Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2005-05-10 16:36:58    
Hatua za Marekani na Umoja wa Ulaya zaenda kinyume na biashara huria

cri

Hivi karibuni umetokea mkwaruzano kati ya Marekani na Umoja wa Ulaya kwa upande mmoja na China kwa upande mwingine kuhusu biashara ya nguo. Baada ya kuondoa kiwango cha biashara ya nguo duniani mwanzoni mwa mwaka huu, Marekani na Umoja wa Ulaya zinadai kuwa zitachukua hatua za kudhibiti kiwango cha biashara ya nguo ya China kutokana na ongezeko la biashara hiyo ya China katika miezi kadhaa tu ya mwanzo wa mwaka huu. Msimamo huo unapingwa na China na pia nchi kadhaa za Umoja wa Ulaya na baadhi ya wataalamu wanaotetea haki.

Mwishoni mwa mwezi Aprili, kwa mujibu wa takwimu za biashara ya nguo ya China katika robo ya kwanza ya mwaka huu iliyotolewa na nchi wanachama wa Umoja wa Ulaya, mwanakamati wa Kamati ya Biashara ya Umoja wa Ulaya Bw. Peter Mandelson alisema kuwa ongezeko la aina tisa za nguo za China katika nchi hizo ni la haraka na limezidi kiwango cha hatari kilichowekwa na kamati hiyo. Alisema kuwa ataiomba kamati yake ifanye uchunguzi wa hali hiyo ili kamati yake ichukue hatua. Kabla ya hapo, wizara ya biashara ya Marekani tarehe 4 pia ilitangaza kuwa itafanya uchunguzi katika muda wa siku 90 kuhusu aina tatu za nguo za shati, suruali, nguo za ndani za nyuzi za kemikali ili kuhakikisha kama bidhaa hizo zinavuruga soko la Marekani.

Katibu mkuu wa WTO Bw. Supachai Panitchpakdi siku chache zilizopita alipohojiwa na waandishi wa habari alisema, anatumai kuwa nchi za Marekani na Umoja wa Ulaya zitafanya uchunguzi kwa muda usiopungua mwaka mmoja ili kubaini kiwango kinachofaa. Katibu mkuu wa zamani wa kamati hiyo Bw. Ruggiero alisema, China haina dhamana yoyote kuhusu tukio hilo. Kadhalika, wagombea wawili wa ukatibu mkuu ambao mmoja alikuwa ni mwanakamati wa kamati ya biashara ya Umoja wa Ulaya, Pascal Lamy, na mwingine alikuwa balozi wa Uruguay katika WTO Bw. Castillo pia wanapinga moja kwa moja hatua hizo za Marekani na Umoja wa Ulaya.

Tarehe mosi Januari mwaka huu "katiba ya biashara ya nguo" ilifutwa kama ilivyopangwa, ongezeko la biashara ya nguo kwa nchi zinazoendelea kama China yenye maendeleo ya uchumi ni jambo la kawaida, na ni hali ya kawaida pia katika mchakato wa kutoka mfumo wa kusimamia kiwango cha biashara kinachopotoka hadi mfumo wa biashara huria. Wataalamu wengi wanaona kuwa ongezeko hilo ni la muda tu, na hatua za kudhibiti biashara ya nguo ya China sio tu itaharibu maslahi ya China, bali pia itawaletea hasara wafanyabiashara wa kimataifa, wafanyabiashara wa rejareja na wateja wa Marekani na Umoja wa Ulaya. Aidha, China haina dhamana kuhusu ongezeko la biashara hiyo, bali nchi zilizoendelea hazikufuata "mkataba wa biashara ya nguo" ambao unataka kuondoa kiwango cha biashara kwa vipindi katika muda wa miaka 10, na zinabakiza kiwango cha 70% mpaka dakika ya mwisho na kuathiri vibaya marekebisho ya uzalishaji wa mashirika.

Ni jukumu la WTO kuangalia mambo kwa mtazamo wa mbali na kuleta uwiano wa haki na wajibu. Tokea ijiunge na WTO China inatekeleza vilivyo wajibu wake. Kwa hiyo haifai kusema kuwa China imepata faida kubwa kwa biashara tu ya nguo. Waziri wa biashara wa China Bw. Bo Xilai aliwahi kufanya hesabu, akisema kuwa China haiwezi kumudu kununua ndege ya A 380 mpaka iuze mashati milioni 800. Kama nchi zilizoendelea zinatetea biashara huria ya bidhaa za mashirika yenye nguvu na kuchukua hatua za udhibiti kwa nchi zinazoendelea zenye mashirika machache yenye nguvu, msimamo kama huo wenye vigezo tofauti utaharibu msingi wa biashara huria. Maofisa wa Wizara ya Biashara ya China wanasema kuwa China inapinga hatua zinazochukuliwa na Marekani na Umoja wa Ulaya na inatetea kutatua mkwaruzano huo kwa mazungumzo.

Idhaa ya kiswahili 2005-05-10