Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2005-05-09 17:58:27    
Mchoraji mashuhuri Bi. Zhang Fuying kisiwani Taiwan

cri

Siku hizi maonesho ya picha za mchoraji mkubwa Bi. Zhang Fuying anayetoka kisiwani Taiwan yanafanyika katika jumba la makumbusho la taifa mjini Beijing. Bi. Zhang Fuying sio tu mchoraji mkubwa, naye pia ni msanii mwenye ukarimu mkubwa wa kuwasaidia wanafunzi maskini wa sanaa na mwenye juhudi za kuchangia maingiliano ya kiutamaduni kati ya China bara na kisiwa cha Taiwan. Bi. Zhang Fuying ana umri wa miaka 70, anaonekana mwemba na mfupi, lakini mchangamfu. Alizaliwa kisiwani Taiwan, kutokana na umaskini tokea utotoni alikuwa analazimika kuhangaika na chakula cha familia. Alikuwa anapenda kuchora picha, anataka kujifunza shuleni. Ili kutimiza tumaini hilo alijitahidi kulimbikiza ada ya shule. Alipokumbuka maisha ya utotoni alisema,

"Wakati huo hata chakula kilikuwa ni shida, niliwezaje kusoma shuleni? Kufanya kazi ya sulubu sina nguvu, basi nilikwenda kwenye studio moja kujifunza kupiga picha, baada ya nusu mwaka nilijitokeza kuwa mwalimu, nilianza kuishi kwa kujitegemea, na baadaye nianza kupiga picha za mandhari, vivyo hivyo nilizama katika usanii wa picha."

Bi. Zhang Fuying alipokuwa na umri wa miaka 14 alifanya maonesho ya picha zake za kamera na alipata tuzo mara nyingi katika maonesho nchini Japan, Marekani na Ujerumani.

Bi. Zhang Fuying alipokuwa na umri wa miaka 18 alianza kujifunza uchoraji wa picha. Tokea hapo alikuwa ameingia kabisa katika uchoraji bila kujali uchovu. Alisema,

"Uchovu, shida na ufukara, yote hayo sikuyajali. Nilipochora picha hata kelele za watu mia kadhaa haziwezi kunipotezea akili kutokana na utulivu wa moyo."

Baadaye alijifunza uchoraji kwa mchoraji mkubwa wa picha za Kichina Bw. Huang Junbi. Mchoraji huyo licha ya kuwa ni mchoraji mkubwa wa mtindo wa jadi naye pia alipokea uchoraji wa Kimagharibi. Bi. Zhang Fuying alijifunza kwake zaidi ya miaka 30 na amepata usanii mkubwa kutoka kwake. Aliwahi kufanya maonesho ya picha zaidi ya mara mia moja. Bi. Zhang Fuying anaona kuwa ni kwa kudhibiti usanii wa mtindo wa jadi tu wa Kichina ndipo mchoraji anapoweza kujipatia mtindo wake mwenyewe. Alisema,

"Kwa kweli naheshimu sana wachoraji wa kabla yetu, kwa sababu wameweka msingi mzuri wa uchoraji. Baadhi ya watu wanapinga, wanaona umepitwa na wakati, lakini naona kuwa njia hiyo ambayo wachoraji wa zamani waliipitia vizuri, inatupasa tuipitie kwa mara kadha wa kadha ndipo tunapoweza kujipatia mtindo wetu wenyewe. Mwalimu wangu Huang aliniambia, 'Uchoraji wa mtindo wa Kichina unapofikia kiwango fulani inakupasa ujifunze kutoka kwa mandhari ya maumbile.' Kwa hiyo lazima nianzia uchoraji wangu kutoka kwa mtindo wa jadi hadi kujiendeleza kwa kuchora mandhari ya maumbile."

Kutokana na hayo Bi. Zhang Fuying alikuwa na hamu kubwa ya kuja China bara angalie uzuri wa maumbile ya milima na maji. Alisema,

"Mandhari ya maumbile ni mazuri kweli katika China bara hata nashindwa kuyaeleza. Kuna watu waliowahi kuniomba niende nao barani Ulaya, lakini sikuenda. Niliwaambia, nataka kwenda China bara, kwani mandhari ya huko ni mazuri kuliko sehemu zote duniani. Kila mara nakaa katika China bara siku tatu, lakini lazima nijinyime nusu siku ili niende kwenye Ukuta Mkuu nikitulia huko kufurahia majabali yaliyo pande mbili za ukuta huo."

Mwaka 1990 kwa mara ya kwanza Bi. Zhang Fuying alikuja China bara, na mwaka 1992 picha zake zilioneshwa China bara na mwaka 1999 alifanya maonesho binafsi ya picha zake katika Makumbusho ya Taifa ya China, picha zilizooneshwa zilikuwa karibu mia moja kwenye maonesho. Katika miaka ya karibuni amekuwa mbioni kati ya pande mbili za China bara na kisiwa cha Taiwan akichangia maingiliano ya utamaduni.

Bi. Zhang Fuying kwa fedha zake alianzisha "mfuko wa Bw. Huang Junbi wa kusaidia elimu na utamaduni", lakini maisha yake ni ya kawaida kabisa, alisema bei ya mavazi yake aliyovaa haizidi zaidi ya yuan 12. Alitumia pesa alizopata kutokana na mauzo ya picha zake kuwasaidia wanafunzi maskini wa sanaa. Bi. Zhang Fuying alisema,

"Nawasaidia wanafunzi masikini wa sanaa kwa pesa nilizojinyima maishani mwangu, lakini nawasaidia kwa jina la mwalimu wangu Hung Junbi kwa ajili ya kumheshimu na kumkumbuka. Ni tumaini langu maishani mwangu kuihudumia jamii kadiri niwezavyo."

Wasikilizaji wapendwa, mlikuwa mkisikiliza maelezo kuhusu mchoraji mkubwa wa picha kisiwani Taiwan, Bi. Zhang Fuying. Kipindi hiki kinaishia hapa. Shukrani kwa kuwa nasi. Kwaherini.

Idhaa ya kiswahili 2005-05-09