Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2005-05-09 21:19:48    
Kukumbuka historia na kuanzisha mustakabali mzuri

cri
    Rais Hu Jintao wa China jana katika ofisi ya ubalozi wa China nchini Russia alionana na askari wazee waliowahi kushiriki katika vita ya kupinga mashambulizi nchini China na vita vya kulinda taifa nchini Urusi, pamoja na wawakilishi wa wafiwa wa askari wazee, na kutoa hotuba. Bw. Hu Jintao alitoa heshima kwa wazee hao na kufikisha salamu za kirafiki za watu wa China kwa watu wa Russia, pia aliwaeleza watu wa nchi mbalimbali nia ya China ya kupenda amani na kutoa wito wa kulinda amani iliyopatikana kwa shida kubwa na kuanzisha mustakabali mzuri wa binadamu.

    Vita ya pili ya dunia ni vita kubwa kabisa katika historia ya binadamu, ambayo ilileta hasara kubwa na kusababisha watu wengi kupoteza maisha yao. Watu karibu bilioni 2 wakiwemo wa nchi zaidi ya 60 zikiwemo za China na Urusi ya zamani walikumbwa na vita hiyo. China ilikuwa uwanja muhimu wa vita vya kupinga mashambulizi ya Japan. Katika vita hiyo iliyodumu kwa miaka 8, watu wa China walitoa mchango mkubwa katika kupigania ushindi wa vita dhidi ya ufashisti. Urusi ya zamani ilikuwa uwanja muhimu wa kupinga mashambulizi ya ufashisti wa Ujerumani. Katika vita hivyo vikatili, watu wa China na wa Urusi walipigana vita bega kwa bega na kujenga urafiki mkubwa katika vita hivyo vya kufa na kupona. Mapigano ya China ya kupinga mashambulizi ya Japan yalipofika katika wakati muhimu, Jeshi Jekundu la Urusi liliingia kwenye uwanja wa vita wa sehemu ya kaskazini mashariki ya China na kushirikiana na jeshi na watu wa China katika mapigano ya kupinga mashambulizi ya Japan na kutoa msaada mkubwa kwa watu wa China kupata ushindi katika vita.

    Katika siku ya leo baada ya kupita miaka 60, rais Hu Jintao wa China amekutana na askari wazee waliowahi kushiriki kwenye mapambano ya kupinga mashambulizi ya Japan nchini China na kukumbuka historia na urafiki. Bw. Hu Jintao aliwafikishia wazee hao heshima na urafiki wa watu wa China. Alisema, "Wengi wenu mlishiriki kwenye vita ya kupinga mashambulizi ya Japan ya sehemu ya kaskazini mashariki ya China na kutoa mchango mkubwa. Nawashukuru sana. Katika vita hivyo askari wengi wa Jeshi Jekundu la Urusi walipoteza maisha yao, ushujaa wao utakumbukwa daima na watu wa China."

    Historia ni kama kioo kwa hali halisi ya hivi sasa, na pia ni kitabu kizuri cha kiada. Bw. Hu Jintao alisema kuwa kukumbuka mafunzo ya historia na kuanzisha mustakabali mzuri ni chaguo sahihi la binadmau kwa historia. Alisema, "Lengo la kukumbuka historia na kutosahau mambo yaliyopata, ni kwa ajili ya kuthamini amani na kuanzisha mustakabali mzuri. Nia yetu ya kuadhimisha ushindi wa vita vya kupinga ufashisti, ni kuthamini amani iliyopatikana kwa shida kubwa na kutoacha janga la vita lirudi tena duniani na kufanya watu duniani waishi kwa usalama."

    Bw. Hu Jintao alisema kuwa China itashikilia amani, maendeleo na ushirikiano, kufuata njia ya amani na maendeleo, kulinda amani ya dunia na kujitahidi pamoja na watu wa dunia kujenga dunia yenye amani, ustawi na maelewano, pia anatarajia watu wa China na Russia wadumishe urafiki wao na kujitahidi kuanzisha mustakabali mzuri wa binadamu.

Idhaa ya Kiswahili