Mkutano wa mwaka 2005 wa kuthibitisha "Mkataba wa kutoeneza silaha za nyuklia" ulifunguliwa tarehe 2 huko New York katika makao makuu ya Umoja wa Mataifa. Kwenye mkutano huo wa wiki 4, wajumbe wa nchi 187 zilizosaini mkataba huo ikiwemo China watajadili malengo matatu makubwa ya kutoeneza silaha za nyuklia, kudhibiti silaha za nyuklia na kutumia kiamani nishati za nyuklia. "Mkataba wa kutoeneza silaha za nyuklia" ni mkataba muhimu kabisa wa kudhibiti zana za kijeshi za nyuklia duniani. Tarehe 12,Juni, mwaka 1968, Baraza kuu la Umoja wa Mataifa lilipitisha mswada wa mkakaba wa kuzuia kutosambaza kwa silaha za nyuklia uliobuniwa na Marekani na Urusi, tarehe 1 Julai mwaka huo, Urusi, Marekani na Uingereza zilisani mkataba huo kwa wakati mmoja. Tarehe 5 Machi, mwaka 1970 mkataba huo ulifanya kazi rasmi. Hivi sasa nchi wanachama 187 miongoni mwa 191 wa Umoja wa Mataifa zimesaini mkataba huo. Mkataba huo umewekwa kuwa, nchi zenye silaha za nyuklia zaahidi kutohamisha silaha zake za nyuklia kwa nchi zisizomiliki silaha za nyuklia, kutozisaidia nchi zisizomiliki silaha za nyuklia kutengeneza silaha za nyuklia; nchi zisizomilikia silaha za nyuklia zaahidi kutofanya utafiti wa kutengeneza silaha za nyuklia, kutopokea au kuomba kupata silaha za nyuklia; kuacha ushindani wa silaha za nyuklia, na kuhimiza upunguzaji wa silaha za nyuklia; kuweka zana za nyuklia za kiamani chini ya uhakikisho wa kimataifa wa shirika la nishati ya atomiki duniani, na kufanya ushirikiano wa kiteknolojia katika kutumia kiamani nishati za nyuklia. Mwaka huu ni mwaka wa 35 tangu uanze kazi "Mkataba wa kutoeneza silaha za nyuklia". Katika miaka 35 iliyopita, baadhi ya nchi zikifuata moyo wa mkataba huo, ziliacha mpango wa kuendeleza silaha za nyuklia, hayo ni mafanikio yaliyopatikana katika utekelezaji wa mkataba huo. Lakini wakati huo huo, mkataba huo unakabiliwa na changamoto kubwa. Suala la nyuklia la Iran na suala la nyuklia la peninsula ya Korea yamefuatiliwa sana na jumuia ya kimataifa; Marekani na Russia zinazomiliki nusu ya ile ya jumla ya vichwa vya makombora ya nyuklia duniani zinafanya polepole upunguzaji wa silaha za nyuklia; Israel, India na Pakistan mpaka sasa bado hazijajiunga na mkataba huo; Korea ya kaskazini ilitangaza kujitoa kutoka mkataba huo mwaka 2003. Hivi sasa hali ya utatanishi umetokea katika utekelezaji wa "Mkataba wa kutoeneza silaha za nyuklia", hivyo ingawa mkutano huo umefunguliwa, lakini ajenda rasmi bado hazijathibitishwa kutokana na migongano mikubwa kati ya nchi mbalimbali. Katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa alitoa hotuba kwenye ufunguzi wa mkutano huo, akizitaka nchi mbalimbali zilizosaini mkataba huo zichukue hatua halisi kutekeleza "Mkataba wa kutoeneza silaha za nyuklia" na kubeba jukumu kwa pamoja ili kuanzisha utaratibu wa dunia nzima wa kupunguza tishio la silaha za nyuklia. Bwana Kofi Annna alisema kuwa, katika zama tulizo nazo jumuia za kimataifa zinategemeana na kuwasiliana, tishio dhidi ya nchi moja ndiyo tishio kwa nchi zote, kulinda usalama wa dunia ni jukumu la pamoja la nchi zote duniani. Bwana Annan alisema kuwa, kupunguza migogoro ya kijeshi ya kikanda na kuimarisha imani ya nchi mbalimbali kwa utaratibu wa usamala wa pamoja uliopendekezwa na Umoja wa Mataifa ni njia mwafaka ya kuepusha usambazaji wa silaha za nyuklia. Kwenye ufunguzi wa mkutano huo, katibu mkuu wa shirika la nishati ya atomiki duniani Bwana Mohamed el Baradei alitoa hotuba akiitaka jumuia ya kimataifa irekebishe utaratibu wa kimataifa wa kuzuia usambazaji wa nyuklia, ili kuhakikisha "Mkataba wa kutoeneza silaha za nyuklia" unatekelezwa kwa kufuata wakati na kuimarisha madaraka ya ukaguzi, udhibiti na usimamizi ya shirika la nishati ya atomiki duniani.
Idhaa ya kiswahili 2005-05-03
|