Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2005-04-29 20:24:55    
Kuhifadhi mandhari nzuri ya kimaumbile

cri

Wakati sehemu nyingi nchini China zinapojitahidi kuendeleza sehemu zenye vivutio vya utalii, mkoa wa Guangxi unazingatia zaidi hifadhi ya raslimali za utalii.

Bora kupunguzwa kwa idadi ya sehemu za utalii ili kuhifadhi mandhari nzuri ya kiasili ya Guilin. Mandhari ya milima na mto ya Guilin ni nzuri sana na inajulikana duniani, mkurugenzi wa idara ya hifadhi ya mazingira ya mji wa Guilin Bw. Tang Cheng alisema kuwa ili kuhifadhi vizuri mandhari nzuri ya kiasili ya Guilin, Guilin imefunga viwanda zaidi ya 30 vinavyotoa uchafuzi mwingi.

Mto Li ni kivutio kikubwa zaidi katika utalii wa Guilin, hivyo mji wa Guilin unatoa kipaumbele zaidi kwa hifadhi ya mto huo. Bw. Tang alisema kuwa mji wa Guilin umeweka kanuni za kudhibiti ujenzi wa majengo kwenye kando mbili za mto Li na kando mbili za barabara kati ya Guilin na Yangshuo; pamoja na kutunza usafi wa maji ya mto Li. Licha ya hayo walianzisha mradi wa kupanda miti kwenye sehemu inayopitiwa na mto Li ili kupandwa miti kwenye 99.3% ya ardhi ya kando mbili za mto. Hivi sasa, hata sifa ya maji yaliyotoka mji wa Guilin inafikia ngazi ya pili na tatu.

Naibu mkurugenzi wa idara ya utalii ya mji wa Guilin Bw. Peng Yuanli alisema kuwa Guilin imebuni mpango wa maendeleo ya utalii ya mji, ambao unazingatia zaidi hifadhi ya raslimali ya utalii ili kuleta maendeleo endelevu ya sekta ya utalii ya Guilin.

Aina ya mikoko ya huko inayojulikana kama "walinzi wa pwani", ni miti maalumu inayoota kwenye ardhi inayoingia chini ya maji ya bahari. Katika miaka ya karibuni miti ya aina hiyo inayositawi kwenye pwani ya kusini mashariki ya China iliharibiwa vibaya na binadamu, na kubaki kwa 30% hivi.

Mwanzoni mwa miaka ya 90 ya karne iliyopita, kampuni ya Huada ilipata haki ya matumizi ya pwani ya mji wa Fangcheng, lakini siku chache baada ya hapo serikali ya mji huo iligundua kuwa kwenye pwani ya sehemu hiyo imeota mikoko mingi, hivyo ikasimamisha matumizi ya ardhi ya sehemu hiyo na kuijenga kuwa bustani ya mikoko, badala ya sehemu hiyo, serikali iliipa kampuni ya Huada ardhi ya sehemu nyingine ili kujenga kiwanda.

Mwezi Machi mwaka jana, shirika la mazingira la Umoja wa Mataifa na Baraza la Miradi ya Hifadhi ya Mazingira Duniani viliuorodhesha mji wa Fangcheng kuwa sehemu ya kielelezo duniani, na msitu wa mikoko wa hekta zaidi ya 1,400 iliwekwa kwenye hifadhi za Shirika la Mazingira la Umoja wa Mataifa. Hivi sasa ndani ya msitu huo kuna ndege, samaki pamoja na chaza za aina mbalimbali. Hivi sasa sehemu hiyo imekuwa yenye mandhari nzuri ya mji huo na kutembelewa na watalii wengi wa nchini na kutoka nchi za nje.

Katika miaka ya 90 ya karne iliyopita, kulitokea wimbi la ujenzi wa majengo katika mji wa Beihai, hivi sasa ujenzi wa miradi 136 ulisimamishwa kwenye eneo la mita za mraba zaidi ya milioni 1.23 na kuwa kama kidonda cha mji huo, hususan ni kuwa nyumba ndogo ndogo za anasa zilizojengwa kwenye sehemu ya pwani ya "silver sand" zimeharibu mazingira ya mji na utalii.

Katika miaka ya karibuni mji wa Beihai ulianzisha harakati za kuhifadhi ufukwe wa bahari, hususan sehemu hiyo ya "silver sand". Mwezi May mwaka 2003, nyumba 38 zilizojengwa katika sehemu hiyo zilibomolewa ili kurejesha mazingira ya asili.

Hivi sasa, nyumba zaidi ya 100 za mji wa Beihai, ambazo ujenzi wake haujakamilika zimebomolewa, mji wa Beihai umekuwa wa kupendeza kama zamani. Meya wa mji huo Bw. Tang Chengliang alisema kuwa kushikilia kuboresha na kuhifadhi mazingira ya pwani kumehimiza maendeleo ya kasi ya sekta ya utalii ya mji huo, hivi sasa sekta ya utalii imekuwa moja ya nguzo nne za uchumi wa mji huo.

Naibu mkuu wa mkoa unaojiendesha wa kabila la wazhuang wa Guangxi Bw. Yang alisema kuwa mkoa huo umeweka mpango kamili wa maendeleo na kuagiza kuwa maendeleo ya sekta ya utalii lazima yaendane na maendeleo ya uchumi, siasa na utamaduni, hususan kuhifadhi raslimali ya utalii.

Mabadiliko ya mawazo yamechangia maendeleo ya utalii na ongezeko la pato la mkoa huo kutokana na utalii.

Idhaa ya Kiswahili 2005-04-29