwezesha kupata ushindi katika uchaguzi. Zaidi ya hayo, ECOWAS na jumuiya nyingine za kikanda kwa kweli zimemtambua Bw Faure kuchaguliwa kuwa rais, hivyo serikali mpya itakayoongozwa na Bwana Faure inatazamiwa kutambuliwa na jumuiya ya kimataifa.

Baada ya kumalizika kwa upigaji kura wa uchaguzi wa rais tarehe 24, chama tawala cha Togo na shirikisho la vyama vya upinzani vililaumiana, na wafuasi wa kila upande pia walifanya maandamano, na kusabiabisha mgogoro kati ya kikosi cha usalama cha Togo na wafuasi wa vyama vya upinzani, ambapo watu kadhaa waliuawa au kujeruhiwa. Tarehe 25 baada ya kufanya mashauriano ya dharura, Bwana Faure na kiongozi wa chama kikubwa cha upinzani Bwana Olumpio wamekubaliana kuwa, yeyote atayeshinda katika uchaguzi ataunda serikali ya umoja wa kitaifa inayowakilisha maslahi yai wananchi wote.

Idhaa ya Kiswahili 2005-04-27