Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2005-04-28 21:45:42    
Mbuga za majani nchini China

cri

Nchini China kuna hekta milioni 320 za mbuga za majani. Eneo hilo ni mara tatu ya eneo la mashamba, na linachukua nafasi ya kwanza katika maliasi ya ardhi nchini China. China ni moja ya nchi zenye maliasili kubwa ya mbuga dza majani duniani, ambayo inachukua nafasi ya tatu duniani baada ya Australia na Russia.

Mbuga za majani nchini China zinaanzia huko Mlima Daxing'anling, tambarare ya Songnen na uwanda wa juu wa Hulunbeier katika sehemu ya kaskazini mashariki ya China, kupitia uwanda wa juu wa Mongolia ya ndani na uwanda wa juu wa Huangtu, na kufikia sehemu ya kusini ya uwanda wa juu wa Qinghai-Tibet. Eneo hilo linaweza kugawanywa katika sehemu mbili, yaani sehemu ya kusini mashariki na ya kaskazini magharibi. Sehemu ya kaskazini magharibi ni malisho ya wanyama yenye eneo kubwa; na sehemu ya kusini mashariki ni sehemu yenye mchanganyiko wa mashamba, mbuga za majani na misitu, na eneo la mbuga za majani linachukua asilimia 30 ya sehemu hiyo.

Mbuga za majani nchini China ni za mbuga za ukanda wa fufutende, zinagawanywa katika aina tatu, yaani mbuga za sehemu zenye baridi kiasi, zenye joto kidogo na zenye urefu mkubwa kutoka usawa wa bahari na baridi kali. Kwa mujibu wa tofauti za hali ya ardhi, maji na joto, mbuga hizo pia zinaweza kugawanywa katika aina nne, yaani mbuga za kawaida, majangwa yenye majani, mbuga za majani na mbuga za vichaka.

Eneo la mbuga za majani za kawaida linachukua asilimia 37.4 ya eneo lote la mbuga za majani, zinaweza kugawanya katika aina tatu, yaani mbuga za tambarare, mbuga za milimani na mbuga za uwanda wa juu. Mbuga za tambarare ziko kwenye mkoa wa Mongolia ya Ndani na mikoa ya kaskazini mashariki; mbuga za milimani ziko katika sehemu za Mlima Tianshan, Mlima Kunlun na Mlima Qilian ambako ni malisho muhimu ya mifugo katika majira ya Autumn nchini China; na mbuga za uwanda wa juu ziko katikati ya uwanda wa juu wa Tibet, na baadhi ya sehemu mkoani Qinghai.

Majangwa yenye majani yanachukua asilimia 34.7 ya eneo lote la mbuga kaskazini mwa China. Eneo la majangwa ya tambarare linachukua asilimia 83 ya eneo lote la majangwa yenye nyasi, na mengi yao yako mkoani Xinjiang, Gansu, Ningxia na Mongolia ya ndani.

Eneo la mbuga zenye majani linachukua asilimia 27.9 ya mbuga nchini China. Pia linaweza kugawanywa katika aina tatu, yaani mbuga za tambarare, za milimani na za uwanda wa juu.

Asilimia 3.1 ya mbuga za vichaka ziko katika sehemu za tambarare na milima midogomidogo zenye urefu wa mita chini ya 500 kutoka usawa wa bahari, asilimia 42.6 ya mbuga hizo ziko katika sehemu za milimani zenye urefu wa mita kati ya 500 na 1200 kutoka usawa wa bahari, na asilimia 54.3 ziko katika sehemu zenye urefu wa mita zaidi ya 1200 kutoka usawa wa bahari.

Idhaa ya Kiswahili 2005-04-28