Bunge la taifa la mpito la Iraq tarehe 28 lilipitisha orodha ya majina ya mawaziri wa baraza la serikali lililotolewa na waziri mkuu Ibrahim al-Jafari, hivyo serikali mpya ya Iraq imeundwa baada ya kutatua matatizo mengi miezi mitatu baada ya kufanyika uchaguzi mkuu wa nchi hiyo mwishoni mwa mwezi Januari mwaka huu.
Habari zinasema kuwa wabunge 185 kati ya wabunge 275 wa bunge la mpito waliipigia kura za ndiyo orodha hiyo ya majina ya mawaziri wapya. Baraza la serikali ya Jafari ina viti 36 vikiwa ni pamoja na vya manaibu mawaziri wakuu wanne na mawaziri 32, ambao 7 kati yao ni wanawake.
Waziri mkuu Jafari alitoa hotuba baada ya bunge la mpito kupitisha orodha hiyo ya majina, ikisema kuwa vyama vyote vya kisiasa nchini Iraq viwe vimeshiriki kwenye madaraka ya serikali mpya au la vina haki ya kushiriki mchakato wa kisiasa wa siku za mbele.
Kupitishwa kwa orodha ya majina iliyotolewa na waziri mkuu Jafari kunamaanisha kuwa serikali ya kwanza iliyochaguliwa na watu wa Iraq imeanzishwa baada ya kupita miaka zaidi ya 50 na kutatua suala la kuanzisha serikali mpya la vyama mbalimbali nchini humo. Hii ni hatua ya kwanza muhimu ya ujenzi mpya wa Iraq, ambayo itanufaisha kurejesha usalama na utulivu wa Iraq.
Majukumu muhimu ya Bw. Jafari na serikali mpya ni kutunga katiba rasmi ya nchi na kuufanyia upigaji kura katiba hiyo mpya. Kutokana na kuwa serikali mpya ya Iraq ni dhaifu tangu ilipoanzishwa, hivyo itakabiliwa na shida na changamoto nyingi.
Kwanza orodha ya majina iliyotolewa na Bw. Jafari haikukamilika, mazungumzo kuhusu uanzishaji wa serikali mpya bado yanaendelea na shughuli zilizobaki hivi sasa bado zina matatizo mengi. Hivi sasa kuna majina ya manaibu mawaziri wakuu na mawaziri watano, ambayo bado yanatakiwa kuthibitishwa. Baada ya baraza jipya kupitisha majina ya mawaziri wapya, baada ya waziri mkuu Jafari kutangaza majina ya mawaziri wa serikali, ujumbe wa madhehebu ya Suni ulitangaza kutoshiriki kwenye serikali mpya na kuondoa orodha ya majina ya wagombea wa dhehebu hilo kutokana na kuwa ombi lao la kupata viti vya uwaziri wa ulinzi na utumishi wa serikali lilikataliwa. Aidha, chama cha tatu kwa ukubwa chenye vitu 40 katika bunge kilitengwa nje ya serikali mpya, hali ambayo huenda italeta matatizo kwa shughuli za uendeshajiwa serikali.
Pili, Bw. Jafari na "Muungano wa Umoja" wana uhusiano mkubwa wa kidini na kijamaa, hivyo uendeshaji wa shughuli za serikali katika siku za baadaye huenda utawekewa vikwazo na Marekani. Vyombo vya habari vya kiarabu vimesema kuwa kuendelea polepole kwa mazungumzo kuhusu kuanzisha serikali mpya huenda kulihusika na uingiliaji kati wa Marekani. Waziri wa ulinzi wa Marekani Bw. Donaod Rumsfeld katikati ya mwezi huu alitembelea Iraq, wachunguzi wengi waliona kuwa moja ya lengo la safari yake ni kuingilia uteuzi wa waziri wa ulinzi na waziri wa mambo ya ndani, kwani nafasi hizo mbili ni muhimu sana kwa kuboresha mazingira ya usalama ya jeshi la Marekani lililoko nchini humo na kuhusika na mustakabali wa kuweko kwa jeshi la Marekani nchini humo.
Tatu, bado hakuna dalili la kuboreshwa kwa mazingira ya usalama nchini Iraq, na namna ya kutuliza mashambulizi ya kisilaha ni suala lingine gumu linaloikabili serikali mpya. Toka kufanyika uchaguzi mkuu wa Iraq, jeshi la polisi na wafanyakazi wa serikali wamekuwa shabaha ya mashambulizi ya wetu wenye silaha nchini Iraq.
Na nne, baada ya uchaguzi mkuu nchini Iraq hadhi ya kisiasa ya Suni, Shia na wakurd imekuwa na mabadiliko makubwa, kutelekezwa katika mambo ya siasa kwa dhehebu la Suni na kuwa na mgongano mkali kati ya dhehebu la Shia na wakurd kutokana na kukosa usawa katika ugawaji wa manufaa vilikwamisha mchakato wa siasa nchini Iraq kwa miezi zaidi ya mitatu.
Hata hivyo, kuanzishwa kwa serikali mpya ya Iraq kumepongezwa na watu nchini Iraq na jumuiya ya kimatafa. Watu wa nchi hiyo wanatarajia serikali mpya itaweza kutekeleza majukumu yake haraka iwezakanavyo na kuhimiza maendeleo ya mchakato wa kisiasa.
Idhaa ya Kiswahili
|