Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2005-05-04 20:50:45    
Serikali ya mpito ya Iraq yaapishwa

cri

Serikali ya mpito ya Iraq iliapishwa tarehe 3 huko Bagdad, hii imeonesha kuwa serikali ya kwanza ya Iraq iliyochaguliwa na raia imeanzishwa rasmi, na mchakato wa ukarabati wa kisiasa wa Iraq umepiga hatua kubwa.

Sherehe ya kuapishwa ilifanyika kwenye kituo cha mkutano kilichoko ndani ya "sehemu ya kijani" ya Bagdad. Serikali ya mpito ya Iraq imewekwa nyadhifa 37 pamoja na wadhifa wa waziri mkuu, Shirikisho la umoja wa Iraq la madhehebu ya Shiya lililopata ushindi katika uchaguzi mkuu uliofanyika mwishoni mwa mwezi Julai mwaka jana limepata nyadhifa 15, na Shirikisho la vyama la wakurd limepata nyadhifa 7. Siku hiyo mawaziri walioapishwa walikuwa 28 tu. Nyadhifa za manaibu mawaziri wakuu na nyadhifa za mawaziri watano pamoja na waziri wa ulinzi wa taifa na waziri wa mafuta bado hazijathibitishwa.

Kituo cha televisheni cha al Jazeera kiliripoti kuwa, siku kadhaa zilizopita, vyama vikubwa kwenye bunge la mpito la Iraq vilifanya mazungumzo na kuwa na makwaruzano makali kuhusu wateuzi wa nyadhifa hizo, ingawa Shirikisho la umoja la Iraq tarehe 2 liliafikiana na madhehebu ya Sunni kuhusu suala la kuundwa kwa baraza la mawaziri, na kukubali kuyapatia madhehebu ya Sunni nyadhifa 6 za mawaziri pamoja na wadhifa wa naibu waziri mkuu na waziri wa mambo ya ulinzi, lakini Shirikisho la vyama la wakurd bado lina maoni tofauti juu ya mteuzi wa waziri wa ulinzi wa madhehebu ya Sunni. Hivyo kabla ya kufanyika kwa sherehe ya kuapishwa, vyama mbalimbali havijafikia maoni ya pamoja, na makamu wa rais wa Iraq ambaye pia ni kiongozi wa madhehebu ya Sunni Bwana Ghazi al Yawar hakuhudhuria sherehe ya kuapishwa kwa serikali mpya siku hiyo. Zaidi ya hayo, waziri mkuu wa serikali ya muda ya zamani Bwana Iyad Allawi ambaye hakupewa wadhifa katika serikali mpya pia hakuhudhuria sherehe hiyo.

Vyombo vya nchi za kiarabu vimeeleza kuwa, hali isiyo ya masikilizano kwenye sherehe ya kuapishwa kwa serikali mpya imeonesha kuwa, vyama mbalimbali vya Iraq bado vina migongano mingi kuhusu ugawaji wa nyadhifa za mawaziri. Madhehebu ya Shia na wakurd wote wanakubali waziri wa ulinzi wa taifa atateuliwa na madhehebu ya Sunni, lakini wote wanapinga mteuzi huyo asiteuliwa kutoka kwa wanachama wa chama tawala cha zamani cha Arab Baath Socialist Party. Aidha, mteuzi wa waziri wa ulinzi unahusiana na usalama wa jeshi la Marekani nchini Iraq, Marekani haiwezi kukaa kimya, ndiyo maana, kuundwa kwa baraza la mawaziri la Iraq kumeongezwa ugumu.

Jukumu kuu la serikali inayoongozwa na Bwana Ibrahim al Jaafari ni kutunga katiba mpya kabla ya tarehe 15 Agosti mwaka huu, na kufanya maandalizi ya uchaguzi mkuu rasmi unaotazamiwa kufanyika mwishoni mwa mwaka huu. Ili kuhakikisha mchakato wa kisiasa wa Iraq unafanyika kwa mpango uliowekwa, Jaafari na serikali yake mpya bado wanakabiliwa na taabu nyingi na changamoto kubwa. Tokea wiki iliyopita bunge la mpito la Iraq kupitisha orodha ya mawaziri, hali ya usalama nchini Iraq inazidi kuwa mbaya, mashambulizi ya kimabavu yaliyotokea siku za karibuni yamesababisha vifo vya watu zaidi ya 170. Aidha, ingawa serikali mpya imeanzishwa, lakini suala la kuundwa kwa baraza la mawaziri bado halijatatuliwa kikamilifu. Kwa kukabiliwa na matatizo kadha wa kadha, Bwana Jaafari ameahidi kuwa serikali mpya itayapa madhehebu ya Sunni muda mrefu zaidi mpaka ateuliwe waziri wa ulinzi atakayekubaliwa na wairaq wengi; itawateua mawaziri wa mafuta na umeme siku mbili zijazo; na pia itaanzisha makao makuu ya kuongoza mapambano dhidi ya wazushaji wa mashambulizi ya kimabavu.

Wachambuzi wamedhihirisha kuwa, serikali mpya ya Jaafari bado inakabiliwa na jukumu kubwa lenye taabu katika kukabiliana na matatizo na changamoto mbalimbali na kuhakikisha mchakato wa kisiasa unasonga mbele bila vikwazo.

Idhaa ya kiswahili 2005-05-04